Unaamini katika uchawi? Tushirikishe uliyowahi kukumbana nayo

Niulize kidogo, hiyo misosi mliyokuwa mnaikuta eunhwa vyema na nazi mlikuwa mnakula?

Nimewahi pia kutana na vibwanga ila si kiasi hicho kwenye nyumba fulani ya kupanga huku wiliya ya Kwimba.

Nilikuwa naishi geto peke yangu, kuna siku niliwahi kuamka asubuhi nikatafuta mswaki sioni, nilitafuta chumba kizima kila kona wapi, ikabidi kununua mwingine.

Kesho yake napangua nguo naukuta chini kwenye kona ya begi.
 
Nayatamani maisha yako mkuu wengine ushirikina umetukwamisha sana
 
Nayatamani maisha yako mkuu wengine ushirikina umetukwamisha sana
Jielimishe zaidi.Soma zaidi elimu za nguvu za asili ufanya vipi Kazi.
Mimi mchawi hawezi ni loga.Ili urogwe ni lzm uwe na connections yaani uwe na sababu ya kuruhusu uchawi kukudhuru.Uchawi ni nguvu hasi Kinga ni kuwa na nguvu positive uchawi ni SAwa na umeme umeme haupiti kwenye poor conductors mfano plastic,mbao,mpira,nk mfano ukiwa mshirikina wewe ni good conductor unatafuta vita na wachawi ya kupimwa nguvu.
Muhimu ni kujua nguvu za asili zinavyofanya kazi.Pia ipo mimea inayoneutralize uchawi usikudhuru.
 
kigoma mwisho wa reli ni hatari.
tupo njiani na private car tunamuona mzee barabarani anatembea na bakora yake!
kuna mwenzetu anamfahamu yule babu vizuri sana!

akasema tumpe lift anaelekea njia moja na sisi....lakini babu alishukuru na hakupanda akasema yeye kuna sehemu atapitia hivyo tuendelee!

yule jamaa alituambia huyu mzee huwa hapandi lifti lakini ajabu tukifika mbele tutamkuta yupo!

yani yule mzee alikuwa na uwezo wa kuwa sehemu zaidi ya moja kwa wakati mmoja!

anaweza kuwa kibaha wakati huo huo yupo kariakoo huku yupo kwake buza anakunywa kahawa na kucheza bao!

watu wa kule niliwakubali sana kwa uchawi wao huo!kuna mlinzi mwingine alikuwa analinda TRA yaani anakaba 24/7 usiku ukipita pale unamuona anaota moto!kama unaenda dukani utamkuta pia dukani anakula fegi na kula stori...

kigoma noma sana!
kuna kidemu nilikuwa natoka nacho si unajua sehemu ukiwa mgeni halafu ndugu zako maarufu hapo!unashobokewa.

hicho kidemu na mamake walikuwa wanauza maandazi na afkeki.
nikawa natoka nacho hicho kidemu.stori zikafika hadi kwa ndugu...

hapo kwao walikuwa wanafuga paka wakubwa ndio walikuwa wanakanda maandazi na afkeki...
ila mimi nilikuwa naona kawaida tuu sjui walinilisha lini..

nisingehamishwa kule saivi na mi ngekuwa mchawi...
maana wale nyau walishakuw washkaji wangu mda mwingine wananipigia simu
 
Jamii nyingi zinazojikita kuamini uchawi hubaki mafukura sana
 
Jamii nyingi zinazojikita kuamini uchawi hubaki mafukura sana
Haisongi mbele kwenye kitu chochote. Wabantu wanaamini mambo mabaya kama magonjwa husababishwa na uchawi. Hivyo ili kujiponya wanaenda kuagua na kufanya matambiko. Lakini wamaasai wanaamini magonjwa yanasababishwa na sumu kuingia mwilini/tumboni. Hivyo ili kujitibu wanatafuta namna ya kuitoa, wanatafuta mitishamba(hasa purgative).
Hilo jambo limepelekea wamaasai kuwa wajuzi sana wa masuala ya dawa za mitishamba, huku wabantu wakiwa hawajapiga hatua hata moja katika tiba.

Kisa kingine. Kulikuwa uasi huko Ufilipino. Sasa CIA walikuwa wanajua jamii ya waasi wale wanaimani ya kuwa kuna wanyonya damu. Walichofanya CIA wakawa wanawaua waasi na kuwaning'iniza kichwa chini miguu juu msituni, damu zikichuruzika. Waasi walipoona mambo hayo, moyo wote wa kupigana ukawasinyaa. Imani za kichawi ni adui mkubwa wa vitu vingi sana. Huwezi kupambana na mazingira vizuri kana unaamini sana uchawi.
 
Ilikua miaka ya 2005 kijiji kimoja pande za Kondoa kinaitwa Kidoka nilikua nikiishi kwa Ustadh mmoja ivi mtu wa Kigoma ambae mda mwingi hakua nyumbani alikua mtu wa kusafiri sana

Mbele ya nyumba tuliokua tukiishi kulikua na barabara then kajishamba kadogo na mbele ya hiko kishamba kulikua na Mbuyu mkubwa sana

Story kijijini ni kua huo mbuyu ni maskani ya wazee wa ucku wanakutana hapo na kufanya mambo yao

Nilikua na tabia ya uoga wakati huo kutokana na experience ya mauzauza niliyokua nikiyaona nyumbani Dom kabla ya kwenda hapo kijijini.

Nyumbani kwa huyo Ustadhi nilikuwepo mimi, maustadh wengine wawili (watu wa Kigoma pia) na dogo mmoja (Marehem) na mke wa huyo Ustadh

Kulikua na mlango wa mbele (upande wenye ule mbuyu) na wa nyuma ni upande wa barabara kuu. Upande wa mbele kulikua na choo cha nyasi chenye mlango wa gunia ambacho binafsi nilikua ckitumii ucku, natokea mlango wa nyuma nabaua kwenye majani then narudi kulala

Basi bhana siku ya kwanza kuona mauzauza nilitoka ucku kama kawaida kukojoa nikamuamsha yule dogo tutoke nje. Wakati nakojoa nikiwa nimeface barabarani nikiupa mgongo ule mbuyu, niliona nimemulikwa na mwanga mkali kama wa taa ya gari ukinimulika kutokea nyuma ghafla then ukazima. Nikageuka nyuma kuangalia nikaona kitu kinaruka kuelekea juu ya ule mbuyu kikiwa kimeshika kama kijinga cha moto ivi. Niliamini kua yule ni mchawi alikua kwenye mishe zake lkn akaona kwa kua niko nje bac niutambue upeo wake, nikamshtua dogo turudi ndani fasta

Siku nyingine ucku wakati nimelala nilishtuka ucku nikawa nackia purukushani upande wa ule mbuyu nikaona nichungulie dirishani nione kuna nin. Ile kuchungulia kule mbuyuni namuona mtu akiwa anatoa nuru mwili mzima anafloat kutoka juu ya mbuyu kuelekea nyumba moja ya jirani na ule mbuyu, nikiwa namuona kupitia dirishani bac akafloat alivofika juu ya paa la ile nyumba akazima ghafla ckumuona tena

Visa ni vingi ila naona nisiwachose na ukizingatia mwalimu wangu wa kiswahili hakuhakikisha nimeelewa somo la Ufupisho
 
Aiseee
 
Mibuyu nayo ni miongoni mwa miti amabyo tunaskia habari zake kuhusu walozi kuweka makao yao hapo
 
ilipoishia sayansi ndipo uchawi ulipoanzia in mshana sound Mshana Jr
 
Mtoa mada kaanza na swali " Do you believe in witchcraft"?

Maana yake ni "Je Unaamini uchawi"

Kama unaamini share your experience

Hajasema kama huamini utoe somo ambalo ni hakika kabisa mtu anaeamini mambo hayo hatalitia maanani
Yaani mkuu kama umemaliza kila kitu yaani🀝🀝
 
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
hahaha mswaki ulichukuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…