Una jambo lolote uliwahi kudanganywa na Mwalimu wako?

Una jambo lolote uliwahi kudanganywa na Mwalimu wako?

Waliniambia kuwa binadamu walianza sokwe kisha akabadirika na kuwa mwanadamu. Nawasubiri awa sokwe wa uku porini hakuna ata anayeelekea kwenye ubinadamu wanazeeka tu
Hawakukuambia binadamu alianza kuwa sokwe bali walikufundisha nadharia (theories) mbili juu ya asili ya binadamu, ya kwanza ikiwa ni creation theory (nadharia ya uumbaji) ambayo huungwa mkono na dini. Na pili ni theory of evolution inayoungwa mkono na wanasayansi.

Nadharia (theories) ni mawazo na hoja tu ambazo pia zaweza kosolewa kwa udhaifu wake. So teacher hakukosea kitu, bali alikufundisha mawazo kinzani juu ya wapo binadamu katokea. Yafuatayo ni utashi wako sasa kwan waweza kuwa na nadharia yako binafsi
 
Kitu nilichoongopewa shuleni ni kwamba nikifaulu basi ntakuwa na maisha mazuri. Na wanaofeli basi washaharibikiwa kimaisha.

Ni UONGO mkubwa huu.
 
Mwalimu wangu wa sayansi "dalili za ualbino ni kupepesa macho" kwahiyo ukiona mtu anapepesa sana macho ujue anaanza kuwa albino daah MUNGU ANAMUONA POPOTE ALIPO
 
Back
Top Bottom