Una hali ngumu, halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela

Una hali ngumu, halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela

Hivi imewahi kukutokea? Una hali ngumu mno...... halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela!?!.

Na wanakuchukia sababu wanaamini unawanyima au unawafanyia midhaha. Wakati ukweli ni kwamba unapumulia oxygen.
Yaani ishanitokea... mpaka mmojawapo siku moja akaniambia.. SIKUJUA KAMA HUWA UNAKOPA HELA
 
Shida inakuja pale unapotakiwa kusolve tatizo dogo tu,Kuna msala nilipataga kipindj fulani nikawekwa ndani lockup,Cha kushangaza

Mshua akawa anahangaika,naona masaa yanaenda dhamana haniwekei,nikawaza mbali Sana haiwezekani kiasi Kama kile mzee ashindwe

Lakini baada ya kutoka nilimwelewa Sana,kulingana na anavyoaminika na majirani,hatari sana
 
Umenigusa mtoa mada.

Ndicho kipindi nnachokipitia Mimi kuanzia Machi mwaka huu mpk sasa
 
Maisha ni vita ya mtu mmoja mmoja wengine huwa wanakuwa watazamaji ili kushuhudia ushindi au kuanguka kwako.
 
Mie juzi tu kuna mtu nilikwazana naye kisa hivyo yaani ye hataki kabisa kuamini kwamba sina.

Nilibakia kumshangaa tu na kuwaza inamana mtu akiwa hana kitu mpaka afanyeje ndo mtu ajue huna, mana aliishia kulaumu as if ninacho nimemnyima kumbe hali yangu naijua mwenyewe.
Na hii hua inatokea sn kwa watu ambao hawapendi kuweka wazi matatizo yao au kayaanika matatizo yao. Basi mtu anaona unazoo kumbe we mwenyewe unaugulia tu moyoni
 
Ni kawaida hiyo hasa kutokana na umaridadi wako unavojiweka

Waswahili walisema umaridadi huficha umaskini
Mtu akikuona unang'aa ukakosa hata buku ya kumpa inakua ngumu kuamini kua huna
 
Hivi imewahi kukutokea? Una hali ngumu mno...... halafu watu wote waliokuzunguka wanakuona una hela!?!.

Na wanakuchukia sababu wanaamini unawanyima au unawafanyia midhaha. Wakati ukweli ni kwamba unapumulia oxygen.
Ndio
 
Ni kawaida hiyo hasa kutokana na umaridadi wako unavojiweka

Waswahili walisema umaridadi huficha umaskini
Mtu akikuona unang'aa ukakosa hata buku ya kumpa inakua ngumu kuamini kua huna
Naomba buku tano Vale[emoji23]
 
Mara nyingi sana

Ni mwezi mmoja tu umepita kuna sister mmoja aliniomba nimkopeshe mimi mwenyewe hata nusu ya aliyoomba sikuwa nayo kabisa cha kushangaza mdada wa watu hakuamini majibu kutoka kwangu

Nilimwambia sina yaani aliona nimemnyima kabisa

Na kweli sina ni vile tu sipendi kuweka shida zangu nje
 
Back
Top Bottom