Umuhimu wa wosia

Hapana ukiacha watu wafanye maamuzi ya namna hiyo ni hatari kweli....unaweza kushangaa nyumba ya familia inarithishwa kwa 'nyumba ndogo'........ndio maana nasema 'will inaweza kuwa contested'....hasa kama inahusu watu ambao kisheria sio warithi. Mind you hata ukiwa mzima kuna nyakati unaweza kuzuiwa kuuza mali zako mwenyewe kama inaonekana maamuzi hayo hayana sababu za msingi na yataathiri familia yako.
 
Bishanga nadhani sio suala la 'si mali yangu mwenyewe!'. Kuna hawa watoto uliowazaa hasa wakiwa chini ya 18 au 20, lazima wapate haki yao kwenye mali yako. Kama unaona choyo na hiyo mali kwa wanao usingewazaa :]]
 
ndo mana wengine huwa wanaamua kuuza mali zao wakiwa hai na fedha wanatafuna,kwisha biashara.
 
Reactions: SMU
ndo mana wengine huwa wanaamua kuuza mali zao wakiwa hai na fedha wanatafuna,kwisha biashara.
.....halafu inatokea 'wanajaaliwa' maisha marefu mpaka miaka 100 na mali kamaliza akiwa na 60!
 
Bishanga nadhani sio suala la 'si mali yangu mwenyewe!'. Kuna hawa watoto uliowazaa hasa wakiwa chini ya 18 au 20, lazima wapate haki yao kwenye mali yako. Kama unaona choyo na hiyo mali kwa wanao usingewazaa :]]

hapa nazungumzia mitoto karateee kutwa kucha iko vijiweni misokoto kwa kwenda mbele,shule hataki kufanya kazi hataki anasubiri dingi asatuke ili aunze nyumba,lol!
 
haya mambo ya mirathi bana,mi siyapendi kabisa hata kuyasikia! sasa huyo kijana wa 'nje', kwani babake alipokufa angekua kaacha kaptula tu na mashati ina maana maisha yake nayo yangekomea hapo? kwani mama yake anafanya nn? hii huwa inasababisha wanawake na sie kuwa na vitu vyetu tunaandika majina ya watoto na kuficha. yeye mama yake alipokua anakutana na mzee vichochoroni,alishindwa kumshawishi wafanye maendeleo? ilikua ni starehe tu na nyamachoma? (sorry im a bit harsh on this manake naamini mafanikio ya mwanamme yanaletwa na mkewe. kukimbizana kubana matumiz na kujenga sion mchezo bana! msione watu wamejirundikia mali..)
NB: ingekua mie mtoto wa nje ningekuwa kimya tu,sio kuingia na kugombea. ndo mambo yanayosababisha watu wanachukia watoto wa nje kwa kuwaona adui.
 

na wanaume kibao wanaozea segerea baada ya harakati za kuwafurahisha wake zao kubuma!
 
Hili la wosia lina ugumu lakini.....Nilishaandika ila kuna jamaa alinambia inaweza kuhamasisha kutatishaji safari yangu!! Kwamba my wife akishajua shea yake na akiweza kushawishi watoto wake wanaweza wakakuwahisha ili waanze kumiliki rasmi!!

Kwa vyovyote vile, huyo kijana ajitahidi kuwalamba viatu ndugu zake hao. Wakimwonea huruma watamsaidia. Kisheria yeye ni mtoto wa nje (wengine wanasema ametokana na starehe badala ya committed relationship) kwa hiyo hana chake pale!
 

Mkuu DC,observation yako nakubaliana nayo kabisa,kweli kabisa wapo kinamama ambao kwa kushirikiana na mitoto yao mikubwa wanammaliza mzee siku si zake.Tatizo wapo kinamama ambao kwao baba amzalishe,alee,asomeshe na watoto wakishaanza kujitegemea baba hana faida tena nyumbani,anakuwa mzigo kazi kusimangwa na wakati mwingine hata kupewa slow death (sumu ya taratibu).
 
Haifai hata kidogo kutegemea mali za urithi.
sasa si mpaka wazazi wakutoke ukiwa tayari kwenye umri wa kujitegemea,what if they die when a person is 14 or 15?
 
sasa si mpaka wazazi wakutoke ukiwa tayari kwenye umri wa kujitegemea,what if they die when a person is 14 or 15?

vipi kama mzazi hakuwa na mali hata kidogo? Unataka kusema wanaochwa bila mali hawakui?
 
vipi kama mzazi hakuwa na mali hata kidogo? Unataka kusema wanaochwa bila mali hawakui?

Husniyo temea mate chini,i happen to be one of those niliyepoteza mzazi aliyekuwa bread earner (my mom) wakati nikiwa mdogo,we acha tu,mengine siyo ya kusimulia.Yes nilikua,yes sikufa,lakini cha moto nilikiona!
 
Husniyo temea mate chini,i happen to be one of those niliyepoteza mzazi aliyekuwa bread earner (my mom) wakati nikiwa mdogo,we acha tu,mengine siyo ya kusimulia.Yes nilikua,yes sikufa,lakini cha moto nilikiona!

bishanga sio kwamba naongea hayajanikuta. Mi pia nilishampoteza mama. Najua maisha yanakuwa vipi b'aada ya kupoteza tunaowapenda na kuwategemea. Tukianza kuelezeana humu tutamwaga machozi. All those difficulties ndio zinatufanya tuwe better not bitter.
 

ukiona mkeo na watoto wanataka kukuwahisha basi hiyo familia haina upendo. na wewe na uhusiano wako na familia yako si mzuri.
 
Sipati picha mwanamke awe na watoto wa kike afu mume afe aandike urith kwa mtoto/watoto wake wa kiume wa nje. Kwa kweli ni dhambi kumnyanyapaa mtoto wa nje; lakini haya mambo ya mali ndiyo yanayofanya wamama wengi kuchukia watoto wa nje. Tuna family friend wetu ana mabinti tu; mumewe ana mtoto mmoja wa nje tena wa kiume; yule mama ni muongeaji huwa anamchana mume wake live kuwa asitegemee mwanae huyo wa nje ataambulia kitu kwani mali wanazisaka wote kwa hiyo jasho lake haliliwi na mtu. Good thing ni kuwa huyo mtoto yuko kwa mama yake. Kwa hiyo kama huyo mama yake ana akili amjengee maisha mwanae mapema ikiwezekana hata kwa kumbana huyo mwanaume.
 
Kuna kijana mmoja aliandikwa mrithi wa nyumba pale sinza, na baba yake alipofariki akaamua kumfukuza mama yake eti aende kijijini anataka nyumba yake auze, hamuwezi amini, mie pia naona watoto hata wakiandikishwa kitu wazazi waandike mpak a wote wafariki ndio warithi mali, sababu wengine huwa haziwatoshi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…