John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Umoja wa Mataifa (UN) unakusudia kuchangisha dola bilioni moja (Sh triloni 2.3) kwa kufadhili misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Ukraine katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths anayeshughlikia misaada ya kibinadamu, ameeleza hayo alipozungumza na waandishi habari.
Umoja wa Mataifa pia umesema unatenga haraka msaada wa dola milioni 20 kwa ajili ya Ukraine, umeeleza kuwa hata kabla ya Ukraine kuvamiwa na Urusi watu wapatao milioni tatu wa nchi hiyo tayari walikuwa wanahitaji misaada baada ya miaka kadhaa ya mapigano kati ya serikali ya Ukraine na waasi wa majimbo yaliyojitenga mashariki mwa nchi hiyo wanaoungwa mkono na Urusi.
Hata hivyo, Griffiths amesema viwango vya misaada kwa ajili ya Ukraine sasa vimeongezeka.
Source: DW