Unafahamu 21% ya waajiriwa wanatakiwa kuwa Wazanzibar?

Unafahamu 21% ya waajiriwa wanatakiwa kuwa Wazanzibar?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
HaBari Wakurugenzi!

Kuna mambo ya Muungano wengi wetu tulikuwa hatujafundishwa shuleni lakini kitaa sasa ndio tunajifundisha.

Mfano hili la ajira zinazotolewa na JMT Wazanzibar wanatakiwa kupata mgawo wa asilimia 21 na Serikali ya Zanzibar inaandaa kanzu data na kuhakikisha wale wanaohitimu vyuo wanaajiriwa JMT.

Kiukweli kuna raha sana kuwa mzanzibar yaani ukatae wewe tu shule ajira nje nje awamu hii ya mzee Mwinyi.
 
Ni kwa kila idara au zile zinazohusu Muungano pekee?
 
Muungano huu,mashuleni huwa unafundishwa kwa kuunga unga. Kwa vile walimu nao walifundishwa kwa kuungaunga.

Mtibwa sugar na Yanga sc wanaheshimu hiyo sheria ya 21%
Tena yawezekana Yanga wamepitiliza.
From Canavaro to Frei toto. Hizi timu zinapenda wachezaji wa kizanzibar
 
HaBari Wakurugenzi..!
Kuna mambo ya Muungano wengi wetu tulikuwa hatujafundishwa shuleni lakini kitaa sasa ndio tunajifundisha.

Mfano hili la ajira zinazotolewa na JMT wazanzibar wanatakiwa kupata mgawo wa asilimia 21 na serikali ya Zanzibar inaandaa kanzu data na kuhakikisha wale wanaohitimu vyuo wanaajiriwa JMT.

Kiukweli kuna raha sana kuwa mzanzibar yaani ukatae wewe tu shule ajira nje nje awamu hii ya mzee Mwinyi.
Utter nonsense. Uwakilishi wa asilimia 21 kwa sehemu ambayo hata ukubwa wake haufikii wa mkoa mdogo kama Kilimanjaor? Acheni utegemezi mjenge nchi na kuachana na ujinga na upuuzi wa haki zisizokuwapo wala kustahili.

Mara nyingi nasikia wazanzibari wakisema tuvunje muungano. Hivi bara wakiwatimua watu wenu ambao ni wengi kuliko mliobakia si visiwa vyenu vitazama kwa idadi ya watu? Fikirini kabla ya kudai upuuzi kama huu.
 
Ndio idara ya polisi wamejaa sana
Hivi huo ni9 uiano wa namna gani? Zanzibar hata wakipewa 10% ni sawa. Fanya hesabu mwenyewe. Zanzibar ina 2% ya watu wa TZ, sasa waso watapataje 21% ya ajira?
 
Hapa tulipigwa watu wa bara 21% ni nyingi sana. Bara tupo takribani 60mil. Population ya zanzibar inazidiwa na mkoa wa mwanza. So maximum hawa wazanzibari ni kama 5mil tu tena napo ni kubwa sana.so kwa hesabu ya haraka haraka ilibidi wapate maximum ya 8%. Pekee ya ajira.so hii ina maana kwenye ajira 100 wao wanapata watu 8. Hii ndio sawa.

Na kwanini tusigombanie tu kwa walio compitent wapate kupitia sekretariet ya ajira. Yaani kusiwe na haya ma asilimia
 
Mfano hili la ajira zinazotolewa na JMT wazanzibar wanatakiwa kupata mgawo wa asilimia 21 na serikali ya Zanzibar inaandaa kanzu data na kuhakikisha wale wanaohitimu vyuo wanaajiriwa JMT.
Na kule kwao asilimia ngapi ya watanganyika wanatakiwa kuajiriwa? Vinginevyo wabakie hukohuko haya mambo ya kubebena bebana yametuchosha
 
Ningefanikiwa kuonana na Nyerere swali la kwanza kumuuliza aliwezaje kufuta nchi yake kwa ajili ya Zanzibari? Ardhi ya Tanganyika ambayo watanganyika wangefaidika nayo leo wanafaidika ambao kwako ni kwako ila kwetu ni kwao pia sijawahi kukutana na Mgogo akijitambulisha kuwa yeye ni Mgogo nchi za nje anajitambulisha kama Mtanzania lakini wazanzibari wote wanajitambulisha kama wazanzibari popote Duniani muungano kama unafaida bhasi ni kwa CCM si raia wa kawaida
 
Back
Top Bottom