The hitman
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 3,673
- 2,288
Yes kukimbia ni kuzuri kwa sababu kuna saidia kuwa na pumziAisee huu uzi ni mfupi unafurahisha ila umeambatana na ukweli.
Napenda sana mazoezi ya kukimbia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes kukimbia ni kuzuri kwa sababu kuna saidia kuwa na pumziAisee huu uzi ni mfupi unafurahisha ila umeambatana na ukweli.
Napenda sana mazoezi ya kukimbia.
Yes uko sahihi mkuu ? Pia uongeza pumzi, cardio ni nini mkuu ?Mkuu hapa naona km unajidanganya anae kimbia anafaida zaid kuliko kutembea maana lengo ni cardio
Hongera bro uko vizuriMimi nilianza kukimbia km 4 kila siku asbh kabla ya kwenda job. Nilikua nikimaliza nakua hoi Balaa na nazimaliza kwa taabu sana. Wakati nakimbia kuna watu walikua wananipita na wanaenda umbali mrefu zaid nikawa nahisi labda wanavuta na bangi niliona kama vitu visivyowezekana. Nikaacha kufanya mazoez asbh sana nilikutana na changamoto kubwa ya nyoka asbh wanatoka maporin wanakuja kwenye lami.nikaanza mazoezi jion naendelea nayo mpaka Leo. Nilianza kuongeza km za kukimbia na sasa nakimbia km 23 kila siku jion ktk wiki napumzika siku 3 na nimegundua waliikua wanakimbia zaid yangu hawakua wanavuta bangi Ila ni mazoez ya muda mrefu.
Vitu vilivyonifanya niongeze bidii kwenye mazoez
1. Nina program ya kutrack performance endomondo kila nikimaliza kukimbia najiona kama nimefanya vizuri zaid ya Jana
2. Kuepukana na magonjwa hasa diabates na hypertension ktk ujana huu ukipata hayo magonjwa ujue mkeo ndo ushamtoa sadaka kwa wenzio na pia gharama za matibabu ni kubwa sana na utakunywa dawa mpaka kufa.
3. Performance ktk sex imeongezeka Mara dufu kuna siku baada ya show mke wangu aliropoka akasema kumbe haina haja ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume mazoezi ni tiba sahihi.
4. Mazoez yamenisaidia sana ktk kutumia muda wangu na fedha vizuri badala ya kukaa bar jion na washkaji nakua mazoezin nikurudi nakua hoi. Pesa niliyokua nanunulia bia sasa nanunulia Matunda ya kutosha
Changamoto
Changamoto kubwa ni kuamua kua naenda mazoezini. Kama ni aabh pale unapotoka ktk blanket
Mkuu jiunge na runners club zitakumotivate sana. Pia tumia app ya strava nzuri sanaKwa wiki napumzika mara mbili tuu nakimbia kila siku 5km nataka angalau nifikie 6km.
Nilianza na 3km tena kwa kutumia muda mwingi naw maendeleo na speed naviona kukata wese from 82kg to 73kg si mchezo target yangu ni 67kgView attachment 1251824
Mkuu tafuta runners club zitakumotivate sana.Pongezi zako mkuu.
Kila kitu kinawezekana penye nia.
Mimi nilikuwa na 88kg na mtu wa kilaji na nyama choma sana.
Taratibu blood pressure ikaanza kusumbua.
Nikashauriwa kubadili mfumo wa maisha.
Nikakacha kilaji na nyama choma,nikaanza kula vizuri kiafya na mazoezi taratibu.
Nilianza mazoezi ya kukimbia kwa tabu sana wastani wa 2Km kwa siku tena kwa shida sana.
Lakini sikukata tamaa.
Nilijibidiisha na kwa sasa nashukuru nimekuwa mkimbiaji mzuri sana.
Nina uwezo wa kukimbia wastani wa 10km bila kusimama kila siku.
Bp iko vizuri sana na weight imeshuka mpaka 74Kg.
Wakati naanza mazoezi ya kukimbia speed ilikuwa chini sana,nilikuwa na uwezo wa kukimbia 1km kwa wastani wa dk7 mpaka 8.
Lakini kwa sasa 1km naimaliza kwa wastani wa dk5 na sekunde kadhaa.
Lengo langu nije nifikie rekodi ya Eliud Kipchoge ya 1Km kwa wastani wa dk 2 na 53seconds...haahaaaaaa!.View attachment 1286059
Ahsante sana kwa ushauri huu mkuu.Mkuu tafuta runners club zitakumotivate sana.
Poa Mkuu, ila natumia app ya AdidasRuntactis ni nzuri pia.Mkuu jiunge na runners club zitakumotivate sana. Pia tumia app ya strava nzuri sana
Uzuri wa strava ni kama ilivyo istagram au fb. unakua na followers pamoja na running groups/clubs. Wanavyokimbia followers wako kila siku Unaona na una uwezo wa kulike na kucomment. Pia unapata updates za upcoming marathon