Unachaguaga lipi, Gazeti la Chini au la juu???!!

JosephElly

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2012
Posts
2,432
Reaction score
1,035
Leo wakati nanunua magazeti niligundua kuwa wote waliotangulia kununua hawakuchukua gazeti la juu. Nikamuomba muuzaji ajaribu kumtolea mteja anayefuata gazeti la juu kabisa, lakini naye akakataa akidai ''aah hili lishasomwaa''
Tukabadili mpangilio na kuyachanganya na bado ishu ikawa ile ile... Hii ni mazoea au? We huwa unachukua gazeti la juu au huwa unachagua chini? ipi sababu yako yakuchagua hivyo?
 
Hivi mpaka leo watu huwa mwasoma magazeti??? washukuriwe waliotuletea internet
 
Hilo la juu tayari limeshasomwa bure na wapita njia hivyo sio jipya kwangu, pia huwa linavumbi, linapauka kuliko la chini ambalo litakuwa safi.
 
Hilo la juu tayari limeshasomwa bure na wapita njia hivyo sio jipya kwangu, pia huwa linavumbi, linapauka kuliko la chini ambalo litakuwa safi.

Yaani hilo ndio jibu walilotoa wengi.. teh teh teh... sasa sijui linaisha utamu au!!!????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…