Unafanyaje ili mteja au client aendelee kufanya kazi na wewe

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888
Unafanyaje ili mteja au client aendelee kufanya kazi na wewe? Ili brand yako ikue ni lazima upate wateja wapya na wateja waliopo waendelee kufanya kazi na wewe.

Huwa natumia hizi njia kumfanya mteja aendelee kufanya kazi na mimi..

Tunatumia gharama sana kupata wateja..!

Tunatumia nguvu sana kupata wateja wapya...!

Mteja au client ni mtu wa muhimu sana, kwahiyo inatakiwa mutumia mbinu mbalimbali ili kumfanya abaki!

Njia ya kwanza ninayotumia ni kumfanya akupatie mawasiliano ya karibu (Whatsapp, telegram, email).

Njia ambayo ni rahisi kumfikia.

Au yeye kukufikia.

Kwahiyo ukibahatika kupata mteja mara ya kwanza, tumia mbinu zote kumleta whatsapp.

Au kwenye contact list inakuwa ni rahisi pia kufanya follow up

Kwa saivi ukirusha tangazo Facebook, Instagram, tiktok

Wanakuwekea options ya kuwaleta wateja au traffic whatsapp.

Hii inamaanisha kuwa whatsap ni sehemu muhimu sana ya kuwa karibu na wateja wako.

Wakifika whatsapp huwa tunawapostia kila siku.

Njia nyingine ya kufanya client abaki na mimi ni

Over deriver, hii nimejifunza kwenye kitabu cha how to win friends and influence people na 48 lows of power.

Mteja ukimfanya aonekane yeye ni bosi atafurahi sana.

Hata kam ni kazi ndogo ukimpa cheo cha kuonekana boss lazima ataendelea kukupa kazi.

Nji ya tatu ni kumuomba kupe kazi nyingine.

Kama ni unamuuzia kitu unaweza kumpatia bidhaa nyingine kwa discount.

Huwa nawapatia offer watej wangu w zamani, inawafanya waone kamawamependelewa zaidi.

Ukiweza toa huduma za kujirudia au zinazotegemeana.

Mfano mteja anayetaka kuanza biashara atanitafuta kwa kazi ya logo na poster, nitamshawishi asajili business name, arushe matangazo, asajili kampuni, atafute reseni, social media.

Zote hizo huduma anazipata kwangu

Kuwa available muda wote kama wewe ni freelancer. Wateja wengi nwapata kwasababu nakuwa online muda wote, nipo active muda wote nikihitajika

Hii inanipa priority kubwa sana client anapofikiria kutafuta mtu wa kumsaidia kazi zake.

Njia nyingine ni hakikisha kila client anakupatia testimonials.

Shuhuda

Shuhuda nyingi zitafanya wateja waendelee kukuamini na kukupatia kazi nyingi.

Shuhuda inamaanisha kazi yako ni nzuri na inapendwa na watu.

Mwisho ni hakikisha unatoa offer mara kwa mara. Offer ndo zinakuletea wateja wapya na kufanya waliopo waendelee kukulipa pesa zao.

Njia ya kutoa offer ni muhimu sana kufanya wateja wa zamani waendelee kukulipa pesa zao

Hizo ni njia natumia sana kupata na kuishi na clients wangu kila siku

Unahitaji kuongeza wateja katika biashara yako? Tuandikie njia unayotumia kwenye coment
 
Aisee mkuu madini mazito na adhimu umedondosha hapa, shukrani sana mkuu kwa darasa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…