Unadhani sababu nyingine za wasanii wasomi kutofanikiwa ni zipi?

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kutokana na ukosefu wa ajira, vijana wengi wanaohitimi shahada mbali mbali nchini hujikuta wakiingia kwenye Sanaa ya muziki

Vijana wenye elimu kubwa ambao wanafanya vizuri kwenye muzika ni wachache mbali na elimu walizonazo.

Robert Kasongo, ni msanii mwenye degree ya ualimu anatamba Mkoani Rukwa, anasema moja kati ya kitu ambacho wasomi wanakumbana nacho kwenye muziki ni maudhui

Wasikilizaji muziki wanataka maudhui mepesi wakati wasomi hupenda kuweka maudhui mazito.

Sababu nyingine aliyoitaja bwana Robert ni kuwa, wanapokuwa wanafanyakazi na watu wanakuwa wanawaza pesa kwanza na kujiona wanajua haki zao, hali inayowafanya mabosi wamuziki kuacha kufanya nao kazi kwa sababu ya usumbufu

Tumesikia wasanii wanaojiona wanajua haki zao wakisema wananyonywa, na baada ya muda wanapotea kabisa kwenye muziki

Wapo vijana wengi wenye shahada wanaofanya muziki lakini hawasikiki, Je wewe unadhani zipi ni sababu Zaidi za wasomi hawa kutofanya vizuri kwenye musiki

Suala la sanaa enzi za wazee wetu ilikuwa ni ngumu sana kulikuta, yaani mtu awe na shahada ya ualimu halafu akaanza kuimba, elimu ilikuwa na hadhi ya kuwa afisa katika ofisi tu

Kipindi hiko muziki ulikuwa ni kwa wasiotaka shule, hali iliyofanya hata baadhi ya watu kuacha shule ili waende kufanya muziki.

Lakini hali imebadilika hivi sasa na watu wengi wenye elimu zao wapo katika muziki na Sanaa nyingine, Sanaa haihitaji elimu bali ubunifu, mbali na watu hao kuingia katika muziki bado kumekuwa na changamoto kubwa ya wasomi hao kupata jina kwenye uwanja wa Sanaa

Ieleweke kwamba kwenye Sanaa wapo waliofika vyuo vikuu na wengine ambao hawakufika hata sekondari, na wanaotamba wengi ni wale ambao hawakufika elimu ya juu.
 
Sababu kubwa ya wasomi wengi kutofanikiwa ni kushindwa kubadilisha elimu walio ipata na kuwa pesa/mafanikio. Na bahatimbaya wasomi wetu wanadanganyika kwamba usomi wao unatosha kujiuza pasipo hata wao kujiuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasomi wengi hawapendi imba nyimbo za kushabikia ulaji/kuliwa tunda kimasiharaaaa...pia hawako karibu na mashabiki ukilinganisha na wasiosoma sana
 
Mimi huwa nawaza kuna vijana wanasoma "arts and media" nk kutoka vyuo vikuu. Hawa watu vyuoni utakuta wanafanyiwa "evaluation" kwa wao kutakiwa kufanya "performances" za kuigiza, kuimba nk.

Kwa hivyo mimi nawaona kuwa ni watu wa sanaa. Cha ajabu sehemu kama "Bongo Movie" imekuwa ikiandamwa na kelele za watu kuwa ipo na kiwango cha chini sana.

Sasa huwa najiuliza hawa vijana huwa wanaenda wapi? Najua sekta nyingi hazifanyi vizuri huku wataalamu wao wakiwa wanamaliza vyuoni kila kukicha, lakini kwa watu wa sanaa naziona kazi zao kuwa za tofauti sana
 
Mafaniko gani mkuu cz hata elimu yao pia ni mafanikio. Uhai wao pia ni mafanikio
 
Kutokana na ukosefu wa ajira, vijana wengi wanaohitimi shahada mbali mbali nchini hujikuta wakiingia kwenye Sanaa ya muziki

Vijana wenye elimu kubwa ambao wanafanya vizuri kwenye muzika ni wachache mbali na elimu walizonazo.

Robert Kasongo, ni msanii mwenye degree ya ualimu anatamba Mkoani Rukwa, anasema moja kati ya kitu ambacho wasomi wanakumbana nacho kwenye muziki ni maudhui

Wasikilizaji muziki wanataka maudhui mepesi wakati wasomi hupenda kuweka maudhui mazito.

Sababu nyingine aliyoitaja bwana Robert ni kuwa, wanapokuwa wanafanyakazi na watu wanakuwa wanawaza pesa kwanza na kujiona wanajua haki zao, hali inayowafanya mabosi wamuziki kuacha kufanya nao kazi kwa sababu ya usumbufu

Tumesikia wasanii wanaojiona wanajua haki zao wakisema wananyonywa, na baada ya muda wanapotea kabisa kwenye muziki

Wapo vijana wengi wenye shahada wanaofanya muziki lakini hawasikiki, Je wewe unadhani zipi ni sababu Zaidi za wasomi hawa kutofanya vizuri kwenye musiki

Suala la sanaa enzi za wazee wetu ilikuwa ni ngumu sana kulikuta, yaani mtu awe na shahada ya ualimu halafu akaanza kuimba, elimu ilikuwa na hadhi ya kuwa afisa katika ofisi tu

Kipindi hiko muziki ulikuwa ni kwa wasiotaka shule, hali iliyofanya hata baadhi ya watu kuacha shule ili waende kufanya muziki.

Lakini hali imebadilika hivi sasa na watu wengi wenye elimu zao wapo katika muziki na Sanaa nyingine, Sanaa haihitaji elimu bali ubunifu, mbali na watu hao kuingia katika muziki bado kumekuwa na changamoto kubwa ya wasomi hao kupata jina kwenye uwanja wa Sanaa

Ieleweke kwamba kwenye Sanaa wapo waliofika vyuo vikuu na wengine ambao hawakufika hata sekondari, na wanaotamba wengi ni wale ambao hawakufika elimu ya juu.
Kama ulivyoeleza hapo, sanaa ni ubunifu, kama kazi yako ni nzuri, bei yoyote utakayoweka itakubaliwa na atakayeipenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom