Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
Do you believe In Witchcraft? Share you Experiences
Wasalaam,
Years ago in life movements, huko Songea katika harakati za msaka tonge, kama ilivyo silka ya Mwanaume kula kwa kutafuta Japo hata Tunda huliwa kimasihara lakini hutafutwa.
Binafsi yangu sijawahi kukumbana na Kioja chochote wala dhahama ya Uchawi Licha kutokea Tanga ambako kuna sifika kwa Uganga,Ulozi na Vioja vya Majini makata wa Subiani.
Zaidi zaidi nilipata kushuhudia tu wengine wakikumbana na dhahama na Ghilba chafu za Walozi, Binafsi ata kuchanjwa sikuwahi ,. nadhani ni kwasababu ya Taratibu na Miiko ya Nyumbani kwetu si vile Mwajua Tanga, nyumba sheikh, Nyumba Mganga, Nyumba Binti Mrembo basi hapa mimi nilitoka ile nyumba ya Masheikh kwetu Uchawi na Uganga ni Shiriki ,shiriki ambayo kesho kwa Allah kiama nitakosa msamaha wake wa kunisitiri katika Pepo na Neema Zake.
Tanga nlipata kushuhudia machache kama, siku moja nakumbuka nilipata kumwona Mama Mmoja ambaye alirogwa na Walozi mpaka akafikia hatua ya Kuwa kipofu hali hajiwezi basi mganguzi akawa anatoa uchafu kutoka katika macho yake (nlikuwa nashuhudia) hapa alitolewa vitu vingi machoni, yule mganga alikuwa anaweka mikono yake machoni na kufanya kama kuvuta kitu hivi.
Basi tuliona uchafu mwingi ukitoka ikiwemo Nyasi, Mabakuli, Vumbi, Mawe, Vipande vya Nguo, na Mifupa Just Imagine vyote vilitoka machoni mwa yule mama, na baada ya huduma hiyo maridhawa walao yule mama akaanza kuona japo kwa Tabu Tuliacha huduma Ikiendelea.
Tuachane na Hilo ambalo halikunikuta mimi
Wakati tunatia timu Songea, tulikuwa na Mission kama ya miezi 6 kama sio 7.
Mji huu umejaliwa watoto wazuri wa kingoni na hapa sikupata kumlaumu Msanii Nassibu Abdul alipopata kuwasifu katika ule wimbo wa "kwangwaru" alipopata kuwasifia kwa mjongeo wa viuno vyao, siku mbili tu baada ya kutia kambi hapo nikajiridhisha nalo hilo.
Kabla hata sijapata mahali pa kuishi kila ifikapo jioni nlikuwa siachi kutia timu , viwanja kama serengeti, krister park, La chaz na Vinginevyo kama hivyo na hapa ndipo nilipata wasaa wa kuwatazama vyema. Pongezi kwao.
Basi nlikuwa na Jamaa yangu ambae tulikuwa nae pamoja kwenye mission yetu, tulipata Nyumba Pale maeneo Mfaranyaki kwa wanaokufahamu.
Lakini siku chache tu baada ya kuanza, makazi katika nyumba hiyo tulianza kusikia Dodoso kadhaa kutoka kwa majirani haswa mama mmoja Muuza genge ambaye tulikuwa tunakwenda kununua mahitaji hapo kwa ajili ya madikodiko.
Hapa nami nikaanza kujiuliza Nyumba ile ina mpangaji mmoja tu ambaye alikuwa ni bidada afanyaye kazi benki Pale NMB Songea.
Na ilhali Vyumba vilikuwepo lakini havikupata wakazi na kwa maeneo yale ni ngumu kukosa mtu kwenye nyumba yenye kila mahitaji yote.
Nikaanza kufukua fukua fununu kutoka kwa yule dada kuna nini hapa, kwa hizi tetesi tusikiazo kuhusu hii nyumba. Alijibu kiutani utani kwamba kuna Maudhi madogo madogo ya kidunia ambayo hata hayana Madhara, kisha akatutoa hofu.
Hapa mimi na jamaa yangu tukajipa hope kama binti yule kaweza siye nani tushindwe na ukizingatia sisi watoto wa Tanga, japo imani yetu ilikuwa inajaribu kutufundisha kuwa ingawa binti yule kajinasibu pale labda huko kwao alikotoka aliaga vyema.
Basi ni kama wiki mbili au tatu baada ya kuhamia hapo, hatukukutana na Kisa chochote, Na mpaka wakati huo nilishaanza kupata washikaji kadhaa maana ilikuwa ni faradhi mimi kusakata kabumbu, pale Misufini shule ya Msingi wakati mwingi , ningepandisha mpaka kule uwanja wa Zimanimoto au kule Matarawe.
Na hapa wadau vijana niliozoeana nao pale uwanjani Misufini walishaanza kuniuliza masahibu tunayokumbana nayo lakini bado sikuwa na lolote la kuwajibu, Hatukukutana na lolote bado.
Jumamosi moja mimi na jamaa yangu ilikuwa tuchomoke ,job saa sita hivyo asubuhi tukakusanya Nguo zote chafu , na kuziacha uwani kwa Ajili ya kuja kufanyiwa Usafi Baadae tukirudi.
Hii siku tulitoka sote kwa pamoja nikimaanisha na yule dada ambaye tulikuwa naye mule ndani Pamoja, tukapanda gari ya Huyu binti, akatuacha eneo letu yeye akaendelea na ya kwake.
Mpaka Wakati tunarejea tukakuta hali ya Tofauti kidogo, zile nguo ambazo tuliacha pale zilikuwa zimefuliwa na kuanikwa vyema kwanzia mashuka, mpaka viatu sio hilo tu mpaka uwani na koridoni kulikuwa kumesafishwa vyema tofauti na Tulivyo acha hapa tukesema pengine yule dada kauvaa uhusika halisi wa kike kujishugulisha na yote hayo.
lakini haikuwa hivyo hii ni baada ya kufungua Chumba chetu, arrangement ilikuwa tofauti kabisaa, hapa tukabaki na viulizo
Mpaka wakati anarejea yule bidada tukampa informations ya yaliyojiri akaongeza yeye ashakutana nayo sana inafika muda hali inatulia na inafika muda, vioja vinaanza lakini Ashazoea.
Basi hapa kidogo uoga ukapungua, na kesho yake tu binti yule alikuja kututhibitisha hilo akaja kutuonyesha kwamba Asubuhi aliacha mchele na Mboga (samaki) aliooenda kanisani lakini aliporejea alikuta vimepikwa vyema na Nazi.
Basi zikakatika siku kadhaa usiku mmoja wakati natype data kadhaa za kazini kwenye PC, hapa haikuwa usiku mwingi ni kama saa 6 hivi huyu mwenzangu alikuwa Ashalala, mara nikaanza kusikia vishindo vya mtu akitembea koridoni kwa sauti viatu vya kike( highheels) hapa pengine uningedhani ni yule bidada lakini hali ilidumu mda mrefu sana.
Nikatuma SMS kwa yule dada kujua kwamba ni yeye au kama sio yeye anaskia akajibu vyema tu kwamba yuko macho na anaskia kila kitu, hapo mie nikatoka fasta kukodelea korido lakini sikuona chochote wala sauti hazikuwepo.
Sitaki kusema sikuwa na hofu ilikuwepo lakini sio kubwa na pengine kwakuwa nilishaandaliwa kisaikolojia ya kwamba walozi hao hawana madhara mengine zaidi ya usumbufu tu kama huo.
Baada ya kurejea ndani, ile kukaa tu mara taa ikaanza kujizima na kujiwasha yenyewe na huku sauti ya Socket switch ikisikika kama ilivyo kawaida, hapa nikamstua jamaa yangu ashuhudie kilichotokea mpaka tunalala hali ilikuwa hivyo , na asubuhi mambo yalikuwa kawaida.
Matukio yalikuwa mengi kila mtu akikutana na ya kwake kwa wakati wake kwanzia yule dada na sisi.
Nakumbuka wakati mmoja yule jamaa yangu alinihadithia kuwa alikutana na msichana, mmoja mrefu koridoni (sio yule dada tunaeishi nae)
akawa anaamuuliza
"We wanifahamu mimi"?
"Unaweza kunisaidia kubeba mizigo"?
Hapa jamaa angu alitimua mbio
Siku nyingine tena Mimi binafsi, nlikutana na mikono ya kike ikiwa imenishika isieleweke imetoka wapi yaani hapa mfano mtu awe amesimama halafu kutoka kwa nyuma mikono ije imshike mabegani niliona kucha zilizopakwa Rangi nyekundu nikagundua hilo kuwa ni ya kike.
Matukio yalikuwa mengi mno.
Muda mwingine tukiacha mboga tunakuta zishaandaliwa
Mara tusikie wanawake wakijadili na kucheka kwa sauti koridoni usiku
Mara upishane na wanawake muda wa kwenda chooni
Mara vitu vipite kwa kasi kama nyoka.
Hii nyumba ilikuwa ya don mmoja maarufu wa magari ya Mikoani (Songea to mikoani) inasemekana hapo ndiyo alikuwa ameweka vikolombwezi vyake humo hii ni kwa mujibu wa fununu za walimwengu wa Maeneo hayo.
Kwa wakazi wa maeneo yale watakuwa wanaijua hiyo skendo. Sijui kama hali inaendelea pale au laah kwa maana sisi bado tulimwacha yule Bidada na mara ya mwisho kuwasiliana nae akasema ashamishiwa Njombe.
Ushawahi kukutana na matukio ya ulozi/uchawi
Ilikuwaje?