Pre GE2025 Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni swali tu la Jumamosi,

Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Swali hili linakuja kufuatia kauli ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Mh. Mongella aliyesema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa kusaka kushika Dola hakuna Kubembelezana.

Sabato Njema.😀😀
 
Walihadaiwa na Samia wakapoteza muda mrefu kuamini kwamba mama ana nia njema.

Wamestuka muda umeenda, kila wanachojaribu hakiendi kuanzia mikutano mpk maandamano.

In short, chadema wamezidiwa akili sana na huyu mama.

Halafu mama wala hatumii nguvu.
 
Nakuunga mkono. Alieharibu ni Mh. Mbowe kwa kutosimamia kile alichokiamini kwa muda mrefu. Kitendo cha kutoka gerezani na kulegea pasi na kupingwa na walio wengi kwenye chama chake, kumeleta shida sana katika kusimamia misingi ya chama chao. Sasa hivi wanahangaika tu, hawajui washike lipi.
Ushauri: Sio vibaya kuanza upya. Wasimamie pale pale kwenye kupata katiba mpya na sisi wananchi tutawaelewa na kuungana nao. Maana ndio tunachokitaka hicho. Katiba mpya itahakikisha misingi bora ya utawala na haki.
 
Wasioposhiriki watapoteza relevancy na ndio utakuwa mwanzo wa kifo cha chama. Hapo watakuwa wamefanikisha lengo la CCM.

CCM imeshawakata makali wananchi. Imebakia CHADEMA tu kumaliza udhia watembee kifua mbere.
 
Walihadaiwa na Samia wakapoteza muda mrefu kuamini kwamba mama ana nia njema.

Wamestuka muda umeenda, kila wanachojaribu hakiendi kuanzia mikutano mpk maandamano.

In short, chadema wamezidiwa akili sana na huyu mama.

Halafu mama wala hatumii nguvu.
Hata bila kuhadaiwa, CHADEMA hawawezi kulazimisha Katiba mpya wala tume huru bila ridhaa ya Rais. CCM ilishawapiga pini Watanzania kiasi kwamba hawana mpango wa kujiunga na mapambano ya kudai mabadiliko nchini.

CHADEMA wanatumainia “people’s power” kufanikisha ajenda zao. Sasa CCM wameshaipiga pini hiyo people’s power. Janja ya CHADEMA imeishia hapo.
 
Ni swali tu la Jumamosi,

Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Swali hili linakuja kufuatia kauli ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Mh. Mongella aliyesema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa kusaka kushika Dola hakuna Kubembelezana.

Sabato Njema.😀😀
Shetani lazima upambane badala ya kumsusia
 
Hata bila kuhadaiwa, CHADEMA hawawezi kulazimisha Katiba mpya wala tume huru bila ridhaa ya Rais. CCM ilishawapiga pini Watanzania kiasi kwamba hawana mpango wa kujiunga na mapambano ya kudai mabadiliko nchini.

CHADEMA wanatumainia “people’s power” kufanikisha ajenda zao. Sasa CCM wameshaipiga pini hiyo people’s power. Janja ya CHADEMA imeishia hapo.
Sahihi
 
Kama chadema inasubiri ridhaa ya rais kupata katiba mpya na bora, na kama unakiri kuwa wananchi wamekubaliana na hali ilivyo Sasa ya kisiasa....basi chadema ifutwe tu.

Kwasabb hatakuja rais yoyote toka ccm akaja akatengeneza katiba bora itakayosaidia kuiondosha ccm madarakani.

Na kama chama cha siasa kimeshindwa kuwashawishi na kuwachagiza wananchi kuunga mkono sera na mitazamo yake basi kifutwe.
 
Hicho chama kimepoteza dira. Hawana wanalosimamia. Mara utakuta wanapambana na kanisa KKKT, mara Diamond Platinumz, na wakati mwingi sana hupambana na Zitto & ACT kwa ujumla. Hawana agenda wanayoisimamia kwa sasa.
 
Hivi hii Katiba mpya ni kwa faida ya Chadema tu au ni kwa Watanzania wote? Maana naona mkwamo wake unaoneka kwa wengine kama ni kuikomoa Chadema.
 
Hicho chama kimepoteza dira. Hawana wanalosimamia. Mara utakuta wanapambana na kanisa KKKT, mara Diamond Platinumz, na wakati mwingi sana hupambana na Zitto & ACT kwa ujumla. Hawana agenda wanayoisimamia kwa sasa.
Hata ccm haina agenda ndiyo maana utaona mwenyekiti wa ccm (rais):-
1. Huyu anakataa mikopo mwingine anapoenda.
2. Mmoja anakataa chanjo mwingine anachukua.
3. Mmoja anazuia mikutano ya vyama vya siasa, mwingine anaruhusu.
4. Mmoja anaua na kuwapora watu wake mwingine hauwi Wala hapori.
5. Mmoja anajenga bwawa la Nyerere mwingine anafungulia maji yanamwagika.
N.k

Kwahiyo ccm ndiyo chama kilichokosa mwelekeo kabisa, lkn kipo kwasabb ya dola na katiba mbovu
 
Ni swali tu la Jumamosi,

Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Swali hili linakuja kufuatia kauli ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Mh. Mongella aliyesema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa kusaka kushika Dola hakuna Kubembelezana.

Sabato Njema.[emoji3][emoji3]
CHADEMA NI matapeli hakuna chama hapo NI kikundi cha watu wanaoisapoti ccm! Walisha pata wanachohitaji wanasahau misingi waliojiwekea inshort NI walamba asali wanapenda nusu mkate
 
Kwahiyo na nyie mnataka kuwa kama CCM? Nyie ni CCM B?
 
Kama chadema inasubiri ridhaa ya rais kupata katiba mpya na bora, na kama unakiri kuwa wananchi wamekubaliana na hali ilivyo Sasa ya kisiasa....basi chadema ifutwe tu.

Kwasabb hatakuja rais yoyote toka ccm akaja akatengeneza katiba bora itakayosaidia kuiondosha ccm madarakani.

Na kama chama cha siasa kimeshindwa kuwashawishi na kuwachagiza wananchi kuunga mkono sera na mitazamo yake basi kifutwe.
Hakina ushawishi? Kifutwe? Na nani? Hakuna mwenye ubavu huo. Hata Jiwe alishindwa. Wajinga walimuaminisha kuwa akihamisha na kutandika risasi baadhi ya wakuu wa hicho chama basi kitajifia chenyewe. Didn’t work.

Siku viongozi wa CCM wakiachana na tamaa ya mikopo/misaada, kula bata, kulundika na kuwekeza maokoto yao ya kifisadi nchi za magharibi, ndipo watakapokuwa na jeuri ya kuifuta CHADEMA.
 
Hata ccm haina agenda ndiyo maana utaona mwenyekiti wa ccm (rais):-
1. Huyu anakataa mikopo mwingine anapoenda.
2. Mmoja anakataa chanjo mwingine anachukua.
3. Mmoja anazuia mikutano ya vyama vya siasa, mwingine anaruhusu.
4. Mmoja anaua na kuwapora watu wake mwingine hauwi Wala hapori.
5. Mmoja anajenga bwawa la Nyerere mwingine anafungulia maji yanamwagika.
N.k

Kwahiyo ccm ndiyo chama kilichokosa mwelekeo kabisa, lkn kipo kwasabb ya dola na katiba mbovu
Namba 5 😂😂😂😂😂😂
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
CHADEMA NI matapeli hakuna chama hapo NI kikundi cha watu wanaoisapoti ccm! Walisha pata wanachohitaji wanasahau misingi waliojiwekea inshort NI walamba asali wanapenda nusu mkate
Inawezekana kabisa 😂
 
Ni swali tu la Jumamosi,

Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Swali hili linakuja kufuatia kauli ya Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM Mh. Mongella aliyesema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa kusaka kushika Dola hakuna Kubembelezana.

Sabato Njema.[emoji3][emoji3]
Wewe binafsi unatakaje? Wasuse? Kuna wakati hata kama umejivika ukada au unatumika, jaribu kuwaza japo kwa kutumia akili.

CCM na serikali yake imehamua kuweka pamba masikioni kuhusu katiba mpya na kuwa na tume huru, kususia uchaguzi maana yake ni kuwachia kila kitu. Sasa huyo Mbowe na Mnyika unataka wafaje?

Haya mambo yanayolalamikiwa na Chadema si kwa manufaa yao tu, ni kwa manufaa ya wanchi na taifa lote, hisipokuwa mmepofushwa na upambe basi endeleeni kujitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom