ili business plan iwe na mashiko inabidi itengenezwe na mjasiriamali mwenyewe na si mtu mwingine. mjasiriamali ambae kwa kiasi kikubwa ndiye mwenye idea ya biashara anatakiwa ajue namna gani ameplan kufanya biashara yake.
sasa kwa vile si kila mjasiriamali anaouwezo wa kudraft business plan...kazi ya mtaalamu inatakiwa kutoa tu mwongozo namna gani anaweza kumwezesha mjasiriamali akaandika plan ya biashara yake.
hoja yangu hapa ni kwamba mjasiriamali ndie anaejua namna anavotaka kuendesha biashara yake..ndie anaejua mazingira anayofanyia biashara yake..ndie anaejua changamoto katika eneo aliopo..ndie anaejua bei na gharama za uzalishaji..ndie anaejua potential market ya bidhaa yake.. sasa inapotokea mtaalamu anaetaka kumwandikia plan badala ya kutoa mwongozo namna mjasiriamali anavoweza kuendeshq biashara yake huwq nashindwa kuelewa