Unaambiwa ya msimu ujao utaiona Afrika

Unaambiwa ya msimu ujao utaiona Afrika

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
UNAAMBIWA

SIMBA ya msimu ujao utawaona watu kutoka UGANDA, KENYA, CONGO, SENEGAL, ZIMBABWE, IVORY COST, GHANA, MALI n.k. inshort utaiona AFRIKA.

YANGA ya msimu ujao utawaona watu kutoka CONGO, inshort utawaona kina Fally Ipupa, Ndama mutoto ya Ng'ombe, Kifaranga mutoto ya Kwiyo n.k.

Unaambiwa,
Yule Peter Banda katika on target mbili anazozipata, basi huwa anafunga goli tatu. Aliwahi kufunga goli siku moja kabla ya mechi yenyewe.

Ingia YouTube andika "Peter Banda tongue dribbling" utaiona Clip yake akiwa ana drible mpira kwa kutumia ulimi baada ya miguu yake kuchoka.

Unaambiwa,
Kuna huyo Duncan Nyoni sasa, watu aina yake Duniani wamebaki watatu. Messi, Pulisic na yeye.
Unaikumbuka ile Penati aliyoipiga kwa goti kwenye michuano ya Afcon?
Huyu ndio yule jamaa akibaki na kipa kama anapiga alafu anafinya kwa ndani kisha anachukua anaweka WAAH!.
Kuja kwa huyu jamaa hatutamsahau Chama na Miqquison tu, tutamsahau hadi mzee Mpili.

Unaambiwa,
SAKHO huyo Veepeee?
Unaambiwa huyu Sakho Club aliyotokea mashabiki wamelia sana na kuilaumu timu yao kumuuza. Sio wamama, wababa hadi watoto wanalia. Viongozi, wachezaji wenzake na benchi la ufundi wamegoma kufanya mazoezi wakidai kwanini ameuzwa.
Wasenegali wanaimba "UMETUACHA IMARAA SENEGALI SALAMAA"

Unaambiwa, Anapiga shuti Tabata mpira unadundia Kawe unaenda kuokotwa Mbagala.
Aliwahi kupiga shuti mtambaa wa Panya ukapinda.
Huyu ndio Sakho original, yule mama dou Sakho liver walipigwa


IMG-20210814-WA0077.jpg
 
Mpira hauchezwi chumbani hao wacongo wataonekana uwanjani na hao wakina sakho pia wataonekana uwanjani
 
UNAAMBIWA

SIMBA ya msimu ujao utawaona watu kutoka UGANDA, KENYA, CONGO, SENEGAL, ZIMBABWE, IVORY COST, GHANA, MALI n.k. inshort utaiona AFRIKA.

YANGA ya msimu ujao utawaona watu kutoka CONGO, inshort utawaona kina Fally Ipupa, Ndama mutoto ya Ng'ombe, Kifaranga mutoto ya Kwiyo n.k.

View attachment 1895147
Umeandika utani unaofanana na ukweli kwenye paragraph mbili za kwanza.

Azam nao walistahiki kusajili wachezaji toka kwenye nchi zote ambazo ving'amuzi vyao vinauzwa ili wajiongezee mvuto.
 
Wamatopeni safi sana kuleta nyuzi kama hizi maana nasubiri league ianze hapa tuwanyooshe vizuri na watu wenu wa kuokota okota huko Africa Magharibi.

Msimu uanze walahi! Hakika msimu uanze!
 
Nilipoona Veepee nikaacha kusoma, nikajua ni walewale wa kwa mpalange
 
Back
Top Bottom