UN: Raia takriban 700 wameuawa Ukraine tangu Urusi avamie

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Umoja wa Mataifa umedai kuwa zaidi ya raia 700 wakiwemo watoto 52 wameuawa nchini Ukraine tangu Urusi ilipoivamia jirani yake wiki tatu zilizopita, lakini idadi hiyo huenda ikawa kubwa zaidi.

Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amelieleza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa "vifo vingi kati ya hivyo vimesababishwa na mabomu katika maeneo yenye watu wengi".

Ameongeza kuwa mamia ya makaazi ya watu yameharibiwa ikiwa ni pamoja na hospitali na shule. DiCarlo amesema kuwa "kiwango cha vifo vya raia na uharibifu wa miundombinu ya raia nchini Ukraine hakiwezi kupuuzwa na kwamba kunahitajika uchunguzi kamili na uwajibikaji".

Naye mkuu wa shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameshutumu athari za vita kwa watu wa Ukraine ambao wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma na matibabu

WHO imethibitisha mashambulizi 43 dhidi ya hospitali na vituo vya afya huku watu 12 wakiuwawa na 34 kujeruhiwa. Ghebreyesus amesema changamoto hiyo ya kukosa huduma na matibabu inatoa kitisho kwa watu walio na maradhi ya moyo, saratani, kisukari, VVU na kifua kikuu miongoni mwa magonjwa yanayo sababisha vifo vingi Ukraine.Urusi yazidisha mashambulizi Kiev

Hayo yakijiri, Urusi imeahirisha kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu azimio la "hali ya kibinadamu" nchini Ukraine, iliyokuwa ipigwe leo Ijumaa kutokana na kukosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa washirika wake wa karibu. kusisitiza kuwa kinachohitajika ni amani.
 
Mbona wachache Sana hao hata 1laki hawajafika Hadi Sasa!!! Basi wanapigana kistaarabu Sana !!

vita na iendelee ,adabu ipatkane.
 
UN ni Organisation ya ajabu sana hivi kweli wanashindwa kuchukua hatua week 3 zote hizo?

angekuwa USA ndio anapigana ndani ya muda mfupi sana wangeshatoa matamko

ila kwakuwa anapigana ukraine hata hawana habar

na ndio maana watu wanasemaga UN ni jeshi la USA tu na wala sio mataifa mengine
 
Back
Top Bottom