Pre GE2025 Unadhani "Viti Maalum" vimefanikisha usawa wa kijinsia vya kutosha au kunahitajika marekebisho zaidi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Sheria kama vile zile za viti maalum kwa wanawake ni muhimu sana katika kuhakikisha usawa wa kijinsia kwenye siasa.

Zinalenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika mabunge na halmashauri mbalimbali nchini Tanzania, ambako kihistoria, wanawake wamekuwa wakipata nafasi ndogo katika maamuzi ya kisiasa.

Viti maalum vimewezesha idadi ya wanawake bungeni kuongezeka, na hii imechangia kwa kiasi kikubwa katika sauti za wanawake kusikika.

Hata hivyo, kuna mjadala kuhusu ufanisi wa sheria hizi. Wakati viti maalum vimeongeza idadi ya wanawake bungeni, baadhi wanahoji kama mbinu hii inawasaidia wanawake kuingia katika siasa kwa ushindani wa moja kwa moja, au kama inawaweka katika nafasi ya utegemezi zaidi kuliko kuwajenga kuwa viongozi wenye nguvu na wenye kujitegemea.

Pia, kuna hoja kwamba wanawake kwenye viti maalum hawapati fursa sawa na wenzao wa viti vya kuchaguliwa moja kwa moja katika kujenga misingi ya kisiasa na kuimarisha nafasi zao katika siasa za nchi.

Je, unadhani sheria hizi zimeleta mafanikio katika kutimiza lengo la usawa wa kijinsia au kunahitajika marekebisho ili kuongeza ufanisi wake?
 
Hivyo viti maalum ndivyo vinavyochangia nchi kufilisika na kuwa na madeni yasiyo na sababu.Kwani wanaochaguliwa mara nyingi huwa sifa yao ni urembo tu na si uwezo wa kufikiri.
 
Najaribu tu kufikiria; viti maalumu ni kwa ajili ya kuwaongezea kipato wateuliwa or wapo kwa ajili ya kutetea wanawake wenzao? Labda mimi sio mfatiliaji, naombeni kujua, ni mchango gani wa maana umewahi kutolewa either bungeni pale au mteuliwa mmoja kwamba hu hapa, huyu alitetea wanawake wenzie.
1. Yule binti aliyebakwa na kufirwa, wabunge wanawake walidanya nini?
2. Yule mama wa Iringa aliyefungwa miaka 21 kwa kosa la kukutwa na nyama ya kulisha familia yake, wabunge wanawake walitoa mchango gani?
3. Kuna utekaji mkubwa wa watoto (hapa sizunhumzii wale wa kisaisa cause huko kuna conflict of interest nao ) ambao umeendelea sana hasa mikoa ya kanda ya ziwa na Dar, nje ya wananchi wenyewe kuandamana (mfano kule Simiyu) lini ulimsikia mwana siasa wa jinsia ya kike akisema chochote kuishinikiza serikali ifanye kitu?

Ipo mifano lukuki kuhusu changamoto za wanawake na watoto na hao wabunge hawana historia ya kusema chochote, wali mute (ieleweke, siwazungumzii wabunge wa chama X, hapa nawazungunzia wa vyama vyote ). Kwangu mimi, viti maalumu havina tija yoyote kwa taifa; vingefutwa tu. Nchi iko mbali sana, mikoa ambayo ilikua inalalamikiwa sana kuhusu unyanyasi wa wanawake kwasasa imeisha wahi kumchagua mwanamke kama mbunge wao, Esther Bulaya kashinda mara 2 pale Bunda (nimesema kashinda, sio kutangazwa ) kuna na pia Esther Matiko kule kwa Wakulya kabisa, nae alishinda. Zile sababu kwamba eti wanawake hatuwezi kuwapa kura sisi wanaume, kwasasa hazina mashiko anymore, mikoa/majimbo korofi kwa wanawake wame prove kwamba that was one of the wrong assumptions we had. Tuachane na viti maalumu, havina msaada kwa taifa
 
Sheria kama vile zile za viti maalum kwa wanawake ni muhimu sana katika kuhakikisha usawa wa kijinsia kwenye siasa.

Zinalenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika mabunge na halmashauri mbalimbali nchini Tanzania, ambako kihistoria, wanawake wamekuwa wakipata nafasi ndogo katika maamuzi ya kisiasa.

Viti maalum vimewezesha idadi ya wanawake bungeni kuongezeka, na hii imechangia kwa kiasi kikubwa katika sauti za wanawake kusikika.

Hata hivyo, kuna mjadala kuhusu ufanisi wa sheria hizi. Wakati viti maalum vimeongeza idadi ya wanawake bungeni, baadhi wanahoji kama mbinu hii inawasaidia wanawake kuingia katika siasa kwa ushindani wa moja kwa moja, au kama inawaweka katika nafasi ya utegemezi zaidi kuliko kuwajenga kuwa viongozi wenye nguvu na wenye kujitegemea.

Pia, kuna hoja kwamba wanawake kwenye viti maalum hawapati fursa sawa na wenzao wa viti vya kuchaguliwa moja kwa moja katika kujenga misingi ya kisiasa na kuimarisha nafasi zao katika siasa za nchi.

Je, unadhani sheria hizi zimeleta mafanikio katika kutimiza lengo la usawa wa kijinsia au kunahitajika marekebisho ili kuongeza ufanisi wake?
Vifutwe
 
Nakumbuka malengo yakuanzishwa viti maalum yalikuwa:-
1. Kuongeza idadi ya uwakilishi wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.
2. Kuwaimarisha, kuwapa ujasiri na kuwaandaa wanawake kwa ajili ya kugombea majimboni.

Hilo la pili linadhihirisha kwamba uwepo wa viti maalum lilikuwa jambo la muda tu; na sasa wanawake wanao uwezo wa kupambana majimboni kama ilivyo kwa wanaume.
TUSEME SASA BASI, VITI MAALUM INATOSHA!
 
Back
Top Bottom