Unafahamu taarifa zako zipi zipo mitandaoni?

Unafahamu taarifa zako zipi zipo mitandaoni?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
1. Jaribu kutafuta kuona kuna taarifa gani zinazokuhusu katika 'search engines' mbalimbali ikiwa ni za kweli au zinadanganya.

2. Iwapo utakutana na taarifa zisizo sahihi, za kupotosha, au zisizofaa au usizotaka ziwepo, wasiliana na tovuti husika ili kuomba ziondolewe.

Taarifa zako za Kidijitali ni kama alama unazoacha unapotembea kwenye mchanga lakini tofauti ni kwamba taarifa za Kidijitali zinaweza zisifutike na kubaki daima.

Taarifa hizi zinaweza kutumika vibaya kama kuiba utambulisho na kupunguza faragha na siri zako. Aidha, Walaghai wa mtandaoni wanaweza kutumia taarifa hizo kukufanyia ulaghai na kukuibia.
 
Back
Top Bottom