IKARAHANSI
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 398
- 479
Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la watu wengi kupinga mfumo dume kwa kusema, eti uondolewe, hawautaki na ni mfumo wa kikandamizaji. Hii imetokana na propaganda za mashirika ya Ulaya na Marekani kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S).
Binafsi nimefanya utafiti na kugundua kuwa baadhi yetu hatujui nini maana ya neno "mfumo" na neno "Dume" kwa wale wanaofahamu baadhi wameamua kujitia wazimu ili wasikose misaada toka kwa "wakubwa wa dunia" na wengine wameamua kukaa kimya na kuacha tukiangamia taratibu.
Kwa maoni yangu "Mfumo dume" ni utaratibu endeshi wa maisha ya binadamu na viumbe hai vingine kasoro mimea. Ni ile hali ya kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu jambo/ mambo yaende vipi.
Mfumo huu ulianzia pale Adamu (binadamu wa kwanza mwanaume) kuumbwa na kuelezwa majukumu na wajibu wake katika hii dunia. baadae alilazwa usingizi na kuondokewa ubavu wa kushoto akapatikana Hawa (binadamu wa kwanza Mwanamke) ili awe msaidizi wa Adamu na siyo mshindani.
Kwa mujibu wa wanasayansi, Mwanaume kupitia mwili wake na bila hiyari yake ndiye anaamua mtoto wa jinsia gani azaliwe na ndiye mwenye kuanzisha utaratibu wa kuendeleza kizazi kwa kuwa wa kwanza kusimamisha tupu yake (Katika haya yote Mwanamke ni msaidizi)
Hivyo basi ieleweke kuwa hakuna hata siku moja ambayo wanaume waliwahi kukaa na kuanzisha kinachoitwa "mfumo dume" bali ni MUNGU mwenyewe.
Ikiwa kuna Mwanaume hatimizi moja wapo ya majukumu ambayo alipewa na MUNGU kupitia Adamu, basi alaumiwe Mwanaume huyo na siyo mfumo. Hatua zichukuliwe kwa mkosaji na siyo kulaumu mfumodume.
Mwenye mchango wa mawazo karibu tuelimishane.