Unaamini katika uchawi? Tushirikishe uliyowahi kukumbana nayo

Dah af huwa hawakubali kabisa [emoji23][emoji23]
 
Kwa io uo wali Nazi na samaki uliopikwa mlikula au...!!

Kama hamkula mlifanya vibaya ni matumizi mabaya ya rasilimali
hiyo misosi iliyopikwa na jini mlikuwa mnakula au......

hiyo misosi iloyopikwa na jini mlikuw mnakula....
mwanzo ilikuwa inamwaga ila baadae ikawa inaliwa na hamna hata dhara tulilopata
 
Aiseee
 
Yawezekana ni kweli kama alivyosema aliwauzi wengi lakini vile vile mzee inawezekana alifanya yakwake
 
Umenikumbusha kipindi niko Form 5 rafiki yangu alipotelewa na Chupi yake siku 2 kabla ya Shule kufungwa. Tulitafuta sana mwishowe tukachoka tukasema kuna mjanja atakuwa amepita nayo kwenye kamba

Tulienda Nyumbani likizo ndefu kama Mwezi, Shule ilipofunguliwa tumerudi kila Mtu anafungua mazaga aliyopewa na Wazazi Chupi ikaonekana kwenye begi la Classmate wetu. Tulipomuuliza akasema ooh alipofika home aliikuta tuu kwenye begi.

Tulichukua ile Chupi Jumapili tukaenda nayo Kanisani tukamuomba Mchungaji aombeee. Tuliporudi Shule mchana tukaenda jikoni na kuitupa kwenye Moto. Baada ya siku 3 yule Classmate alitoka majibu yenye usaha sehemu za siri hata kutembea alikuwa hawezi

Mpaka leo hatuelewi kwamba alimfanyia Uchawi rafiki yangu kupitia ile Chupi na maombi yalifanya kibao kimrudie yeye au ni nini kilitokea hapo?
 
Uchawi/ushirikina/ulozi/wanga ni story za kusadikika zisizo na ukweli wowote. Story hizi za hearsay zinaaminiwa sana na kuenezwa na wajinga.

NB: ujinga sio tusi
 

Ni mwizi.

Kafanya ngono zembe kapata magonjwa ya zinaa ukizingatia mmetoka likizo.

Coincidence. Nikikwambia nitakuua na baadaye ugonjwe na gari ufe bila mimi kushiriki kwa namna yeyote ile, mimi ni mchawi?

Story zote za uchawi zipo kama yako, huwa zina lots of loopholes; coincidental; can be explained scientifically ila sababu miafrika hatupendi kuumiza vichwa tunakimbilia kusema uchawi; na hata zile ambazo hazina maelezo haimaanishi kwamba ni uchawi labda hatuna majibu yake kwa sasa.
 
Popote pasipo na elimu maarifa na teknologia uchawi ushamiri, uchawi umasikini na ujinga ni pacha.
Huna Kazi nzuri sababu ya elimu nzuri jioni umepewa laptop assignment kwa ajili ya morning call asubui usiku muda wa kwenda kuwanga uutoa wapi hali asubui unatakiwa uwahi foleni usichelewe ofisini.
 
Alipata ugonjwa wa zinaa huyo.
 
Kwa kutumia sayansi tuelezee jinsi nguo zilivyo kua zina fuliwa, switch ya taa kujiwasha na kuzima na kushikwa na mtu usie muona
 
Uchawi/ushirikina/ulozi/wanga ni story za kusadikika zisizo na ukweli wowote. Story hizi za hearsay zinaaminiwa sana na kuenezwa na wajinga.

NB: ujinga sio tusi
Inategemea upo sehemu gani na unafanya nn.
Ushahidi Mimi nachimba madini cha ajabu kifusi kikavu kilichotolewa shimoni kinarejea chenyewe shimoni, chemchem inatoka yenyewe sehemu iliyokavu na kuelekea shimoni,kijiko kikifika shimoni kinakosa nguvu ya kuchimba yaani ukirudi rivas mbali na shimo ni kizima.
 

Nimewekeza kwenye madini hamna cha ajabu zaidi ya story tu za hearsay kama hii yako.
 
Mtoa mada kaanza na swali " Do you believe in witchcraft"?

Maana yake ni "Je Unaamini uchawi"

Kama unaamini share your experience

Hajasema kama huamini utoe somo ambalo ni hakika kabisa mtu anaeamini mambo hayo hatalitia maanani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…