Una majibu ya kukera sana we baba kama sura yako

Una majibu ya kukera sana we baba kama sura yako

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Wakuu,

Kwanza nilishtuka, na kisha nikajitafakari kidogo then nikaona nikinyamaza itakuwa njema. Nimuite dada, mama, binti ambae ni mwenyeji wa kitambo mbali hapa kwetu.

Ghafla bila hiyana akanambia nimekuwa na majibu (comments) ya/za kukera, lugha mbaya zenye kukwaza. Nimekuwa mzee mkorofi mwenye majibu ya ghafla ndio maana nina sura mbaya hata sivutii na kadhalika.😜

Basi mwenyewe nikatabasamu na nikacheka tena.😂😂 Mwisho nikamuomba radhi kwa kumkera pasipo kumtia neno, nikasema nitaichana bahasha kisha nije niwasomee barua ya siri kwenu hapa ndani.

Na kama kweli nimekuwa kikwazo kwa yeyote, ikikupendeza niandikie ama nitumie barua.
 
Wakuu.....
Kwanza nilishtuka, na kisha nikajitafakari kidogo then nikaona nikinyamaza itakua njema.
Nimuite mdada, mama, binti ambae ni mwenyeji wa kitambo mbali hapa kwetu.
Ghafla bila hiyana akanambia nimekua na majibu "comments" ya/za kukera, lugha mbaya zenye kukwaza. Nimekua mzee mkorofi mwenye majibu ya ghafla ndiomaana nina sura mbaya hata sivutii na kadhalika...😜
Basi mwenyewe nikatabasamu na nikacheka tena..😂😂
Mwisho nikamuomba radhi kwa kumkera pasipo kumtia neno, nikasema nitaichana bahasha kisha nije niwasomee barua ya siri kwenu hapa ndani.
Na kama kweli nimekua kikwazo kwa yeyote, ikikupendeza niandikie ama nitumie barua.
Hii thread yenyewe tayari imeshakera... Ina sura mbaya kama avatar yako
 
Hii thread yenyewe tayari imeshakera... Ina sura mbaya kama avatar yako
Lakini nashukuru mlimpokea shangazi yenu vizuri ambae ni mke wangu. Pamoja na kukukera siku wekundu walipo lisakata ila bado najua udugu wetu bado utadumu...🤣
 
Lakini nashukuru mlimpokea shangazi yenu vizuri ambae ni mke wangu. Pamoja na kukukera siku wekundu walipo lisakata ila bado najua udugu wetu bado utadumu...🤣
Sina ubaya wowote na shangazi yangu. Namkubali kama navyolikubali shuti la KIBU DENIS. Lile kombora lilinisaidia kupata mkopo usio na riba pale STANBIC BANK
 
Kwa wasiopenda kuumiza kichwa, hii ni Summary..

Mkuu Ushimen alimuendea mrembo mmoja anayaonekana amekula chumvi nyingi PM.

Huyo mrembo akamjibu ana majibu mabovu kama sura yake mbaya kama inavyoonekana kwenye Avatar.

Mzee akaona aimwage humu.

Na huu ndiyo ndiyo Muhtasari wa Uzi kutoka hapa JF FM, Mikocheni Dar es Salaam.
 
Sina ubaya wowote na shangazi yangu. Namkubali kama navyolikubali shuti la KIBU DENIS. Lile kombora lilinisaidia kupata mkopo usio na riba pale STANBIC BANK
Yessuuu....🙆‍♂️
Mpwa, tabia zako za mambo mbalimbali umehamishia hadi Benki...🤔, basi hiyo dawa itunze kwa bidii...🤣
 
Kwa wasiopenda kuumiza kichwa, hii ni Summary..

Mkuu Ushimen alimuendea mrembo mmoja anayaonekana amekula chumvi nyingi PM.

Huyo mrembo akamjibu ana majibu mabovu kama sura yake mbaya kama inavyoonekana kwenye Avatar.

Mzee akaona aimwage humu.

Na huu ndiyo ndiyo Muhtasari wa Uzi kutoka hapa JF FM, Mikocheni Dar es Salaam.
Subhanallah....🙊
 
Yessuuu....🙆‍♂️
Mpwa, tabia zako za mambo mbalimbali umehamishia hadi Benki...🤔, basi hiyo dawa itunze kwa bidii...🤣
Namsubiria mjomba kwenye fainali ya shirikisho... JENERALI PHIRI na BALEKE wameniahidi watanipa udhamini wa mkopo pale CRDB...
 
Huyo ndio wewe halisi na hauna haja ya kufake
 
Kwa wasiopenda kuumiza kichwa, hii ni Summary..

Mkuu Ushimen alimuendea mrembo mmoja anayaonekana amekula chumvi nyingi PM.

Huyo mrembo akamjibu ana majibu mabovu kama sura yake mbaya kama inavyoonekana kwenye Avatar.

Mzee akaona aimwage humu.

Na huu ndiyo ndiyo Muhtasari wa Uzi kutoka hapa JF FM, Mikocheni Dar es Salaam.
Lakini mkuu.....
Mimi sihawahi kujibia MP hata nilipo jaribu kwa yule ajuza foksi alinikaushia mbona..🤓
 
Back
Top Bottom