Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Na wewe huwa unafanya hivyo?Acha kufundisha vijana uvivu, mwanaume wa kweli aoge baada ya siku 3 kwa wiki ×2.
Usisahau hapo kuna kujimwagia mashahawa wakati wa kufanya mambo fulani na yanavyotoa harufu kali, wanawake wana roho za kubeba.. sasa imagine mtu kaishi nayo wiki km sio mafua na kikohozi mfululizo ni nini?Na wewe huwa unafanya hivyo?
Sijawahi kuelewa kutia udhu ni kwa jinsi gani ni usafi na kujitakasa wakati mtu hatumii sabuni.my people,
Katika maisha ya kila siku, mwanaume mara nyingi hupimwa kwa nguvu, kazi, au uwezo wa kuwajibika. Lakini kuna kipimo kingine cha msingi ambacho mara nyingi hupuuzwa: usafi na kujipenda.
Hivi viwili si anasa wala mapambo ya juu juu, bali ni mizizi ya afya njema, heshima binafsi, na uhusiano mzuri na watu pamoja na Allah.
1. Usafi ni sehemu ya imani
Katika Uislamu, usafi si hiari, ni wajibu.
Mtume ﷺ amesema:
“Usafi ni nusu ya imani.” (Muslim)
Hii inamaanisha kuwa mwanaume anayejali usafi wa mwili, mavazi, mazingira, na moyo wake anajenga uhusiano bora na Allah na watu. Usafi huleta utulivu wa nafsi na heshima ya kijamii
2. Kujipenda ni kutambua thamani uliyopewa na Allah
Kujipenda hakumaanishi kiburi, bali ni kujithamini. Ni kukubali kwamba wewe ni kiumbe wa Allah mwenye thamani, unastahili afya, utunzaji, na maisha yenye ubora.
Mwanaume anayejipenda:
Hujali afya yake
Hujiheshimu
Huepuka tabia zinazomharibu
Hujijengea nidhamu ya maendeleo
Hili humfanya awe bora kwa familia yake, jamii, na dini yake.
3. Usafi huongeza kujiamini na mvuto wa kimaadili
Mwanaume msafi huingia mahali akiwa na utulivu wa ndani na nje. Harufu nzuri, mavazi safi, na mwonekano nadhifu ni lugha ya kimya inayosema:
“Najiheshimu, na ninawaheshimu wengine.” Hili huongeza kujiamini na kuimarisha mahusiano ya kijamii na kifamilia
4. Kujipenda humjenga mwanaume mwenye akili timamu
Mwanaume anayejipenda hujipa muda wa kupumzika, kujifunza, kufanya ibada, na kurekebisha makosa yake bila kujichukia. Hii humsaidia kuwa na utulivu wa kiakili, subira, na uwezo wa kukabiliana na changamoto bila kukata tamaa.
5. Usafi na kujipenda huimarisha ndoa na familia
Mwanaume msafi na anayejipenda humfurahisha mwenzi wake na huwapa watoto mfano bora wa kuigwa. Hujenga nyumba yenye amani, heshima, na mawasiliano mazuri
Hatua za vitendo kwa mwanaume
Oga mara kwa mara na tumia
manukato kwa kiasi
Va mavazi safi na nadhifu
Dumisha usafi wa kinywa, ndevu, na nywele
Jali afya ya mwili na akili
Jisemee maneno chanya na jithamini
Hitimisho:
Mwanaume msafi na anayejipenda ni kama bustani iliyotunzwa: huvutia, hutuliza, na huzaa matunda mema. Katika Uislamu na maisha kwa ujumla, kujitunza si udhaifu bali ni nguvu iliyovaa utulivu.
Ni hayo tu!
Yesu aliogea sabuniSijawahi kuelewa kutia udhu ni kwa jinsi gani ni usafi na kujitakasa wakati mtu hatumii sabuni.
Hivi MCHANGA/UDONGO unaweza ukauosha na Sabuni ?Sijawahi kuelewa kutia udhu ni kwa jinsi gani ni usafi na kujitakasa wakati mtu hatumii sabuni.
Anuke kama nguchiro Ili iweje sasa!Acha kufundisha vijana uvivu, mwanaume wa kweli aoge baada ya siku 3 kwa wiki ×2.
Watu wanajitutumua tu , ila hakuna mtu mwenye akili timamu asiye jua umuhimu wa usafi wa mwili, kinywa , mavazi na hata mazingira yanayomzunguka .Anuke kama nguchiro Ili iweje sasa!
Binadamu asipojiswafi, ni kiumbe anayezalisha harufu mbaya sana kuliko viumbe wengine wote wasiooga.
Eutugrul Bey katoa somo zuri sana kutukumbusha wajibu wetu, tumpigie makofi mengibtafadhali.
Waislamu tunatia udhu kwa sababu ni amri ya Allah, ni ibada, na ni njia ya kujitakasa kabla ya kusimama mbele Yake katika swala.Sijawahi kuelewa kutia udhu ni kwa jinsi gani ni usafi na kujitakasa wakati mtu hatumii sabuni.
Nimeipenda hiiAnuke kama nguchiro Ili iweje sasa!
Binadamu asipojiswafi, ni kiumbe anayezalisha harufu mbaya sana kuliko viumbe wengine wote wasiooga.
Eutugrul Bey katoa somo zuri sana kutukumbusha wajibu wetu, tumpigie makofi mengibtafadhali.
Tatizo la watu kama huyu ustadh na Waswahili wengine wanafikiri usafi muhimu ni kuoga na kujinyunyuzia marashi tuWatu wanajitutumua tu , ila hakuna mtu mwenye akili timamu asiye jua umuhimu wa usafi wa mwili, kinywa , mavazi na hata mazingira yanayomzunguka .
Wamatumbi wengi usafi na ustaharabu kwenye vyoo hasa vya umma , mfano vyoo vya standi , bar , maofisini na nk ni zero kabisa.
Unakuta mtu kafunga na tai au mdada mzuri ,na mrembo na ni mtu mzima lina pupu , halafu hali flash na maji linanyanyuka kama goigoi🚮🚮
Umeonja chimpumu wewe badili tabia.Anuke kama nguchiro Ili iweje sasa!
Binadamu asipojiswafi, ni kiumbe anayezalisha harufu mbaya sana kuliko viumbe wengine wote wasiooga.
Eutugrul Bey katoa somo zuri sana kutukumbusha wajibu wetu, tumpigie makofi mengibtafadhali.
Yeah! Bila shaka, ndivyo inavyotakiwa.Na wewe huwa unafanya hivyo?
Mkuu, mkuu, mkuu!Umeonja chimpumu wewe badili tabia.
Samahani ndugu sikujua kama hutumia maji ya uzima, samahani yangu ikutie moyo na kukuondolea kinyongo cha kukuhalibia siku.Mkuu, mkuu, mkuu!
Nimekuita mara tatu, temea chini kuashiria ulimi wako umeteleza na uniombe radhi ili nisijali.
Sinywagi hayo makitu mie, umeniunderate sana na kuniharibia siku!