Usifikiri kwamba Mimi sina akili kama ulivyo wewe.
UN wana Ofisi zao karibia kwenye Nchi zote kabisa zilizopo hapa duniani ikiwamo na Tz, isipokuwa kwenye nchi chache sana kama vile Korea ya Kaskazini ambako hawana Ofisi huko.
Aidha, Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) zipo pia katika Nchi zingine tofaufi na huko New York Marekani. Mathalani, Jijini Geneva nchini Uswizi pia zipo Ofisi Kuu za UN. Si hivyo tu, lakini pia UN wanazo Ofisi zao zingine za Makao Makuu ya Kikanda karibia kwenye Mabara yote kabisa yaliyopo hapa duniani, isipokuwa katika Bara la Antarctica.
Hivyo Basi, Hoja yako ya kwamba UN wamefulia haina mashiko hata kidogo.
Vile vile, siyo kweli kabisa kwamba Ofisi za UN zilizopo nchini Kenya hazina manufaa yoyote kwa Wananchi wa kawaida wa Kenya. Hii siyo kweli kabisa, Mimi binafsi ninayeandika comment hii hapa katika mtandao huu wa JF pia ni Shuhuda na mnufaika mmojawapo wa kuwepo kwa Ofisi hizo za UN hapo Nairobi nchini Kenya, japokuwa Mimi siyo raia wa Kenya, bali ni mTanzania. Aidha, pia nimewahi kuishi na raia wengi wa Kenya huko ughaibuni, kuwepo kwa Ofisi hizo za UN zimechangia kwa kiasi kikubwa kwa Kenya kuwa na DIASPORA wengi Sana waliosambaa katika nchi mbalimbali zilizopo hapa duniani, licha ya Ofisi hizo za UN kuongeza pato la ndani la Nchi hiyo ya Kenya kwa kukuza Uchumi wa Wananchi na Serikali kwa ujumla wake.