Umoja wa Mataifa (UN) kupitia ukurasa wake wa twitter wameutaja mtandao wa kijamii wa WhatsApp kama njia rahisi ya kusambaza taarifa zisizo sahihi.
Wameandika ujumbe kupitia WhatsApp huweza kuonekana kama umetoka kwa mtu wa karibu. Wamesema ni muhimu kuhakiki ujumbe kabla ya kuutuma kwa wengine.
Wataalamu wa Usalama wa mtandaoni wamekuwa wakishauri matumizi ya mitandao mingine kam telegram na signal kwa uthabiti wa ulinzi na usalama wake ukilinganisha na WhatsApp.