Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,158
Huyu bi dada aliolewa, mume wake akiwa safarini ilitokea baba mkwe amekuja na ujumbe wa kanisa mjini kwao. Yeye na mume wake wamejenga nje kidogo ya mji, hivyo Muda wa kumchukua mzee kumpeleka nyumbani haukuwepo.
Aliamua kwenda kwenye hoteli ya karibu na kanisa kula chakula na baba mkwe. Alifikiria kuendesha gari peke yake usiku baada ya chakula, aliamua kumkaribisha rafiki yake.
Watatu hawa walichukua meza wakaagiza chakula, vinywaji maongezi yalianza. Mzunguko wa hela maisha, siasa yakawa maongezi. Baba mkwe alimuuliza rafiki wa mkwewe unajishuhulisha na nini hapa mjini?
Mdada alitiririka kuwa ana saloon na pia anapika chakula na kuuza maofisini na kumalizia pia nina mabwana wenye pesa.
Baba na mkwewe hamu ya chakula ilifikia ukingoni.