SoC02 Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini

SoC02 Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Andiko langu litakuwa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza itakuwa ni utangulizi hapa nitaelezea maana ya mikataba na faida ya mikataba, sehemu ya pili nitaelezea mikataba iliyoleta migogoro au sintofahamu katika mambo mbali mbali nchini. Sehemu ya tatu itakuwa ya mwisho hapo nitatoa ushauri pamoja na maoni yangu.

MKATABA
Mkataba, kwa ufafanuzi rahisi zaidi, ahadi inayotekelezeka kwa sheria. Ahadi inaweza kuwa kufanya jambo fulani au kutofanya jambo fulani. Uundaji wa mkataba unahitaji idhini ya pande zote ya watu wawili au zaidi, mmoja wao kwa kawaida akitoa ofa na mwingine akikubali. Iwapo mmoja wa wahusika atashindwa kutimiza ahadi, mwingine ana haki ya kusuluhishwa kisheria.

Sheria ya mikataba inazingatia maswali kama vile mkataba upo, nini maana yake, kama mkataba umevunjwa, na ni fidia gani inastahili kulipwa mhusika, (Maana kutoka Britannica).

Mikataba ina faida kama, kuonyesha makubaliano ya watu wawili au zaidi pamoja na mashahidi. Husaidia kupunguza migogoro sheria ikisimamiwa vizuri na Husaidia vyombo vya kisheria katika kufanya maamuzi iwapo kutatokea sintofahamu katika mkataba husika, pia huhakikisha ulinzi wa makubaliano husika. Yote hayo huchochea maendeleo, uwajibikaji, na mabadiliko katika jamii zetu.

IFUATAYO NI BAADHI YA MIKATABA ILIYOZUA UTATA KATIKA UTENDAJI NCHINI

1. MKATABA WA WANUFAIKA WA MKOPO WA ELIMU YA JUU NA BODI YA MIKOPO(heslb).

Mkataba huu wa bodi ya mikopo ulieleza kiasi ambacho kingerejeshwa na mnufaika wa mkopo kuwa ni asilimia 8 lakini utawala wa Hayati John Pombe Magufuli ulibatilisha na kuongeza marejesho yawe kwa asilimia 15. Ongezeko hilo la makato limepelekea wafanyakazi kulalamikia japo hawakufika katika vyombo vya sheria lakini liliwaathiri kiuchumi. CAG alithibitisha hili alisema:-

"Nilibaini upungufu huu unatokana na sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyoongeza makato ya wanufaika kutoka asilimia nane hadi 15 ya mshahara,” amesema CAG kwenye ripoti yake.(Nukuu ya CAG Charles Kichere, Mwananchi).

2. MKATABA WA MCHEZAJI BERNARD MORRISON NA TIMU YA MPIRA YANGA SC.
Kwa wapenda mpira wote nchini hakuna asie kumbuka hili. November 22, 2021 Mahakama ya Usuluhishi katika Michezo CAS, Ilitoa maamuzi katika kesi ya mchezaji Morrison na Timu ya Yanga kwa kutupilia mbali rufaa ya timu ya yanga kwa kuona dosari zilizopo kwenye mkataba wa Yanga walioupeleka kule CAS.

Screenshot_20211122-170056_WPS Office (1).jpg

Picha maamuzi ya CAS baina ya Morrison vs Yanga. (Picha kutoka mtandaoni).

3. MKATABA WA MWANAMUZIKI RICH MAVOKO NA WASAFI.
Mkataba wa mwimbaji wa bongo fleva Rich Mavoko na lebo ya Wasafi nao uliingia katika mgogoro. Kwa maana mwimbaji Rich Mavoko alitambua kuwa mkataba ule ulidhamiria kuathiri taaluma yake pamoja na mapato yake. Kwa msaada wa (BASATA) Baraza la Sanaa Tanzania mwimbaji Rich Mavoko alishinda kesi na mkataba ukavunywa. (Taarifa zilitangazwa mitandaoni)
Rich.jpg

Rich mavoko akisaini kujiunga na WCB ya diamond platnumz. (Picha kutoka mtandaoni)

4. MIKATABA BAINA YA WAMILIKI WA VIWANDA NA WAFANYAKAZI WA VIWANDA.
Mikataba inayotolewa na wamiliki wa viwanda nchini kwa wafanyakazi wa viwandani hususani wale wa kazi ndogo ndogo kama kupanga bidhaa, kupakiza bidhaa, kufanya usafi, kushona mabox na mifuko. Mikataba wanayopewa kundi hili huwa haina msaada kwa wafanyakazi. Haiwalindi, muda wowote hata bila kosa wanaweza kufukuzwa au kutolipwa. Mikataba hii kwenye viwanda ni bora vyama vya wafanyakazi pamoja na serikali ikaitazama kwa faida ya wote.

5. MIKATABA YA SHULE NA HOSPITALI ZA MASHIRIKA BINAFSI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WAKE.
Mikataba inayotolewa na mashirika ya shule binafsi nchini kwa baadhi sio yote haipo sawa. Zipo shule nyingi walimu wanafundisha kwa kukubaliana kwa njia ya mdomo bila kupeana mkataba unaoeleweka. Jambo hili ni hatari kwa mwajiriwa kwa maana anaweza dhulumiwa au kufutwa kazi bila taarifa ya kueleweka. Katika hospitali za binafsi baadhi nazo zinafanya hivyo hivyo.

6. MIKATABA YA MAUZIANO NA SHUGHULI ZINGINE NDOGO NDOGO KATIKA JAMII ZETU.
Mikataba inayotolewa katika mauziano mbali mbali kwenye jamii zetu hususani katika kuuziana ardhi, mikataba mingi ina mapungufu yanayopelekea kuibuka kwa migogoro. Zipo kesi nyingi za migogoro ya ardhi zilizosababishwa na mikataba mibovu. Zipo mali nyingi zimewekewa zuio na mahakama kutokana na sintofahamu iliyopo katika mauziano kwenye mikataba husika. Jambo hili ni kubwa katika jamii zetu.

7. MIKATABA KWENYE ASASI ZA MIKOPO BAINA YA MKOPAJI NA WATOA MIKOPO.
Mara nyingi katika kukopa wengi wanashindwa kusoma na kuelewa mikataba husika. Jambo hili huzua simtofahamu au migogoro kwenye kufanya marejesho. Ni vyema mkopaji na mkopeshaji wakakaa pamoja na kuandaa mkataba utakao bainisha hatua zote za kufanya ili kupata mkopo na njia zitakazo tumika kurejesha mkopo. Na sio mkopeshaji anaandaa mwenyewe mkataba na kuutumia bila kumsikiliza mkopaji. Jambo hili likisimamiwa litasaidia kupunguza kufirisiana katika jamii zetu. Kwa maana mlipaji akijieleza na kutoa mapendekezo yake yanayoeleweka na kukubalika katika mkataba yatasaidia kuondoa migogoro.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI, JAMII NA MASHIRIKA BINAFSI KUHUSIANA NA MIGOGORO YA KIMIKATABA.

1. Elimu itolewe kwa jamii kuhusu umuhimu wa mikataba kwenye mauziano, makubaliano na maamuzi. Jamii zetu zielimishwe kwa kuelezwa umuhimu uliopo iwapo mambo yakifanyika kwa mikataba inayozingatia taratibu za kisheria. Hii itasaidia kuondoa migogoro.

2. Mikataba iwe moja ya mada(Topic) katika mitaala yetu ya elimu nchini. Wanafunzi wetu nchini wafundishwe kuhusu mikataba kwenye somo la uraia(civics) na General Studies kwa advanced level. Hii itasaidia kuandaa kizazi kinachojua misingi na taratibu za mikataba. Dunia ya leo mambo mengi huendeshwa kwa mikataba.

3. Vyombo vya sheria kama mahakama, polisi na serikali za mitaa vitoe ushirikiano zaidi inapohitajika kwa wananchi. Wananchi wanapohitaji kutambua hatua za kufuata ili kufanya mikataba baina yao au na taasisi yoyote ni vema vyombo vya sheria vikawa tayari kuwa patia mwongozo.

4. Serikali ifuatilie mikataba inayotolewa na mashirika binafsi kwa wafanyakazi wake. Serikali yetu pia ifuatilie kwa kina mikataba wanayopewa wananchi wake kwenye viwanda, shule binafsi, hospitali binafsi ili itambue na kuona je mikataba hiyo inaeleweka na inakidhi vigezo vya kimikataba.

5. Viongozi waache kubatilisha mikataba kwa mihemko bali wafuate mashauriano na maridhiano ya kisheria kwa faida ya wote. Viongozi wetu wakifuatilia mikataba ni jambo jema ila wakibatilisha mikataba kwa mihemko na sio kwa kuzingatia sheria itazua migogoro. Mfano mkataba wa wanufaika wa bodi ya mikopo, uongozi wa awamu ya tano haukutumia sheria kuongeza makato kutoka asilimia 8 hadi 15.
 
Upvote 27
Hapana mkuu. Kwanini.?
mimi nafanya kazi sekta binafsi na kiukweli kama ulivyo sema kwenye bandiko lako mikataba kwenye sekta binafsi inaminya sana wafanyakazi...nikadhani wewe ni mwanasheria nikupe kisa cha kampuni yangu unisaidie jinsi ya kukabiliana nao.
 
Nishawahi kufanya kazi huko ndio maana. Nilipewa mkataba wa mdomoni aisee yalinikuta ndio maana mkuu.

Lete kisa chako mkuu tusaidiane
 
Na kura yako muhimu sana mkuu hapo juu.
 
Nishawahi kufanya kazi huko ndio maana. Nilipewa mkataba wa mdomoni aisee yalinikuta ndio maana mkuu.

Lete kisa chako mkuu tusaidiane
mimi nafanya kazi kwenye kampuni ambayo inadai inalipa malipo ya overtime mshahala wangu kwa mwenzi basic ni 150,000/=

kuna baadhi ya overtime ninapunjwa haswa overtime ya siku za siku kuu ambapo ukichukua ile principle ya kukokotoa malipo ya saa 150000/4.333*45=769.20

hivyo kwa kila lisaa nalipwa 769.20

sheria ya ajira inamtaka muajiri kunilipa 200%*769.2*masaa nitakayo fanya kazi siku za sikuku.

kwenye kampuni yetu sisi huwa tunaingia masaa 12... hapo ukichukua 200%769.2*12=18460.8 ila wao wanalipa elfu 12,000/= tu...kwa kila sikukuu badala ya elfu 18....je hapo nikitaka kuwashitaki naweza kudai fidia...?

kingine huwa awapeleki mafao yetu ya nssf kwa wakati...hali inayopelekea sisi kukosa huduma za afya za bure zinazotolewa na nssf...hapo napo hakuna kafidia kweli...?
 
Pole mkuu. Hapo inakubidi ukutane na mwanasheria umuelezee hayo yote na pia vyama vya wafanyakazi kama vinaweza kukusaidia. Sijasomea sheria hivyo siwezi kwenda deep sana kama mtu wa sheria. Naweza kusema kutokufuatiliwa kwa mikataba ya mashirika binafsi na wafanyakazi wake kiukweli inawatesa wafanyakazi. Kama hivyo. Kazi masaa 12 lakini unalipwa 150,000/= na hapo haina kuongezwa na hata wakiongeza naimani ni hela kiduchu saana ambayo bado ndogo sana
 
Mimi najua waandishi wote ni wale ambao wanapenda kazi yao ya uandishi. Sio watu wa maslahi, bali pia wanapenda kazi yao.
Shukrani mkuu kwa kumpa maneno yabusara huyo jamaa. 👏🏻👏🏻
 
Mimi najua waandishi wote ni wale ambao wanapenda kazi yao ya uandishi. Sio watu wa maslahi, bali pia wanapenda kazi yao.
Pamoja mkuu. Tunakuomba utuongezee madini humu. Afu wewe mkongwe kwenye jukwaa hili. Hivyo wazee kama nyie hamkosi madini. Kwa ila maana ya jungu kuu halikosi ukoko
 
Unataka kuniambia vyombo vya serikali, mahakama, bunge, na raisi hawatoi ushirikiano kwa wananchi kwenye mikataba ?
 
Unataka kuniambia vyombo vya serikali, mahakama, bunge, na raisi hawatoi ushirikiano kwa wananchi kwenye mikataba ?
Wanatoa ushirikiano ila ukiongezeka zaidi ni jambo la muhimu. Sio wote wanaopata ushirikiano wa moja kwa moja kwa maana watanzania wote milioni zaidi ya 55 hawawezi kupata ushurikiano moja kwa moja kwa wakati mmoja. Na pia niseme serikali kupitia mahakama na serikali za mitaa waongeze kusaidia wananchi pale wanapohutaji msaada wao wa kisheria katika mambo yanayohitaji mikataba. Wapo watanzania wanauziana vitu kwa mikataba yao wenyewe ambayo haizingatii misingi ya kisheria katika mikataba.

Mwisho. Serikali kupitia mahakama na serikali za mitaa na vyombo vyovyote vyenye uwezo wa kusaidia wananchi katika kuandaa mikataba viwasaidie ili kuondoa migogoro na utapeli katika shughuli zao zitakazo husisha mikataba
 
Wananchi miilion 50 hawawezi kupata ushirikiano moja kwa moja kutoka kwa serikali kwani hakuna vitengo vya chini vya kiserikali kuanzia wajumbe wa mitaa mpaka wilaya na mikoa ?
 
Wananchi miilion 50 hawawezi kupata ushirikiano moja kwa moja kutoka kwa serikali kwani hakuna vitengo vya chini vya kiserikali kuanzia wajumbe wa mitaa mpaka wilaya na mikoa ?
Vipo ndio maana nimesema serikali za mtaa na mahakama zitoe ushirikiano wa moja kwa moja kwani zipo karibu na wananchi.
 
Wananchi miilion 50 hawawezi kupata ushirikiano moja kwa moja kutoka kwa serikali kwani hakuna vitengo kuanzia wajumbe wa mitaa mpaka wilaya na mikoa ?

Vipo ndio maana nimesema serikali za mtaa na mahakama zitoe ushirikiano wa moja kwa moja kwani zipo karibu na wananchi.
Kwahiyo umaanisha serikali za mitaa na mahakama hazitoi ushirikiano kwa raia ?
 
Kwahiyo umaanisha serikali za mitaa na mahakama hazitoi ushirikiano kwa raia ?
Mkuu nimesema ziongeze kutoa ushirikiano panapo hitakika kama ushurikiank uliopo hautoshi basi uongezwe ili mambo yaende kwa haraka na wepesi zaidi
 
Kwahiyo umaanisha serikali za mitaa na mahakama hazitoi ushirikiano kwa raia ?
Ushirikiano uunatolewa lakini yapo malalamiko kwa wananchi hudai kuwa muda mwingine hawapati ufafanuzi unaozingatia taratibu za kisheria kuhusiana na mikataba husika. Hivyo hapo panahitajika kuongezewa nguvu zaidi ili ushirikiano uwe mkubwa na waharaka zaidi
 
Back
Top Bottom