Una hali ngumu, halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela

Una hali ngumu, halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela

Ivi umewahi kukutokea?? Una hali ngumu mno...... afu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela!?!.
Na wanakuchukia sababu wanaamini unawanyima au unawafanyia midhaha. Wakati ukweli n kwamba unapumulia oxygen.
Ndugu hiyo ni Mimi kabisa na huwezi amini hata mke Wangu anaamini Nina hela wakati anajua hata Kazi sina.
 
Ndo vizuri kukuwazia Mema? unalia nini sasa!! wanune wapasuke wewe viwanja hamishiakwingine wakuone kwa nadra!!
mbunye unapata bure!! mpaka na wake zao hao!!!

kwanza wachawi watakuogopa kuwa hurogeki wanajua una hela nyingi , km wakiroga utautafuta uchawi popote!! sababu una hela wewe hapo ongeza sarakasi usijikunje kimaskini. utashangaa inakuwa kweli, watu wengine wamesha kuona rohoni!!!

Piga kamba umenunua Meli!!! jisemee mazuri tuuu!! kama wanavo kuwazia siku moja ina kuwa kweli!! walio nuna wakutafute vizuri!!
 
Ndio maisha sometimes inatokea. Kuna watu ukiwa na shida huwezi kuwaambia maana hawatoamin kutokana na wasiyoyajua kuhusu wewe
 
Mie juzi tu kuna mtu nilikwazana naye kisa hivyo yaani ye hataki kabisa kuamini kwamba sina.

Nilibakia kumshangaa tu na kuwaza inamana mtu akiwa hana kitu mpaka afanyeje ndo mtu ajue huna, mana aliishia kulaumu as if ninacho nimemnyima kumbe hali yangu naijua mwenyewe.
 
ukijiona unaonekana una hela wakati huna kitu choka mbaya basi ujue kuwa kwenye maisha yako utakufa MASIKINI
 
Hivi imewahi kukutokea? Una hali ngumu mno...... halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela!?!.

Na wanakuchukia sababu wanaamini unawanyima au unawafanyia midhaha. Wakati ukweli ni kwamba unapumulia oxygen.
Hiyo ni dalili nzuri kuwa watu waliokuzunguka wanakutazama kama kiongozi, msaada, tumaini lao, mkombozi.

Sasa jitahidi ufanye jitihada ili mambo yakae sawa uweze kuwapa mkono wa huruma japo hata buku buku, MUNGU atakuongezea na atakuzidishia.
 
inatokeaga mtu Ni rafiki yako kabisaa lakini anakukopa 1000 wakati wewe ata Mia huna. Unachezea 50 kushuka chini. Jibu huwa nawajibu kuna kaniazima week iliyopita.
 
Back
Top Bottom