Kuna kisa sijui kama ni cha kweli au la
Ilikuwa hivi mama alimnunulia mtoto wake mkubwa mdoli tuseme ana miaka 10, kisha akawa anamuachia huyo mtoto amuone mdogowake wa mwaka mmoja, anapotoka kwenda dukani sokoni au sehemu ya karibu.
Tatizo ikawa kila mama akiondoka yule mtoto anakuwa bize na mdoli wake mpaka anasahau kuangalia mdogo wake, mtoto anajinyea, analia, anakula uchafu mama akirudi anamgombeza sana, siku moja akarudi...
Akakuta mtoto kalia sana yule mkubwa wake yuko bize anauremba mdoli, alimpiga sana akamchapa sana, kesho yake akamuachia mtoto amuangalie,
Yule mtoto mpenda mdoli alichukia sana akamchukua mdogo wake akamtupa shimo la choo (vile vyoo vya zamani latrine), mama aliporudi anauliza mdogo wako yuko wapi mtoto kimya...tafuta sana ndio kupiga kilio majirani wakaja wakatafuta akakutwa chooni hali mahututi hakufanikiwa kupona alifariki, chanzo ni mdoli...