Katika Mashindano ya mchezo wa kuogelea huko Budapest, Anita Alvarez wa Marekani alizama chini ya swimming pool.
Akitazama huku na kule na kugundua kuwa Anita alikua ndani ya maji muda mrefu sana, kocha wake, Andrea Fuentes mara moja akaingia ndani ya maji na kumuokoa. Anita alikuwa amepoteza fahamu na hakuwa na uwezo wa kujisaidia kwa njia yoyote ile.
SWALI:
Unapokuwa chini kwa muda mrefu sana, ni watu gani ambao watakutafuta, watagundua, na kuzama ndani ili kukuvuta juu unapopoteza nguvu zako za kuogelea?
Ni watu gani ambao wako tayari kufanya hivyo kwa ajili yako?
Na je, una mtu/watu wanaoweza kukutegemea wewe kuwa mtu huyo ambaye ataweza kwenda kutazama na kugundua wakiwa chini kwa muda mrefu sana kwenye maji haya yenye misukosuko tunayoita MAISHA?