Unaenda hotel unaambiwa ina usalama wa kutosha, je unajisikiaje?

Unaenda hotel unaambiwa ina usalama wa kutosha, je unajisikiaje?

ANTA

Member
Joined
Nov 20, 2011
Posts
66
Reaction score
7
Unaenda hotel unaambiwa ina usalama wa kutosha, unajisikiaje? Na mwonekano wake uko poa, uzio mnene, na security guard akiwa getini. Kwa upande wangu huwa napende kujua
hali halisi ya usalama wa hotel niifikiayo kila ninapokuwa safarini. Lakini huwa nashangazwa ninapoingia chumbani
na kukuta tangazo mlangoni, au karatasi la maelezo mezani kuwa, "ACHA/KABIDHI VITU VYAKO VYA THAMANI PALE
RECEPTION VIKIWEMO HELA, SIMU, LAPTOP NK, HOTEL HAITAHUSIKA NA UPOTEVU WOWOTE" Je usalama
(security state) wa hoteli hiyo utaupimaje? Au kwa nje ni salama, ila kwa ndani hawako salama.


Je? wahudumu ndo tatizo?
Je? wahusika wa hotel wanataka kujua una vitu gani vya thamani?

Maana hata nyaraka tunazokuwa nazo ni za thamani na pengine zaidi ya hela, laptop au sim. Je na hizo nyaraka
tunakabidhi kaunta? maana ni siri na hawatakiwi kuzijua, na mwizi hachagui cha kuiba, na nguo ya ndani je? tuache kaunta? maana nayo ni ya thamani. Jamani nisaidie kuchekecha hiki kitu kichwani ili wenye mahotel watuambie
usalama wa hotel uko wapi? Ni uzio mnene au ni ndani ya vyumba?
 
Usalama wa hotel ni ndani na nje. Wakikwambia wanao usalama wa kutosha ujue wana uwezo wa kujikinga na wezi wenye nia ya kuvamia. Ndo maana wnaweka uzio na mlinzi wenye silaha getini. Ila tatizo la nyumba za wageni ni kwamba uhalifu unaweza ukafanywa na wapangaji waliokodisha vyumba kama wageni kumbe ni majambazi. Hivyo inakuwa vigumu sana kuweza kuweka ulinzi katika kila chumba. Ndo maana wanakushauri ukabidhi vitu vya thamani kwani wanao uwezo wa kuweka ulinzi hapo mapokezi. Kumbuka sio wateja wote wana nia njema, wengine utakuta wamesha kufatilia tangu unaanza safari, wanajua nini ulichobeba. Cha msingi kabidhi vitu mapokezi ila hakikisha wamekupa risiti.
 
majuzi nilikua Tanga wakanichapia walet yenye pesa zangu..kufuatilia kumbe walikua na ratiba yangu ya kuondoka halafu wahudumu wa siku hiyo walikua wamebadilishwa, nimerejea hotelini walet hamuna pesa hamuna..wahudumu wamebadilishwa utabakia huko kwa vilaki tu??? janja yao ndio hiyo..wahudumu wanaiba sana..
 
Back
Top Bottom