Kama ulichokisomea unakipenda kweli kweli basi hata ukikosa ajira utatengeneza namna ya kujiajiri ili uweze kukifanya vema.
Mfano, kama ulisomea udaktari ukakosa kuajiriwa muhimbili au kairuki, unaweza kuwa dokta wa majumbani mbona watu kibao wanaumwa majumbani ila wanaokwenda kuwaona na kuwapa msaada ni wachungaji tu madokta hawajatengeneza mfumo.
Muhasibu, kama umekosa ajira ya uhasibu unaweza kujiajiri kwa kuwa auditor wa kampuni private kuwapangia vitabu vyao na mambo ya TRA.
Kama ni mwalimu unaweza fungua tuition center yako.
Kama ni engineer unaweza jiunga na wenzako mkaingia sekta ya ujenzi na kupata kazi kama subcontractors au kusimamia ujenzi wa nyumba za watu soko linauhitaji wa wataalamu wa ujenzi why ukose kazi.
Kama mtu wa human resources unaweza tengeneza kampuni inayodeal human services kama wafanya usafi, mahousegirl, wapishi na kadhalika then ukawa na contract za kuwapa na kuwalipa kwa kuwatafutia kazi kwenye majumba ya watu. Na kadhalika.
So sidhani kama inashindikana wewe kutumia elimu yako ya chuo kwa kujiongeza ingawa ni ngumu mwanzoni especially kama hakuna mtu wa kukuongoza na kukupa directions but ukishasoma codes za mtaa hautaweza kukwama zaidi utafanikiwa kufika mbali.