Well said. Kuna ujinga umeenea sana nchini kufikiri kwamba hilo ni tatizo la CHADEMA. Wajinga wanafurahi kwamba CHADEMA imeshindwa; eti imezidiwa akili na CCM!
Hawaoni kwamba katiba mpya na tume huru ya uchaguzi zitawarudishia wananchi NGUVU ya kuchagua na kuwawajibisha viongozi wao. Hawalioni hilo kabisa! Ni upumbavu wa hali ya juu sana.
Watu wako tayari kuwahakikishia mafisadi wa CCM utawala wa milele bila kujali kuwa hao wezi wamefikia hatua ya kuwadharau kabisa wananchi kiasi cha kutaka kuabudiwa.
Pesa yao inafujwa kwa fujo, huduma za jamii zinazidi kudumaa, ajira na fursa za kiuchumi zinazidi kuwa finyu, upendeleo wa kikabila, kidini, kindugu unashika kasi, n.k. Lakini hawataki nyenzo za kuwawezesha kubadili uongozi. Eti bora zimwi linalotujua! Kama vile hawajui kuwa nchi ina watu wengi sana wenye uwezo mkubwa na vipaji vya uongozi; wengi wasio na majina yanoyovuma katika jamii.
Nchi yenye watu milioni 60+ watu kila siku wanazungumza: Makonda, Mwigulu, Makamba, Ndugai, … and all such trash. Acha nchi ipigwe hadi iingie kuzimu labda fahamu ndio zitarejea!