Unafaidika na nini ukifanya mazoezi ya Kutembea au Kukimbia?

Me mazoezi nafanya ila kukimbia mara moja tu kwa wiki, Jumatatu naanza push up, Jumanne na nyoosha mgongo, Jumatano off, Alhamisi squat, Ijumaa push up , Jumamosi kukimbia na kichurachura, Jumapili off mazoezi yote huwa naanza saa kumi moja asubuhi mpaka saa moja kamili nimemaliza
 
Nani alikufundisha mkuu?. Au ulijifundisha mwenyewe?
Hapana mkuu haya masuala lazima upande mtu wa kukuelekeza mwanzo bila instructor siyo rahisi kuyaweza vizuri zaidi utakuwa mtu wa kucheza kata nusunusu na stances za kuiga boss.
 
Kiongozi mwezi mmoja unatosha ku-master zile basic technics
Hapana mkuu haya masuala lazima upande mtu wa kukuelekeza mwanzo bila instructor siyo rahisi kuyaweza vizuri zaidi utakuwa mtu wa kucheza kata nusunusu na stances za kuiga boss.
Mkuu mwezi mmoja unatosha ku-master zile basic technics?
 
Mimi nilianza kukimbia km 4 kila siku asbh kabla ya kwenda job. Nilikua nikimaliza nakua hoi Balaa na nazimaliza kwa taabu sana. Wakati nakimbia kuna watu walikua wananipita na wanaenda umbali mrefu zaid nikawa nahisi labda wanavuta na bangi niliona kama vitu visivyowezekana. Nikaacha kufanya mazoez asbh sana nilikutana na changamoto kubwa ya nyoka asbh wanatoka maporin wanakuja kwenye lami.nikaanza mazoezi jion naendelea nayo mpaka Leo. Nilianza kuongeza km za kukimbia na sasa nakimbia km 23 kila siku jion ktk wiki napumzika siku 3 na nimegundua waliikua wanakimbia zaid yangu hawakua wanavuta bangi Ila ni mazoez ya muda mrefu.

Vitu vilivyonifanya niongeze bidii kwenye mazoez
1. Nina program ya kutrack performance endomondo kila nikimaliza kukimbia najiona kama nimefanya vizuri zaid ya Jana
2. Kuepukana na magonjwa hasa diabates na hypertension ktk ujana huu ukipata hayo magonjwa ujue mkeo ndo ushamtoa sadaka kwa wenzio na pia gharama za matibabu ni kubwa sana na utakunywa dawa mpaka kufa.
3. Performance ktk sex imeongezeka Mara dufu kuna siku baada ya show mke wangu aliropoka akasema kumbe haina haja ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume mazoezi ni tiba sahihi.
4. Mazoez yamenisaidia sana ktk kutumia muda wangu na fedha vizuri badala ya kukaa bar jion na washkaji nakua mazoezin nikurudi nakua hoi. Pesa niliyokua nanunulia bia sasa nanunulia Matunda ya kutosha

Changamoto
Changamoto kubwa ni kuamua kua naenda mazoezini. Kama ni aabh pale unapotoka ktk blanket
 
Ni kweli mazoezi yanasaidia sana,nina mwaka wa pili sasa magonjwa ya kipuuzi yote yamekaa pembeni,No malaria,no typhoid,no hypertension,no back pains n.k am physically ok,tufanye maozezi wadau inasaidia sana,hata kwenye yale mambo yetu,unakuwa vizuri kwakweli...
 
Kama upon fit tupange mechi kidogo kupasha
 
Sie vimbau mbau tusiyo na miili mazoezi yetu ni yapi, maana sisi miili yetu haina stake kabisa full mifupa.
 
Kwa wiki napumzika mara mbili tuu nakimbia kila siku 5km nataka angalau nifikie 6km.
Nilianza na 3km tena kwa kutumia muda mwingi naw maendeleo na speed naviona kukata wese from 82kg to 73kg si mchezo target yangu ni 67kg
 
Ulitumia muda gani kupunguza hizo kg mkuu
 
Ulitumia muda gani kupunguza hizo kg mkuu
Hii ilinichukua kama miezi 4,hili lilifanikiwa pamoja na kuacha baadhi ya vyakula hasa vinavyoongeza mafuta kwenye mwili na hata pombe nilikuwa nakunywa nazo niliachana nazo...
 
Kwa wiki napumzika mara mbili tuu nakimbia kila siku 5km nataka angalau nifikie 6km.
Nilianza na 3km tena kwa kutumia muda mwingi naw maendeleo na speed naviona kukata wese from 82kg to 73kg si mchezo target yangu ni 67kgView attachment 1251824
Pongezi zako mkuu.
Kila kitu kinawezekana penye nia.
Mimi nilikuwa na 88kg na mtu wa kilaji na nyama choma sana.
Taratibu blood pressure ikaanza kusumbua.
Nikashauriwa kubadili mfumo wa maisha.
Nikakacha kilaji na nyama choma,nikaanza kula vizuri kiafya na mazoezi taratibu.
Nilianza mazoezi ya kukimbia kwa tabu sana wastani wa 2Km kwa siku tena kwa shida sana.
Lakini sikukata tamaa.
Nilijibidiisha na kwa sasa nashukuru nimekuwa mkimbiaji mzuri sana.
Nina uwezo wa kukimbia wastani wa 10km bila kusimama kila siku.
Bp iko vizuri sana na weight imeshuka mpaka 74Kg.
Wakati naanza mazoezi ya kukimbia speed ilikuwa chini sana,nilikuwa na uwezo wa kukimbia 1km kwa wastani wa dk7 mpaka 8.
Lakini kwa sasa 1km naimaliza kwa wastani wa dk5 na sekunde kadhaa.
Lengo langu nije nifikie rekodi ya Eliud Kipchoge ya 1Km kwa wastani wa dk 2 na 53seconds...haahaaaaaa!.
 
Mkuu hii unatumia app gani
 

Mkuu hapa naona km unajidanganya anae kimbia anafaida zaid kuliko kutembea maana lengo ni cardio
 
Kwa week mara tatu,na kula jogging saa moja na mazoezi ya hapa na pale saaaafi kabisa,zamani mafua palikuwa part of my life saizi nilishasahau kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…