Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 889
- 1,789
Kwanza nitoe pongezi kwa majeshi yote ya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na mipaka ya nchi yetu, Huu ni mtazamo wangu kwa jinsi ninavyotazamia haya masuala ya ulinzi na usalama.
Kuna jambo ambalo kama serikali inabidi ilizingatie kwa maslahi mapana ya taifa, Jambo hilo ni umakini na mabadiliko katika kutafuta na kufundisha askari wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama.
Hapa nitazungumzia mambo wawili, Jambo la kwanza ni uzalendo wa vijana wanaojiunga na Jeshi. Ifahamike kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaojitokeza kuomba nafasi pale zinapotangazwa katika majeshi ya ulinzi na usalama ikiwemo polisi, magereza, uhamiaji, zimamoto na JWTZ, Kwa haraka haraka jambo hili halitii wasiwasi wowote kwa taifa bali linatoa hamasa na Faraja kwa taifa, kuwa kuna vijana wanaotaka kulitumikia taifa.
Hoja yangu ipo kwenye Je ni kweli vijana hawa wanapenda kulitumikia taifa na Jeshi au wanakuja Kwakuwa hakuna option nyingine? Namaanisha ajira zimekuwa ngumu miaka hii.
Kwa experience niliyonayo na picha ya haraka niliyoipata nasema hivyo Kwakuwa nimewahi hudhururia interview za majeshi mbalimbali. Ukiwa unaongea na kubadilishana mawazo na co-interviewee utagundua kuwa wengi wanataka kujiunga na majeshi ya ulinzi na usalama for the reason of making life only and no other reason ijapokuwa kwenye interview wanasema sababu tofauti kama uzalendo na mapenzi kwa Jeshi.
Jambo hili la vijana kutaka kujiunga na majeshi kwa sababu za kimaisha si jambo la kupuza hata kidogo kwani wengi katika wasomi wa fani tofauti kwa ngazi za elimu tofauti kimbilio limekuwa ni Jeshi, Hii inamaanisha kuwa maafisa wengi wa Jeshi kwa siku za usoni watakuwa wameingia katika vyombo vya ulinzi na usalama, Maafisa hawa ndio tutao wategemea kulinda amani ya Tanzania lakini pia ndio tutawatumia katika masuala yato yanayohusu ulinzi na usalama kwa taifa hili.
Je kwa sababu hii hatuoni umuhimu wa kuwa na vijana wazalendo wa kweli kwa taifa?
Kama tutakuwa na askari wanaoingia kwa ajili ya pesa tutegemee rushwa, uvunjwaji wa haki za binadamu, uasi Pamoja na tamaa za madaraka kukithiri katika majeshi yetu. Hivyo, Kuepuka yote haya ni lazima tuwe na mipango ya uhakika katika kuandaa askari bora Zaidi na wenye weledi kwa Jeshi letu.
Jambo la pili linatokana na swali hili..Ikiwa askari wamejiunga na jeshi kwa sababu ambayo si uzalendo kwa nchi, Je kuna uwezekano wa kuwafanya kuwa wazalendo ?Hapa niseme kuwa ndio kuna uwezekano wa mtu kufundishwa uzalendo, Ndio maana nikasema kuna haja ya kubadilisha kidogo mitaala ya kijeshi mbali na mafunzo ili iweze kuwajengea uzalendo wa kweli askari wetu.
Uzalendo unafundishwa kwa njia mbalimbali, Lakini kwanza tujiulize kwanini vijana wanajiunga na majeshi yetu bila uzalendo? Kisha ndio tuainishe njia za kufundisha uzalendo. Sababu za askari wetu kutokuwa na uzalendo ni pamoja na kutokujua historia ya nchi yetu, Historia za wapigania uhuru Pamoja na umuhimu wa amani tuliyonayo. Ikiwa utakuwa kuwa na askari ambaye hajui historia ya nchi yake vipi ataweza kukipenda na kukilinda asichokijua?
Lakini pia askari wetu wanakosa uzalendo kwa sababu ya kutoelewa Jeshi ni nini hasa, kwanini wao ni askari, Kwanini serikali inagharamikia pesa nyingi ili wao wawe trained. Tukiweza kufundisha kwa usahihi mambo haya tutaweza kuwajenga askari wetu katika misingi bora na automatic hisia za uzalendo zitamea katika nyoyo zao.
Katika kuwajengea uzalendo askari wetu tunaweza pia kuunda mfumo wa kimazoezi ili kuwajengea spirit ya kizalendo, Kwamba katika arena za mazoezi kufungwe bendera za nchi pembeni ili askari anapokuwa anateseka kwa ajili ya mafunzo ajue yote hayo anayapitia kwa ajili ya kuitumikia Tanzania, kila siku askari akiwa anaona hilo basi spirit ya ujasiri na uzalendo itajijenga kwake.
Jambo hili lifanyike Pamoja na kuimba nyimbo za kizalendo kila siku asubuhi na jioni kabla ya mazoezi yote kwa Pamoja yatasaidia kujengea askari wetu uzalendo.
Mwisho niseme huu ni mtazamo wangu binafsi, kama unatoka ya kuongeza kuhusu njia za kuwajengea uzalendo askari na viongozi wetu unaweza ongezea.
Nawasilisha. Asanteni