Una ndoto gani unayotamani kuitimiza mwaka 2023?

Ni kumuomba Mungu akupe watu sahihi katika maisha yako, watu waovu hawakosekani ila pia katika ngazi ya mafanikio huwezi kila siku ukapanda peke yako bila msaada wa wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Mungu anapanga
2. Shetani anapanga
3. Binadamu anapanga
Utakuwa una jambo zuri lkn ukishawambia watu wanakukatisha tamaa, shetani anaingilia hapo. Kitu usichokijua binadamu tunatenda dhambi Mungu na dhambi ni kama mafuta na maji.
Ni ulimbukeni sana kila mipango unawaambia watu. Unataka kununua kiwanja unawaambia watu, unataka kufanya hiki unawambia watu, mipango yako yote unawambia watu. Utakwama. Mungu au shetani hupitia kwa watu.
Unataka kununua kiwanja waambie watu kuna ndugu yako au rafiki anahitaji kiwanja chenye sifa hii.
Unabiashara yako, anakuja mtu anakuuliza unafanyaje biashara mpk kupata wateja basi unamueleza yote, utakuja shangaa huyo huyo uliyemwambia kafungua hapo hapo karibu yako na anauza bidhaa hiyo hiyo tena bei ya chini kuliko yako.
 
Amina! Mapambano lazima yaendelee. Ukawe wa heri na kwako pia!!
 
kwamba unamaanisha Mungu akupangie kununua Kiwanja halafu mtu amzuie Mungu kwa maneno yake??

Si ndio unacho maanisha??

Kama ni hivyo Acha imani potofu.

Ishi na msemo wa mtaani "kama ipo, ipo tuu"
Soma hii hapa chini
 

Soma story hii hapa chini
 
1.Kununua magari mapyaa sio used hata moja kati ya haya

(i) Genesis GV80 ya 2022
(ii)Volvo XC90 ya 2022
(III) Range Rover Velar ya 2022
(iv) Mercedes Benz S class ya 2021
(v) BMW 7 series ya 2022
(vi)Audi A8 ya 2022
(vii)Infiniti QX80 ya 2023
(viii) Tata Nexon ya 2022
(ix) Genesis GV70 ya 2023
(x) Mercedes Benz GLE coupe ya 2022
(xi) BMW X7 ya 2022
(xii)Honda Accord hybrid ya 2022
(xiii) Genesis G90 ya 2023
(xiv)Ford Ranger ya 2022
(xv) Volkswagen Arteon ya 2023
(xvi) Jaguar XJ L ya 2023
(xvii) Jaguar XF ya 2022
(xviii) Volvo S90 ya 2023
(xix) Lexus LS ya 2022
(xx) Volkswagen Atlas ya 2022
(xxii) Range Rover Sport SVR ya 2022

2. Nijenge Mansion yangu Kisongo, Arusha iliyo na
- Gym
-Spa
-Basketball court
- Swimming pool
-Game room
- Big Walk in closet like a boutique near Master bedroom
- Cinema Room( Home Theater) using Laser tv
- 5 self contained bedrooms and 8 bathrooms
- Two modern kitchen ( one open kitchen and another one chef kitchen)
- 3 Lounges
- Laundry room
-Home Bar
- Outdoor kitchen for BBQ
- modern home garage like a showroom with a carwash

3.Ninunue apartment kati ya Masaki au Upanga kwa safari za kibiashara na mapumziko


4. Niende kutazama mechi ya ligi kuu England live ndani ya Old Trafford

5 . Ninunue ardhi kubwa maeneo tofauti nianzishe kilimo cha umwagiliaji cha soya beans na poa nifuge kuku wa kienyeji kwa wingi kwa soko la hotel kubwa kubwa

6.Nijenge Warehouse tatu mkoani Pwani( Kibaha) ili mchele, mahindi nitakaonunua kwa wakulima na soya beans nayolima nifanye parking kabla ya kuuza ndani na nje ya nchi.( Hasa soya beans kwa Asian market is 🔥)

7. Nijenge nyumba 3 za kisasa za kukodisha hasa kwa wazungu Arusha (Airbnb)

8.Ninunue Treasury bonds BOT kwa Miaka 25, niweke pesa fixed account, bonus account nk

Nikishindwa mwaka huu nitashukuru Mungu na pia nitamwomba Mungu anipe uzima na afya tele ili mapambano yaendelee mwakani 🙏
 
Mungu akutimizie malengo na ndoto zako mkuu. Ndoto zako zimefanya nijiulize kweli hapa duniani kwa umri huu nacheza au vipi. Ila all in all naamini wakati wa Mungu ndio wakati sahihi kila ndoto itatimizwa kwa jina lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…