Daniel Adam Kidingija
New Member
- Jan 20, 2015
- 2
- 1
Utangulizi
Huenda hulijui hili, kwa wewe ambae unalijua basi nakukumbusha. Sionekani ila nipo kila mahali ambapo binadamu huishi. Mataifa makubwa duniani na nchi nyingi zinazoendelea zinatambua umuhimu wa mimi kuwa timamu. Ila nasikitika kuona taifa lililo na watu zaidi ya millioni sitini (60), wakipuuzia umuhimu wa mimi kuwa timamu.
Nisikuchoshe, tambua na kumbuka mimi nsipokuwa sawa shughuli zako zitayumba, maendeleo hayatakuwepo, mahusiano yatavunjika, migogoro itakuwa mikubwa, na afya ya mwili itadolola. Mimi ni AKILI. Hitaji langu ni uwepo wa WATAALAMU WA AFYA YA AKILI ndani ya taifa hili.
Upo na maswali, nipo na majibu;
Mtaalamu wa afya ya akili ni nani?
Ni mtu aliebobea katika kuhakikisha watu wana itamamu wa akili. Hufanya hivyo kupitia njia za kisayansi ili kuboresha utimamu wa akili, kutambua na kutibu magojwa mbalimbali ya akili. Wengi hupenda kuwaita wanasaikolojia.
Uhalisia kuhusu wataalamu wa akili ndani ya nchi
Taifa linazalisha wataalamu wa akili kwa kiwango kidogo. Hii inatokana na sitofahamu juu ya umuhimu wa wataalamu hawa katika jamii.
Bahati mbaya hata hawa wanaozalishwa na baadhi ya vyuo hapa nchini wamejikuta katika wakati mgumu kwani thamani ya taaluma yao baado ni ndogo katika jamii ya inayowazunguka.
Viashilia vya umuhimu wa wataalamu wa afya ya akili katika jamii
1. Ongezeko la kesi za mauaji/watu kujiua.
Kutokuwa sawa kisaokolojia kutokana na changamoto za kimaisha kumefanya vijana wengi wakatishe uhai yao. Wengine huchukua maamuzi ya kuua kisha kujiua, hali hii inatokana na kukosa msaada wa kisaikolojia.
2. Unyanyaswaji wa kijinsia endelevu.
Ni watu wangapi wanapigwa, na kubakwa na wapenzi wao? Jibu ni wengi.
Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia huacha makovu sugu kwenye akili ya wahangwa wa matukio haya. Bila msaada wa kisaikolojia tabia na kufikili kwao huathilika. Pia wanaofanya matukio haya huhitaji msaada wa kisaokolojia ili kuacha matukio haya.
Ifahamike sio kila anaefanya unyanyasaji wa kijinsia anafahamu kuwa anafanya hivyo.
3. Ufahamu mdogo juu ya magonjwa ya akili ulikoambatana na imani potofu.
Daima imani ya mtu iheshimike, daima, imani potofu juu ya magonjwa ya akili ipigwe vita. Kumekuwa na unyanyapaa mkubwa kwa watu walio na magonjwa ya akili, wengine hufikia hatua ya kuwaita neno nsilopenda tamka (kumradhi)
Wapo ambao hutenga ndugu na jamaa zao pale wanapokuwa na tatizo la akili. Wapo wanaoamini magonjwa ya akili hayatibiki. Wapo wanaoamini matatizo ya akili huwapata baadhi ya watu tu. Pia, wapo wanaomini mtu akipatwa na ugonjwa wa akili basi kalogwa.
Imani kama hizi zinatokana na kukosa ufahamu wa kutosha juu ya magonjwa na matatizo ya akili.
Kasi ya ndoa nyingi kuvunjika kuwa kubwa.
4. Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na kukosa msaada sahihi
Wanasaikolojia hawashirikishwi kutatua changamoto na kusaidia imalisha mahusiano. Kwani tunasahau mahusiano ni saikolojia.
5. Unyanyaswaji wa watoto na malezi mabovu ambukizwi kizazi adi kizazi
Sote ni mashuhuda jinsi wimbi la watoto wa mitaani linavyokuwa kubwa. Watoto wengi hutelekezwa na wengine hukimbia majumbani kutokana na unyanyasaji. Bahati mbaya ni kwamba wengine hubeba yale malezi mabovu waliopitia adi kwenye familia zao ukubwani.
Baadhi ya changamoto katika kuhakikisha Watanzania wanautimamu wa akili ulio bora
1. Kuajili watu wasio na taaluma ya saikolojia kufanya kazi za wanasaikolojia. Mfano mzuri ni kutegemea mwalimu atoe msaada wa kisaikolojia vile inapaswa kwa mwanafunzi. Au mtu wa ustawi wa jamii na nesi atoe msaada wa kisaikolojia vile inapaswa.
2. Kutotambulika kwa shirika la wataalamu wa saikolojia nchini (TAPA – Tanzania Psychologists Association).
3. Vyuo vichache kutoa mafunzo juu ya afya ya akili. Vyuo kama Chuo Kikuu cha Iringa, St. George, UDOM, na Muhimbuli ndivyo vimekuwa vikizaliza wanasaikolojia kwa kiasi kidogo.
4. Wananchi kukosa ufahamu wa kutosha juu ya afya ya akili.
Wataalamu wa akili wanavyoweza changia maendeleo ya nchi
Wanasaikolojia watasaidia kuimalisha afya za watu, kwa kuwasaidia epuka na pambana zaidi ya changamoto zinazoweza athili maendeleo yao na taifa. Mfano, mfanyakazi atafanya kazi vizuri zaid akiwa hana msongo wa mawazo
Maeneo nyeti yanayohitaji wataalamu wa akili kwa wingi na haraka
Wanasaikolojia wanahitajika kila kona, kwa kuzingatia mambo kadha ni vyema tukuanza kukahikikisha wanapatikana kwanza maeneo kama vile
1. Shuleni na vyuoni.
Maeneo haya yanamuingiliano wa watu tofauti na mwingiliano wao mkubwa. Tazama, kesi za mimba mashuleni, watoto kulawitiwa mashuleni, wadogo zetu kunyanyaswa kingono, ufaulu mdogo, na matukio tofauti yanayosikitisha yanavyojitokeza mashuleni. Mambo haya yanaathili saikolojia ya wanafunzi wengi, je ni msaada gani wanapata?
Nsiwe mchoyo wa pongezi kwenda Chuo Kikuu cha Iringa kwa kumiliki kituo cha ushauri nasihi na msaada wa kisaikolojia.
2. Hospitalini.
Wataalamu wa akili afya ya akili ni wengi, na wote wanaumuhimu. Serikali ione umuhimu kuwa na wataalamu wa afya ya akili mahospitalini, kwani afya ni utimamu wa mwili na akili, na si utimamu wa mwili peke yake.
Ngazi ya ustawi wa jamii.
Wanasaikolojia waajiliwe katika ngazi ya ustawi wa kijamii kama wanasaikolojia na sio kama watu waliosomea maendeleo ya jamii. Kufanya hivi matatizo mengi ya kisaikolojia yatatatuliwa.
3. Vyombo vya dola na magerezani
“Ametoka jela jana, leo ameshapata kesi nyingine”. Baadhi ya maneno ambayo watu huweza sema juu wa ndugu na jamaa zao wakitoka jela.
Kuna umuhimu wakuwa na wanasaikolojia maeneo haya kwani watu huhitaji kuandaliwa kisaikolojia juu ya maisha baaada ya kutoka gerezani. Lakini pia, wengine hujikuta magerezani kutokana na changamoto za kisaikolojia walizonao.
Hitimisho
Hakuna binadamu ata moja anaestahili kusema yuko na afya njema wakati afya yake ya akili imedolola. Kama taifa ni wajibu wetu kuzilinda afya zetu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kesho.
Msaikolojia;
Daniel Adam Kidingija
+255758951751
rixdanix@gmail.com
Huenda hulijui hili, kwa wewe ambae unalijua basi nakukumbusha. Sionekani ila nipo kila mahali ambapo binadamu huishi. Mataifa makubwa duniani na nchi nyingi zinazoendelea zinatambua umuhimu wa mimi kuwa timamu. Ila nasikitika kuona taifa lililo na watu zaidi ya millioni sitini (60), wakipuuzia umuhimu wa mimi kuwa timamu.
Nisikuchoshe, tambua na kumbuka mimi nsipokuwa sawa shughuli zako zitayumba, maendeleo hayatakuwepo, mahusiano yatavunjika, migogoro itakuwa mikubwa, na afya ya mwili itadolola. Mimi ni AKILI. Hitaji langu ni uwepo wa WATAALAMU WA AFYA YA AKILI ndani ya taifa hili.
Upo na maswali, nipo na majibu;
Mtaalamu wa afya ya akili ni nani?
Ni mtu aliebobea katika kuhakikisha watu wana itamamu wa akili. Hufanya hivyo kupitia njia za kisayansi ili kuboresha utimamu wa akili, kutambua na kutibu magojwa mbalimbali ya akili. Wengi hupenda kuwaita wanasaikolojia.
Uhalisia kuhusu wataalamu wa akili ndani ya nchi
Taifa linazalisha wataalamu wa akili kwa kiwango kidogo. Hii inatokana na sitofahamu juu ya umuhimu wa wataalamu hawa katika jamii.
Bahati mbaya hata hawa wanaozalishwa na baadhi ya vyuo hapa nchini wamejikuta katika wakati mgumu kwani thamani ya taaluma yao baado ni ndogo katika jamii ya inayowazunguka.
Viashilia vya umuhimu wa wataalamu wa afya ya akili katika jamii
1. Ongezeko la kesi za mauaji/watu kujiua.
Kutokuwa sawa kisaokolojia kutokana na changamoto za kimaisha kumefanya vijana wengi wakatishe uhai yao. Wengine huchukua maamuzi ya kuua kisha kujiua, hali hii inatokana na kukosa msaada wa kisaikolojia.
2. Unyanyaswaji wa kijinsia endelevu.
Ni watu wangapi wanapigwa, na kubakwa na wapenzi wao? Jibu ni wengi.
Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia huacha makovu sugu kwenye akili ya wahangwa wa matukio haya. Bila msaada wa kisaikolojia tabia na kufikili kwao huathilika. Pia wanaofanya matukio haya huhitaji msaada wa kisaokolojia ili kuacha matukio haya.
Ifahamike sio kila anaefanya unyanyasaji wa kijinsia anafahamu kuwa anafanya hivyo.
3. Ufahamu mdogo juu ya magonjwa ya akili ulikoambatana na imani potofu.
Daima imani ya mtu iheshimike, daima, imani potofu juu ya magonjwa ya akili ipigwe vita. Kumekuwa na unyanyapaa mkubwa kwa watu walio na magonjwa ya akili, wengine hufikia hatua ya kuwaita neno nsilopenda tamka (kumradhi)
vichaa.Wapo ambao hutenga ndugu na jamaa zao pale wanapokuwa na tatizo la akili. Wapo wanaoamini magonjwa ya akili hayatibiki. Wapo wanaoamini matatizo ya akili huwapata baadhi ya watu tu. Pia, wapo wanaomini mtu akipatwa na ugonjwa wa akili basi kalogwa.

Upvote
1