Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mwanamke mwenye kundi lolote la damu ambalo ni negative (A-, B-, AB- na O-) akipata ujauzito kutoka kwa mwanamme mwenye kundi la damu ambalo ni positive (A+, B+, AB+ au O+) mwili wake unaweza kutengeneza kinga mwili ambazo huwa ni hatari kwa ujauzito unaofuata.
Athari za kinga mwili hizi huanza kuonekana kwenye ujauzito wa pili na kuendelea ambapo humshambulia mtoto akiwa bado yupo tumboni na kumsababishia upungufu mkubwa wa damu, umanjano, kuharibika kwa ini pamoja na magonjwa ya moyo.
Mambo haya huwafanya watoto wafariki wakiwa tumboni au muda mchache baada ya kuzaliwa.
Ili kuondoa changamoto hizi, mwanamke mjamzito hupaswa kupata sindano yenye kinga (Anti D) kwenye wiki ya 28 ya ujauzito au ndani ya saa 72 baada ya kujifungua.
Ni muhimu kwa wachumba (wanandoa) kufahamu makundi yao ya damu kabla hawajaamua kupata ujauzito ili kujiandaa na changamoto za aina hii ambazo ni rahisi kuzikabili kabla hazijaleta madhara ya kudumu.
ACOG