Nimeamua kuanzia leo niwapatie mawazo ya Biashara na namna ya kufanya biashara kwa wale wote wenye mitaji lakini hawawezi na hawajui wafanye biashara gani,nitatoa ushauri huu bure ila kwa yeyote atakayefanikiwa kupitia ushauri wangu si mbaya nami akanikumbuka kwa chochote.
Ushauri huu ni bure kabisa,utanikumbuka mara baada ya kufanikiwa haya karibuni wakuu.
Wakuu msiwe wagumu wa kuelewa kiasi hicho,biashara zipo aina tofauti na mitaji pia haifanani,kwa hiyo siwezi kuelezea kila aina ya biashara hapa na mtaji wake,unachotakiwa kufanya ni kuni pm kisha unaniambia mtaji wako kiasi gani na ungependa kufungua biashara gani,mimi ndo nakushauri kama wazo lako lipo sahihi au unatakiwa ufanye biashara gani kulingana na mtaji wako,na pia nakufundisha na namna ya kutunza pesa ili uelekee kwenye mafanikio,sasa nikianza kuelezea tu bila kutofautisha biashara na mtaji wa mtu wengi hamtanielewa,kwa mfano kuna mtu ana mtaji wa sh 500,000 hajui afungue biashara gani,na kuna mwingine ana mil 10 naye hajui aanzaje sasa ushauri kwa hawa wote unatofautiana sana maana mitaji yao hailingani hata kidogo,sasa hapo ni vigumu kuweka kiwango kimoja ktk ushauri,na mwingine ana mtaji wa laki 2,ushauri lazima utofautiane,nadhani nimeeleweka.