Una mawe kwenye figo? Soma hapa

Una mawe kwenye figo? Soma hapa

MziziMkavu , last 4 years baba yangu mzazi alishawahi kuupata huu ugonjwa,bahati nzuri alipona,kwa kufanyiwa operation ya mionzi.two years later mdogo wake akaumwa ugonjwa huu huu,too bad he never survived,,,je unadhani ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa kurithi?..........kama ushaonaga ile operation ya mionzi inavyofanywa....ni kwanini zile stones zikipasuka,unazisikia zikilia ndani ya mashine na sio kwenye mwili wa huyo mgonjwa?
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky iko shida sana na hii miili yetu............

Mkuu Rutashubanyuma kwa sasa sijui ulime mchicha wako na mboga zako na matunda yako mwenyewe ndo uyatumie kwa chakula chako
Maana kila uchao unasikia hiki kina madhara haya na haya
mbona babu zetu walitumia sana hivi vyakula tunavyokula na hatukuona mabadiliko au hatukuyaona madhara tunayoambiwa kwa sasa
Ni balaa mkuu ni kujitahidi tuu kula kwa kujipangilia maana hata hao wauzaji na wakulima hawaaminiki tena
Mboga za majani wanatumia chemical za hatari, maziwa wanawapa ng'ombe madawa ili watoe maziwa mengi, mafuta tunayotumia kupikia nayo ni hatari nyingine yanachakachuliwa mpaka mwisho sijui tuende wapi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.@Rutashubanyuma hebu angalia hapa Olive Oil: can it treat gallstones? Ona majibu yake yako mangapi?
About 4,200,000 results (0.41 seconds) Utagunduwa kuwa Mafuta ya Zaituni yaani Olive Oil yan faida kubwakutibu Mawe kwenye Figo.Mkuu
Rutashubanyuma ukubali au ukatae lakini hilo ndilo jibu langu chanzo bonyeza hapa https://www.google.com/search?q=Oliv...hrome&ie=UTF-8

MziziMkavu nafikiri sikueleweka..sipingi na nimesoma nimeona uwezekano ila inabidi mgonjwa apimwe na kuona ukubwa wa tatizo lake na aina ya mawe aliyonayo kama ni makubwa zaidi ya 15mm inawezekana yasimsaidie.

Pili nilipenda majibu ya Olive Oil na juisi ya apple inafanyaje kazi yake...............huyayeyusha au huyasukuma nje.................yaelekea ni kuyalainisha ili yatoke...........kwa namna gani hapo ninahitaji darasa lakini yawezekna kutibu matatizo yanayoanza.......
 
Mkuu Rutashubanyuma kwa sasa sijui ulime mchicha wako na mboga zako na matunda yako mwenyewe ndo uyatumie kwa chakula chako
Maana kila uchao unasikia hiki kina madhara haya na haya
mbona babu zetu walitumia sana hivi vyakula tunavyokula na hatukuona mabadiliko au hatukuyaona madhara tunayoambiwa kwa sasa
Ni balaa mkuu ni kujitahidi tuu kula kwa kujipangilia maana hata hao wauzaji na wakulima hawaaminiki tena
Mboga za majani wanatumia chemical za hatari, maziwa wanawapa ng'ombe madawa ili watoe maziwa mengi, mafuta tunayotumia kupikia nayo ni hatari nyingine yanachakachuliwa mpaka mwisho sijui tuende wapi

Mr Rocky umesema kweli uchafuzi wa mazingira na hasa hawa wawekezaji bomu ambao kila kukicha tunaagizwa tuwapishe ndiyo kiama chetu tutakuwa wagonjwa mno na tunachoumwa hakina tiba labda huku kwenye matibabu mbadala kwa maana ya usafishwaji wa uchafu ndani ya mwili..........
 
Mkuu Rutashubanyuma hatari iliyopo mbele yetu ni kuwa hata pale unapoambiwa kula matunda kwa wingi au vyakula vya kijani kwa wingi navyo vyakula vyenyewe haviaminiki mkuu
Vinalimwa kwa madawa na vinakuzwa kwa madawa na vinahifadhiwa na madawa mpaka kikufikie wewe mlaji ushachanganyiwa chemicals kibao
Mbegu nazo siku hizi ni hizo za genetic ambazo nazo ni madhara mengine mbegu zile za asili zishapotezwa na hawa wawekezaji na tumekaa tunashangilia mkuu ni hatari kubwa sana
 
Mr Rocky na hii balaa ya genetic na kushindana na Mwenyezi Mungu ni balaa kushinda hata vvu itakapoanza kulipua magonjwa sugu yasiyosikia dawa tutajuta kwanini hata tulizaliwa..........................tutalaani kile kitanda ambacho mama zetu walidungwa mimba na baba zetu.............iko shida kubwa sana mbeleni huko We need God's guidance on this..............
 
safi sana mzizi mkavu kwa matibabu we ni mkali zaid yao ndo maana avatar yako imekua ni topic kwao:typing:
 
Wana Jf njia nyingine rahisi ya kuondoa mawe na kuzuia mawe kwenye figo ni kujijengea tabia ya kula matikiti maji kila wakati. Tikiti maji ni kiboko ya njia.:laser:
 
Ahsante mzizi......naomba kujua dalili za haya mawe...na vipimo husika......yaani ntajuaje kama nina mimawe

Dalili za vijiwe katika figo ni zipi?

Dalili ni pamoja na

  • Kuhisi maumivu makali ya tumbo hasa sehemu za mbavu (colicky loin pain). Maumivu haya huwa na tabia ya kuja kwa ghafla, kudumu kwa sekunde kadhaa kisha kuachia. Maumivu huweza kushuka kuelekea kwenye ncha ya uume (tip of penis) kwa wanaume na kwa wanawake huelekea kwenye kinena.
  • Kujihisi kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kukojoa mkojo uliochanganyika na damu (hematuria)
  • Wakati mwingine uwepo wa usaha katika mkojo (Pyuria) hasa iwapo kuna maambukizi ya bakteria
  • Maumivu wakati wa kukojoa (dysuria)
  • Mkojo kutoka kwa kiwango kidogo sana (oliguria)
  • Mkojo hushindwa kupita katika mirija ya ureter na kusababisha figo kushindwa kutoa uchafu mwilini na kusababisha mlundikano wa uchafu kwenye damu hali inayojulikana kama postrenal azotemia
  • Kushindwa kupita kwa mkojo husababisha pia kutanuka kwa sehemu tofauti za figo (renal pelvisna calyces) hali inayojulikana kama hydronephrosis
  • Iwapo kutakuwa na maambukizi katika mkojo, mgonjwa anaweza kuwa na homa.@Smarty
 
Mkuu tiba ya mawe nafkiri itategemea na namna jiwe lilivyokuwa formed nikimaanisha component ya jiwe lenyewe. Mfano; chanzo cha jiwe inaweza kuwa excess calcium, oxalate au uric acid. Hii tiba yako haijaeleza ni aina gani ya stone inatibu.

Hebu soma hapa.

Types of kidney stones include:

Calcium stones.
Most kidney stones are calcium stones, usually in the form of calcium oxalate. Oxalate is a naturally occurring substance found in food. Some fruits and vegetables, as well as nuts and chocolate, have high oxalate levels. Your liver also produces oxalate. Dietary factors, high doses of vitamin D, intestinal bypass surgery and several metabolic disorders can increase the concentration of calcium or oxalate in urine.
Calcium stones may also occur in the form of calcium phosphate.Struvite stones. Struvite stones form in response to an infection, such as a urinary tract infection. These stones can grow quickly and become quite large, sometimes with few symptoms or little warning.

Uric acid stones.
Uric acid stones can form in people who don't drink enough fluids or who lose too much fluid, those who eat a high-protein diet, and those who have gout. Certain genetic factors also may increase your risk of uric acid stones.

Cystine stones.
These stones form in people with a hereditary disorder that causes the kidneys to excrete too much of certain amino acids (cystinuria).

Other stones.
Other, rarer types of kidney stones can occur.
 
dalili za vijiwe katika figo ni zipi?

dalili ni pamoja na

  • kuhisi maumivu makali ya tumbo hasa sehemu za mbavu (colicky loin pain). Maumivu haya huwa na tabia ya kuja kwa ghafla, kudumu kwa sekunde kadhaa kisha kuachia. Maumivu huweza kushuka kuelekea kwenye ncha ya uume (tip of penis) kwa wanaume na kwa wanawake huelekea kwenye kinena.
  • kujihisi kichefuchefu
  • kutapika
  • kukojoa mkojo uliochanganyika na damu (hematuria)
  • wakati mwingine uwepo wa usaha katika mkojo (pyuria) hasa iwapo kuna maambukizi ya bakteria
  • maumivu wakati wa kukojoa (dysuria)
  • mkojo kutoka kwa kiwango kidogo sana (oliguria)
  • mkojo hushindwa kupita katika mirija ya ureter na kusababisha figo kushindwa kutoa uchafu mwilini na kusababisha mlundikano wa uchafu kwenye damu hali inayojulikana kama postrenal azotemia
  • kushindwa kupita kwa mkojo husababisha pia kutanuka kwa sehemu tofauti za figo (renal pelvisna calyces) hali inayojulikana kama hydronephrosis
  • iwapo kutakuwa na maambukizi katika mkojo, mgonjwa anaweza kuwa na homa.@smarty
asante sana kwa elimu
 
JIKINGE NA UGONJWA HATARI WA MAWE KWENYE FIGO KWA CHAKULA

UGONJWA wa mawe kwenye figo ni miongoni mwa magonjwa yanayowapata na kuwasumbua watu wengi hivi sasa. Hata hivyo, kudhani kwamba wewe huwezi kupatwa na ugonjwa huo bila kuchukua tahadhari mapema ni sawa na dereva kudhani gari lake haliwezi kuishiwa mafuta wakati hajaenda kwenye kituo cha mafuta kuweka.

Kama kweli unahitaji kujiepusha na ugonjwa huu ambao tiba yake mara nyingi huwa ni operesheni, ni vizuri ukaanza kuchukua tahadhari mapema ya kujikinga kwa kula vyakula ambavyo vitakusaidia kuzidumisha na kuziweka figo zako katika hali ya usalama na usafi daima. Zifuatazo ni dondoo muhimu za vitu vya kula ambavyo hutoa kinga hiyo:

JUISI HALISI NA MATUNDA

Figo husaidiana na kibofu katika usagaji wa chakula na uondoaji wa sumu mwilini. Lakini kiungo kimoja kati ya hivi viwili kikijaa uchafu kwa sababu ya lishe duni au kula vyakula vyenye sumu, vitu mfano wa vimawe vidogo hujitengeneza kwenye figo, na vikifikia hatua hii, huwa vigumu kuyeyuka na huwa ndiyo mwanzo wa matatizo ya kiafya.

Hata hivyo, tatizo hili linaweza lisikupate ukiwa na tabia ya kunywa juisi halisi za matunda (ya kutengeneza nyumbani, siyo viwandani) pamoja na mboga za majani kila siku, kwani juisi na mboga za majani huondoa mrundikano wa uchafu na sumu katika kibofu na figo hivyo kuuacha mwili wako salama.

Miongoni mwa matunda yenye uwezo mkubwa wa kutoa kinga na hata nafuu kwa mgonjwa wa mawe kwenye figo ni pamoja na ‘epo’ (apple), ambalo lina kirutubisho aina ya ‘pectin’ ambacho kina uwezo wa kulainisha na kuyeyusha mawe na kuzuia mengine kujitengeneza kwenye figo. Pia juisi za limau, machungwa (jamii zote), nyanya pamoja na ‘beet root’ hutoa kinga imara dhidi ya ugonjwa huu hatari.

MAFUTA MAZURI

Ingawa wataalamu wengine huwashauri wagonjwa wa mawe kwenye figo kujiepusha na ulaji wa mafuta kabisa, hasa wale waliofanyiwa operesheni ya kuondolewa mawe, lakini kuna baadhi ya mafuta ni muhimu katika kuondoa mawe yaliyopo na kuzuia kutokea kwa mengine kwenye figo.

Kwa mafano, mafuta ya mzeituni (Olive Oil) hutumika mara nyingi katika tiba mbadala ya kusaidia usafishaji na uondoaji wa mawe kwenye figo. Vilevile mafuta ya nazi na hata mafuta ya wanyama wanaofugwa katika mazingira asilia ya kula majani porini, yanahusika katika afya ya kibofu na figo kwa kuziepusha sehemu hizo kupatwa na mawe.

Epuka kutumia mafuta yatokanayo na Soya ambayo yanaelezwa ni miongoni mwa mafuta yanayosabibisha magojwa ya uvimbe na kolestrol mbaya mwilini na mafuta mengine ya mimea ambayo yamesafishwa kiwandani na kuondolewa virutubisho vyake vyote vya asili.

attachment.php

BIZARI

Bizari au manjano, kama inavyojulikana na wengine, ni miongoni mwa viungo vya mboga ambavyo huzuia utengenezaji wa mawe kwenye figo. Pendelea kutumia bizari kwenye mboga kwani utafiti unaonesha kuwa kiungo hiki, ambacho kina kiwango kingi cha madini ya kashiamu, kina uwezo mkubwa wa kutoa kinga na kuzuia magonjwa ya uvimbe, likiwemo la utokeaji wa mawe kwenye figo. Pia husadia sana usagaji wa chakula tumboni.

Mwisho, wakati ukizingatia ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu katika kutoa kinga au kupambana na mawe kwenye figo, jiepushe na ulaji wa sukari nyingi na ulaji wa vyakula vya kusindika, kwani hivyo ndivyo huchangia kwa kiasi kikubwa matatizo haya. Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba, chukua tahadhari mapema kabla ya hatari.

Attachments

  • oliveoil_.jpg
    oliveoil_.jpg
    14.3 KB · Views: 1,410
Mkuu tiba ya mawe nafkiri itategemea na namna jiwe lilivyokuwa formed nikimaanisha component ya jiwe lenyewe. Mfano; chanzo cha jiwe inaweza kuwa excess calcium, oxalate au uric acid. Hii tiba yako haijaeleza ni aina gani ya stone inatibu.

Hebu soma hapa.

Types of kidney stones include:

Calcium stones.
Most kidney stones are calcium stones, usually in the form of calcium oxalate. Oxalate is a naturally occurring substance found in food. Some fruits and vegetables, as well as nuts and chocolate, have high oxalate levels. Your liver also produces oxalate. Dietary factors, high doses of vitamin D, intestinal bypass surgery and several metabolic disorders can increase the concentration of calcium or oxalate in urine.
Calcium stones may also occur in the form of calcium phosphate.Struvite stones. Struvite stones form in response to an infection, such as a urinary tract infection. These stones can grow quickly and become quite large, sometimes with few symptoms or little warning.

Uric acid stones.
Uric acid stones can form in people who don't drink enough fluids or who lose too much fluid, those who eat a high-protein diet, and those who have gout. Certain genetic factors also may increase your risk of uric acid stones.

Cystine stones.
These stones form in people with a hereditary disorder that causes the kidneys to excrete too much of certain amino acids (cystinuria).

Other stones.
Other, rarer types of kidney stones can occur.
Mkuu Chenge asante sana kwa kuchangia mada yangu ninakushukuru hii tiba yangu inatibu mawe ya aina yoyote yaliyomo ndani ya figo ili mradi iwe ni jiwe tu litatoka inshallah ukitumia hii Dawa yangu.
 
Lakini ugonjwa huu pia husababishwa na bacteria through the urinary tract kama hawatatibiwa kwa muda mrefu mmoja wa hao bacteria ni Proteus mirabilis siyo lazima iwe source itokane na vyakula pekee yake
 
Back
Top Bottom