Kumekua na dhana ya muda mrefu ya kwamba jina analopewa mtu huwa lina athiri haiba yake. Hii inapelekea watu kuwapa watoto wao majina yanayoambatana na watu waliofanikiwa ili wafanikiwe pia.
Lakini pamoja na hayo nimekua nikiona kunabaadhi ya watu hawaendani na majina. Mf. unakuta mtu anaitwa Isaya, ni mwizi, Mohammed ila tapeli au Ronald bangi sana ama Maria mcharukooo.
Wewe unaamini majina yanaathiri watoto kama tunavyoyapa uzito? Kwanini?
Mimi naamini majina hayaathiri watoto kama tunavyoyapa uzito.
Na kama ukisema majina yanaathiri kama tunavyoyapa uzito, Hapo inaweza ikaibuka hoja nzuri kidogo.
Mfano kwenye vitabu vya dini, nyakati zetu kuna watu wana majina ya kwenye vitabu vya dini, ambapo matendo yao hayaendani na yale yaliyoandikwa kwenye vitabu.
Inawezekana tabia walizonazo akina James Delicious ndizo tabia halisi za akina James wa kwenye kitabu.