Unadai huli Kitimoto lakini Sausage unakula

Unadai huli Kitimoto lakini Sausage unakula

Marko 7:18-22
18Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; 19kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. 20Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, 22wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

K.torati 14:8 "Na nguruwe kwa kuwa amepasuliwa kwato lakini hacheui,huyu ni najsi kwenu,msile nyama zao wala mizoga yao msiguse"

Marko 13 "akawapa ruhusa(Yesu), wale pepo WACHAFU wakatoka,wakaingia katika wale nguruwe...."

Najisi+mapepo≠halali

Kwani Hawa bandugu wanasoma hii biblia?wao wanabeba tu.
Kama ni halali ngoja walete andiko

Mwanzo 9:3
3Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa
 
Kiti moto ikitumika vizuri ni sekta itakayoingizia taifa mabilioni ya dola na kufanya T. Shilling kuimarika. Shikamoo kitimoto
 
Unakutana na mtu anadai hali Kitimoto lakini anakula SAUSAGE, si kujidanganya nafsi? Bora uamue mojaaaa

Zipo sausage za Ng'ombe ambazo ndizo zinazopatikana kwa wingi hapa kwetu na hata kwenye vifungashio imeandikwa beef sausages.
Lakini pia zipo za Nguruwe ambazo ziko kwenye supermarkets nyingi maarufu na baadhi ya mini supermarkets ambazo pia zimeandikwa hivyo pia.
Zipo sausages za damu, utumbo, za kuku, mbuzi nn.k lakini zinapatikana baadhi ya maeneo kama mahotelini n.k
Hivi vitu havichanganywi vinapouzwa na hakuna mkanganyiko katika kuvitambua kwani ni makosa kumuuzia mteja kitu ambacho ni haramu kwake sawa na kumlisha nyama ya mbwa,paka mtu asievitumia kwani kuna makundi mengi ya watu wasiotumia nguruwe kama Jews, SDAs, Muslims, na wengine wengi.
Labda utueleze sababu ya madai yako.
 
Kitimoto kimeshuka bei mwezi huu
 
Pizza nazo zinawekwa kitimoto. Ni taarifa tu
 
Watengenezaji wahuni wengi wao wanaandika ni nyama ya ng'ombe but kiukweli ni zaidi nguruwe. Infact, wenzetu wanaojizuia kula kitimoto wanakosa vingi
Dah..,, wapi huko? Huku kwetu nyama ya n g'ombe ni 8,000 na kitu moto ni 13.000 [emoji12]
 
Marko 7:18-22
18Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; 19kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. 20Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, 22wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.

Mwanzo 9:3
3Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa

tatizo kukariri mstari mmoja.
 
YEYOTE ANAEKULA HIYO KITU AJUE ANAKULA MIZOGA. MAPUNDA,MAFARASI YANI NI HATARI SANA HAYO MADUDU.....
 
Nijuavyo zile rolls kubwa ndio kitimoto but hizi nyembamba sio noah product!
 
Back
Top Bottom