#COVID19 UN yaipa Tanzania takribani Dola 900,000 kusaidia wahanga wa UVIKO-19

#COVID19 UN yaipa Tanzania takribani Dola 900,000 kusaidia wahanga wa UVIKO-19

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
UN yaipa Tanzania karibu dola laki tisa kusaidia wahanga wa UVIKO-19.

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD umeipa Tanzania karibu dola laki 8 na 83 elfu kwa ajili ya kusaidia wakulima wadogo zaidi ya elfu 6 nchini Tanzania ambao wameathiriwa na janga la ugonjwa wa korona au UVIKO-19 pamoja na nzige vamizi. Wakulima hao ni kutoka mikoa ya Dodoma, Njombe, Singida, Simiyu na mikoa ya kisiwani Unguja.

Mashirika mbalimbali ya habari kama vile Devdiscourse na AllAfrica yameripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, ukuaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania ulikadiriwa kupungua kutoka asilimia 5 mwaka 2019 hadi asilimia 2 mwaka huu kutokana na janga la korona au UVIKO-19 (COVID-19) pamoja na nzige vamizi walioingia nchini humo na kuharibu mazao ya wakulima.

Kupungua huko kumeleta madhara mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei ya pembejeo za kilimo pamoja na wakulima wadogo kutofikiwa na masoko.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaendelea kusema kuwa: Athari hizo zinatishia kuwatumbukiza kwenye lindi la umaskini zaidi ya wakulima wadogo laki 5. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kupitia mfuko wake wa ruzuku ya kusaidia kupunguza umasikini umetoa takriban dola laki 8 na 83 elfu kusaidia Tanzania kuhimili madhara ya UVIKO-19 kwa wakulima.

Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti kuhusu hali ya UVIKO-19 (COVID-19) nchini humo.

Walengwa wa msaada huo ni wakulima wadogo wadogo katika mikoa ya Dodoma, Njombe, Simiyu, Singida na mikoa mitatu ya kisiwani Unguja.

Makundi yatakayonufaika nusu ni wanawake, asilimia 30 ni vijana na wengine ni wafanyabiashara wa mazao ya kilimo, wanunuzi, na maafisa kilimo.

Licha ya changamoto nyingi wanazokutana nazo wakulima, sekta hiyo itaendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania na shughuli kuu ya kujitafutia riziki kwa wakulima wengi wadogo wadogo nchini humo.

Tangu mwaka 1978 IFAD imesaidia programu 16 nchini Tanzania zenye thamani ya dola za kimarekani Milioni 917.
 
Mbona hela ndogo sana....
kweli beberu limechukia
Hapana, wameanza na hiyo kidogo waone kama itafikia wananchi masikini waliolengwa, au zitafadhili mizunguko na misururu ya magari kwa Rais na wapambe wake nchi nzima ,huku akigawa maburungutu mabarabarani na kusema serikali yangu inapesa sana.

tuliona kwa Mwendawazimu akiwa hana pesa anatulia, akipata tu mkopo , kiguu na njia na matusi juu.
 
Back
Top Bottom