Pre GE2025 Unadhani kwanini Mbowe na Mnyika wanang'ang'ania CHADEMA kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Tume ile ile ya Uchaguzi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haya 🐼
 
Hivi hii Katiba mpya ni kwa faida ya Chadema tu au ni kwa Watanzania wote? Maana naona mkwamo wake unaoneka kwa wengine kama ni kuikomoa Chadema.
Well said. Kuna ujinga umeenea sana nchini kufikiri kwamba hilo ni tatizo la CHADEMA. Wajinga wanafurahi kwamba CHADEMA imeshindwa; eti imezidiwa akili na CCM!

Hawaoni kwamba katiba mpya na tume huru ya uchaguzi zitawarudishia wananchi NGUVU ya kuchagua na kuwawajibisha viongozi wao. Hawalioni hilo kabisa! Ni upumbavu wa hali ya juu sana.

Watu wako tayari kuwahakikishia mafisadi wa CCM utawala wa milele bila kujali kuwa hao wezi wamefikia hatua ya kuwadharau kabisa wananchi kiasi cha kutaka kuabudiwa.

Pesa yao inafujwa kwa fujo, huduma za jamii zinazidi kudumaa, ajira na fursa za kiuchumi zinazidi kuwa finyu, upendeleo wa kikabila, kidini, kindugu unashika kasi, n.k. Lakini hawataki nyenzo za kuwawezesha kubadili uongozi. Eti bora zimwi linalotujua! Kama vile hawajui kuwa nchi ina watu wengi sana wenye uwezo mkubwa na vipaji vya uongozi; wengi wasio na majina yanoyovuma katika jamii.

Nchi yenye watu milioni 60+ watu kila siku wanazungumza: Makonda, Mwigulu, Makamba, Ndugai, … and all such trash. Acha nchi ipigwe hadi iingie kuzimu labda fahamu ndio zitarejea!
 
Sasa Watanganyika wanazungumzia Goli la Yanga 🐼
 
Inasikitisha sana. Na mtaji wa CCM ni ujinga na umasikini wa Watanganyika ndiyo wanazidi kuifisadi nchi wafaidi na familia zao na kurithishana utawala . Haingii akilini mtu anakula mlo mmoja kwa siku na akaja na kauli eti heri zimwi likujualo akimaanisha CCM iendelee kutawala na anamalizia na kibwagizo eti kwani Katiba mpya itaniongezea sahani ya ugali. Ngoja niishie hapa.
 
Mbowe na Mnyika wamemzunguka Lissu ndio maana lissu kasusa
 
Mambo ya ngawira, shekel, yuan, dinar, euro, ruble aka mapene
 
Uchawa ni laana acheni vijana
 

People's power ya cdm iliisha baada ya Mbowe kumuokota Lowassa yule mzee tapeli wa kisiasa. Alipokuja cdm akawafundiaha siasa za uoga eti ni siasa za kistaarabu.
 
People's power ya cdm iliisha baada ya Mbowe kumuokota Lowassa yule mzee tapeli wa kisiasa. Alipokuja cdm akawafundiaha siasa za uoga eti ni siasa za kistaarabu.
Mkuu jaribu kupunguza hasira kwa Mbowe kuhusu habari ya Lowasa. It wasn’t that bad, really. Hata kwenye uchaguzi wa 2015 mchezo uliochezwa na dola unajulikana. CHADEMA hawakushindwa kwa kura. Na ndio uchaguzi walioperform the best. Kilicho dhahiri ni kuwa CHADEMA walipunguza sana MORAL CURRENCY yao. Lakini mkakati wa uchaguzi hawakukosea.

Halafu hata wewe mwenyewe utakuwa shahidi. CHADEMA bado hawajapoteza people’s power. Hawajapoteza convening power. Wakiitisha mikutano bila hata kutoa vivutio (incentives) kama pesa, pilau, usafiri, n.k. wananchi wengi wanahudhuria. Kwenye chaguzi, wanapigiwa kura nyingi.

Bila shaka uliona jinsi Halima Mdee na timu yake walivyopambana na wavuruga uchaguzi jimbo la Kawe 2020. Mchezo uliochezwa na dola nchi nzima unajulikana.

Kuhusu siasa za mapambano, sidhani kama ingewezekana kwa murderous regime iliyokuwepo awamu ya 5. Wanaodai angekuwepo Dr. Slaa tungeshuhudia CHADEMA ya awamu ya 4 naona wanajifariji tu.

Kama unamchukia Mbowe kwa kushusha moral high ground ya CHADEMA nakuelewa. Lakini si kwa kuipotezea people’s power wala si kwa kuzuia siasa za mapambano.
 
Hakuna chama cha upinzani chenye jeuri ya kukataa pesa za uchaguzi Tanzania hakuna hivi vyama vinapata mgao wa pesa za kampeni na ndio wabane bane humohumo na wao wapate chochote

hiyo jeuri ya kukataa kushiriki uchaguzi wataitoa wapi..
 
Ruzuku tamu
 
Unafikiri kwanini CCM wanatumia mbinu zilezile za 2020 kuharibu uchaguzi???😀🤔🤔
 
Mbowe na myika wamechika labda waachi ngazi tu waje watu wengine
Wamekipooza chame labda wamelamba asali
 

Not for national but personal interests by all means!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…