Una ufahamu gani juu ya Shamba 17 (Farm 17) la Wilaya ya Nachingwea?

Una ufahamu gani juu ya Shamba 17 (Farm 17) la Wilaya ya Nachingwea?

ingekuwa vyema kama ingependekezwa rasmi kuwa eneo la kihistoria na kuwekwa taarifa mbalimbali za kipindi cha harakati za kupigania uhuru kwa nchi za SADC...

Tatizo maeneo kama hayo yanasahulika taratibu na kubadilishiwa matumizi ivyo kupoteza uhalisia wake... kama mazimbu, morogoro.
na kongwa dodoma ina hitaji kupewa uangalizi
 
Kongwa ndiyo sehemu kunakojengwa Kituo cha Kumbukumbu za Ukombozi wa Bara la Afrika, kwa hiyo, hilo halina shaka
 
Aende mtu akatengeneze video ya aiweke ypu tube watu wengi wakiona na kelele zikisikika viongozi wanaweza kufanya kitu aione milladi Ayo
 
Uzi umenikumbusha mwaka 1976 - niliishi Farm 17 kwa miezi kadhaa nikiwa JKT (kwa mujibu wa sheria) operation Mapambano!
 
Kuna General Mmoja aliitwa Muhidin Kimario. Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele. Ndio alikuwa mbabe wa hayo makitu I guess
 
Baba yangu mzazi - Bwana Fanuel Mgendi, alikuwa jeshini Nachingwea, bahati mbaya sikumbuki kuelezwa alikuwa kambi ipi. Mada ya Kambi ya Nachingwea inanikumbusha historia fupi ya mpaka kufika Nachingwea kambini.

Siku moja mwanzoni hivi mwa Novemba 2007, tukiwa nyumbani Dar es Salaam, aliulizwa: wewe mtu wa bara huko, ilikuwaje ukaja kufanya kazi baharini huku?

Baba akaanza kusimulia:

Mnamo mwaka 1964 palitokea maasi ya kijeshi. Kwa hiyo serikali ikaona iboreshe mchakato wake wa kuwapata watu wa kujiunga na jeshi. Ikatangazwa nchi nzima wanatafutwa vijana wenye sifa kadhaa, mojawapo ikiwa ni uzalendo ulitukuka 😉 Kijana Fanuel naye alikuwa mmojawapo wa waliochaguliwa kujiunga na jeshi.

Alipofika jeshini, akaambiwa achague: kuingia jeshi la anga ataenda mafunzo Kanada; akijiunga na jeshi la maji ataenda mafunzo Urusi.

"Urusi si ndio kule nchi ya Lenin, muasisi mwenyewe wa mapinduzi ya Ujamaa?" alituambia ndio ikawa kigezo cha yeye kuchagua kwenda kusoma Umoja wa Kisovieti.

Fanuel_at_Poti.jpg

Januari Mosi, 1965. Fanuel akiwa mji wa Poti, Umoja wa Kisovieti.


Alipomaliza mafunzo ya jeshi la majini nchini Urusi, alirejea Tanzania.

Wakati huohuo, mpango wa Tanzania kupata manowari ulikwama. Hii ilitokana na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ujerumani Mashariki. Nyerere alikataa kupangiwa cha kufanya na Wajerumani-Mashariki (nadhani walimwambia avunje uhusiano na Ujerumani Magharibi), hivyo Ujerumani Mashariki ikasusa kuleta manowari.

Hapo Fanuel na wenziwe wakapelekwa jeshi la nchi kavu, kambi ya Nachingwea.

Baada ya muda kupita, wakuu wa jeshi waliwaambia wachague iwapo wanataka kubaki jeshini au kuacha. Bwana Fanuel akaamua kuacha. Baadae alijiunga na kampuni ya meli ushirikiano kati ya China na Tanzania (Sinotaship) mwishoni mwa miaka ya 1960 akiwa fundi melini. Baada ya kufanya nao kazi, akahamia Mamlaka ya Bandari (Tanzania Harbours Authority) kama ilivyokuwa ikijulikana wakati huo, na kuwa fundi pale kwenye karakana ya meli (Dock Yard) alikofanya kazi mpaka kustaafu, akizoeleka kwa jina lake la Mzee Mgendi au majina mengine kama vile:
Mzee Kibandawazi (mwaka 1980 alipata kumiliki gari aina ya kibandawazi); Mzee Kidumu (alipenda kibwagizo cha 'Kidumu Chama Cha Mapinduzi'); Kizee cha Mungu (alipenda kujitaja hivyo yeye mwenyewe). Alifariki mnamo Novemba 17, 2007.

FanuelMgendi.jpg

Fanuel Mgendi (1939 - 2007) a.k.a Kizee cha Mungu.


kibandawazi.jpg

Kibandawazi (CHANZO: http://vw-store.com . Last accessed on February 23 2012.)
 
Back
Top Bottom