Una namba ya simu ya nani ambaye hutakaa uisahau?

Una namba ya simu ya nani ambaye hutakaa uisahau?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Hii inatokana na umuhimu wa mtu huyo au watu hao kwako..

Mwenzenu toka mwaka 2004 nikiwa bado primary school, enzi hizo tunatumia simu za kukoroga (za Ttcl), kama hii pichani

Screenshot_20230411-220113.png


Mwenzenu hapa ndio niliweza kuiona namba ya simu ya Kaka yangu ambapo baba mdogo alikuwa akimpigia mara kwa mara.

Ile namba niliikariri haraka sana baada ya wiki na mimi chautundu nikaenda kuipiga kwa uangalifu wa hali ya juu nikiwa na hamu ya Kuongea na simu😅😅😅😅

Kweli bwana ile namba iliita, nikasalimiana sana na bro, mpaka wa leo hio namba iko kichwani..

Brother toka mwaka 1999 hajawahi kubadili namba ya simu hadi wa leo.

Vipi wenzangu una namba gani muhimu ambayo hata ukiamshwa saa nane usiku unaitaja bika shida?
 
Obvious yule x ambaye alikukumbusha kwamba hujui kama hujui
 
Mwajuma Kinong'o. Mtoto anajua kutiana yule mpaka basi. Mwepesi unaweza mkunja kama kambare na haumii.

Hata uniamshe saa 8 ya usiku namba yake ipo kichwani.
 
Mm nakumbuka namba Kama 50 hivi wengi wao ni wa muhimu but Kuna Hawa makenge
074664-32
065733-10
06598-767
Sijui umuhimu wao na Kama mpo humu ndani futeni hizi namba kichwani
 
Umetisha sana.
kuna mijitu mingine ni ya muhimu kweli lakn kutwa kuchwa kubadili namba
Ipo hivi! Hata marafiki zako wakati mpo the same level of life mnapendana Sana, wengine wakifanikwa zaidi wanabadili namba
 
Nina namba ya Ex wangu. Yaani ule mchezo wa kufuta namba na kusevu. Ku block na ku unblock nikajikuta nimeshaikariri.
Wewe ni mimi kabisa, kuna muda anakuudhi unaamua kufuta namba yake. Halafu baadaye unagundua umefuta kwenye simu lakini kichwani ipo sana tu, unaamua kuisave tu.
 
Nina namba ya Ex wangu. Yaani ule mchezo wa kufuta namba na kusevu. Ku block na ku unblock nikajikuta nimeshaikariri.
we ndo kama mimi, mwisho wa siku nimeamua nisi isave tu nnayo kichwan
 
Back
Top Bottom