Pongezi zako mkuu.
Kila kitu kinawezekana penye nia.
Mimi nilikuwa na 88kg na mtu wa kilaji na nyama choma sana.
Taratibu blood pressure ikaanza kusumbua.
Nikashauriwa kubadili mfumo wa maisha.
Nikakacha kilaji na nyama choma,nikaanza kula vizuri kiafya na mazoezi taratibu.
Nilianza mazoezi ya kukimbia kwa tabu sana wastani wa 2Km kwa siku tena kwa shida sana.
Lakini sikukata tamaa.
Nilijibidiisha na kwa sasa nashukuru nimekuwa mkimbiaji mzuri sana.
Nina uwezo wa kukimbia wastani wa 10km bila kusimama kila siku.
Bp iko vizuri sana na weight imeshuka mpaka 74Kg.
Wakati naanza mazoezi ya kukimbia speed ilikuwa chini sana,nilikuwa na uwezo wa kukimbia 1km kwa wastani wa dk7 mpaka 8.
Lakini kwa sasa 1km naimaliza kwa wastani wa dk5 na sekunde kadhaa.
Lengo langu nije nifikie rekodi ya Eliud Kipchoge ya 1Km kwa wastani wa dk 2 na 53seconds...haahaaaaaa!.
View attachment 1286059