Ona
Oneni
Fikra zipo nje ya muda, kwa hiyo hata kupima spidi yake ni absurd.
Kwanini? Fikra ni nini? Nadhani tungeaza by definitions, utanipa yako ila yangu ni hii:
Fikra ni mawazo kuhusu jambo Fulani yanayotokea akilini baada ya kitendo Cha kufikiri.
Sasa, Kwasababu fikra ni wazo(idea) tu, basi Haliwezi kuwa na spidi maana wazo(idea) haliexist kwenye physical world Bali lipo kwenye mental/conscious space. ili kitu kiwe na spidi lazima kisafiri kwenye nafasi Fulani (ndani ya physical world) kwa muda Fulani.
Lakini Kwasababu wazo halichukui nafasi yoyote wala halitumii muda wowote basi haliwezi kuwa na spidi yoyote. (Ni sawa na kuuliza huzuni Ina spidi gani? Huzuni IPO kichwani tu haipo duniani physically, haionekani haishikiki)
Lakini Sasa usichanganye fikra na kufikiri... kufikiri kunatumia muda. Kufikiri ni kitendo Cha kutumia ubongo (mental gymnastics, neuronal coordination ,synapses,etc.) Kutengeneza fikra/wazo.
Kwasababu ubongo unafanya kazi kwa kutumia umeme kwenye neurons, na kemikali kwenye synapses basi hiki kitendo Cha kufikiria kinatumia muda na nafasi. Nafasi ikiwa ni ule umbali kati ya neourones zote zinazohusika kutengeneza fikra Fulani, na muda ni ule muda ambao umeme (kwenye axons), na kemikali (kwenye synapses) vinatumia kufika katika hizo circuits ili kutengeneza wazo Fulani.
Hivyo kufikiria kuna spidi maana kunatumia nafasi na muda. Spidi yake roughly tunaweza kuestimate itakuwa chini kidogo tu ya spidi ya umeme Ndani ya free liquid electrolytes. Ambayo kwa udogo wa size ya kichwa chakona ubongo wako unaona ni kama inafika instantaneous. Lakini trust me ungekuwa na kichwa kikubwa kama Dunia lazima ungenotice lag katika kufikiria.
Niwaambie kitu kimoja kwa ambao bado mnataka kulinganisha spidi mazee? Ipo hivi;
Fikra katika spidi hatutaipa namba, tutaipa u 'instantaneous' ambayo kama ni namba basi ni infinity ambayo pia ni sawa tu na ziro.
Hili nmeelezea hapo juu
Yas, spidi ni ziro kwa sababu kiukweli fikra hata haisafiri kamwe. Yaani fikra ikishawazwa mahala A ni muda huohuo hilo wazo lipo mahala B hadi mahala XYZ! Kwa hiyo fikra huwepo ulimwengu mzima mara baada tu ya kuwepo.
Uko sahihi fikra haisafiri, lakini sio kwa sababu hizo. Ni Kwasababu haipo kwenye physical world. Unatakiwa utofautishe kuhusu kitu na fikra kuhusu hiko kitu. Unapofikiria kuhusu Ubungo kwa mfano, fikra hazisafiri kwenda Ubungo na wala hazitoki kichwani mwako, Bali inabaki kama wazo tu ndani ya kichwa chako linalojaribu kuigilizia picha ya real world Ubungo palivyo. Hata details za fikra Huwa ni chache sana (<0.0000000000......00001%) kuliko reality. Mfano jaribu kuwaza kuhusu picha ya tembo(pause kidogo uwaze kuhusu tembo) tayari?.....hapo tayari imekuja picha kichwani ya tembo, lakini najua hujawaza kuhusu mikunjo kwenye magoti yake, umewaza kuhusu weusi wa kucha zake?, umewaza kuhusu unene wa mkonga wake?, umewaza kuhusu ufupi wa mkia wake? Umewaza kuhusu jinsia ya huyo tembo? Umri wake je? Na vipi umewaza mazingira aliyopo? Ni zoo au porini?
Umeiona? Mwanzoni ulitengeneza wazo kuhusu tembo lakini hukuinclude vitu vyote hivyo nilivyotaja, ila ukaendelea kuviongeza kwenye fikra zako kadri nilivyokuwa navitaja.
Nimefanya hivyo kukuonesha tu kuwa fikra zipo tu ndani ya kichwa na wala haziwakilishi asilimia kubwa ya uhalisia. Ni kama rough representation ya ulimwengu ndani ya kichwa chako.
Kama fikra hiyo ina athari kwa mazingira iliyofikiriwa basi tutakachokiona ni kuanza, kuendelea na kuchelewa kwa mchakato wa matokeo ya fikra hiyo. Lakini fikra yenyewe imeshafika pote na katika yote.
Natumai umeelewa ni kweli Fikra haijafika popote Kwasababu haiendi popote. Lakini kitendo kufikiri Kuna Mwanzo, mwendelezo na kuchelewa. Ndiyo maana huwezi kufikiria vitu 8000 kwa wakati mmoja. Vinapeana muda ndani ya working memory yako. Kuna vitu vinatumia muda kufikiria kuliko vingine, mfano ukiulizwa 1+1 utatumia muda mchache kufikiri kuliko ukiulizwa mwaka Jana mwezi huu ilikuwa wapi.
Ndiyo maana FIKRA iliweka wazo la 'UWEPO MWANGA!' Pale palipokuwa na giza na kilichotokea ndio hicho mwanga ukawepo, sema kwa kuchelewa kwa spidi ya mwanga ndiyo maana hadi leo huo mwanga unasafiri katika duara (ever expanding cycle) katika mchakato wa kulibadili giza.
Hapa umeenda kiimani zaidi na Mimi sitacomment, lakini utambue kuwa fikra zako Wewe binaadamu pekee haziwezi kutengeneza kitu chochote kwenye material world. Lakini unaweza kutumia mikono Yako physical kutengeneza kitu kwa kufuata direction ya Ile image kwenye fikra zako.
Mwanga una kasi ndogo kuliko FIKRA/WAZO na ninao uthibitisho wa hili🤔. Uthibitisho upo hukohuko katika kosmolojia na nadharia na majaribio kiasi sikiliza; Inafahamika kwamba hata leo ukianza kukimbia kwa spidi ya mwanga kujaribu kuukamata 'mwanga' wa kwanza katika pembe ya ulimwengu HAUTAKAA UUPATE!....... Tena hata ukifanikiwa kuukimbiza kwa kasi mara kadhaa ya mwanga bado hutaupata! Kwa nini? Ni kwa sababu mwanga huo unakimbia kwa spidi zaidi ya spidi ya mwanga na spidi hiyo inaongezeka (it is accelerating!).
Kitendo cha sayansi kusema spidi ya mwanga ni X, kisha hapohapo kusema tena kwamba kuna 'mwanga' una spidi zaidi ya mwanga na inaonesha inajiongezeka. Ni sawa na kusema kuna 'kitu' kingine kina spidi zaidi ya mwanga huko kwenye ncha ya ulimwengu (ambayo ni sawa na kusema kwenye mwanzo wa ulimwengu🤨. It is the same thing).
Hicho 'kitu' ndugu zangu wala sio mwanga tena. Hiyo ndiyo fikra ya mwanzo na ya mwisho na ya hata sasa. Yaani ya pote. NIKO (kule) ambaye NIKO (hapa pia). Fikra/wazo/idea ambayo imewakilishwa kwa NENO 'LET THERE BE LIGHT'.....
Fikra inayo kasi kuliko mwanga. Na kasi yake ni ukipenda sema infinity, ukipenda sema ziro/sifuri. Maana fikra ikishawazwa katika pointi yoyote ya ulimwengu basi inakuwepo ishafika pote.
NB: Kama nyongeza basi someni Quantum Entanglement. Quantum entanglement inawasiliana kati ya pointi tofauti kwa 'kasi' ya fikra yaani ziro/infinity. Zote hizi ni uthibitisho kiwa kuna 'vitu' vina kasi zaidi ya mwanga.
Okay hapa umeongelea mwanga. Ni kweli hakuna
kitu kinaweza kusafiri
through spacekwa spidi kuliko mwanga.
Hapo nimebold key words. Kitu na through space.
Kinachofanya mwanga uonekane unaaccelerate sio kwamba wenyewe ndiyo unaaccelerate Bali ni space unamosafiria ndiyo inaexpand kwa kuaccelerate.
Ni sawa muwe ndani ya basi pamoja na Usain bolt, ukasema kuwa humu kwenye basi hakuna mtu mwenye spidi kuliko Usain bolt. Hiyo sentesi itakuwa ni kweli. Lakini Hilo basi likianza kutembea kwa spidi kuliko Usain bolt, kwa mtu aliye nje atapona abiria wote mna spidi kuliko Usain bolt. Hata Usain bolt atakuwa na spidi kuliko Usain bolt.
Kwahyo kinachofanYa mwanga kwenye ncha za ulimwengu uoneakane una spidi kuliko mwanga sio kwamba kweli una spidi kuliko mwanga, Bali ni Ile space au nafasi ya huko kwenye ncha za ulimwengu inaexpand kwa spidi kubwa kuliko mwanga.
Ni kweli nothing can travel through space at a speed greater than light, but space itself can expand faster than the speed of light.