Binafsi nakubaliana na Prof. Shivji na nina sababu kuu mbili.
1. Kwanza kabisa ni kwa nini mchakato wa awali ulishindikana kufika mwisho? Sababu ya msingi ilikuwa ni kwa sababu ya kundi fulani waliona kwamba wao ndo wanapaswa kusikilizwa tu. Hivyo wakajitoa na hatimaye kudhoofisha juhudi alizo zianzisha Mzee Kikwete.
Hapa hoja ya msingi kabisa ninkwamba katiba ni maridhiano. Inahitaji kukubaliana. Kuna makundi hayataweza kupata 100% ya wanachokitaka. Hivyo its a give and take process. Sasa kama bado kuna kundi linataka 100% ya kile wao wanachodhani ni sahihi na kiingizwe kwenye katiba bila kujali hoja za mwenzao ni tatizo.
Swali ni je katika huu mchakato mpya yatakuwepo maridhiano? Au utakuwa tena mchakato wa kupoteza fedha?
Hapa ndipo nadhani prof anaona kuna haja ya mjadala.
2. Pili ni dhamira ya makundi mbalimbali yanayo shinikiza katika mpya. Je dhamira yao ni nini? Ingawa wengi wanadai katiba lakini ukweli ni kwamba kila kundi lina dhamira iliyojificha. Makundi haya yanatumia kivuli cha wananchi kudai katiba mpya ingawa nyuma ya pazia wana agenda zao. Kuna wale ambao wanataka katika mpya iwasaidie kuingia madarakani, kuna wale wanataka katiba mpya iendelee kuwaweka madarakani na kuna wale wanaodai katiba mpya isaidie wananchi.
3. Pamoja na katiba ya sasa kuwa na upungufu kadhaa lakini katika awamu ya tano tumeona katika hiyo ikivunjwa waziwazi bila vyombo husika kuchukua hatua. Tumeshuhudia wanao takiwa kulinda katiba wakiisigina. Swali ni je katiba tu inatosha? Hapa ndo dhana ya katiba kuwa si mwarobaini wa matatizo ya watanzania inakuja. Kama tulishindwa kutetea katiba iliyopo hadi ikasiginwa wazi wazi pengine hata tukipata katiba nyingine mtawala atakaye kuwepo anaweza kuosigina vile vile. Hivyo ni muhimu kufikiria zaidi...je tatizo ni katiba?
Kwa hoja hizo tatu nakubaliana kabisa na prof kuwa pengine tatizo hasa si katiba, na tunahitaji kufanyia kazi vitu vingine zaidi. Na pengine hata tukianzisha mchakato mpya utaishia njiani au kuleta sinto fahamu.