'Unafiki' huu sijauzoea japo ni mwana Simba SC tena 'lia lia' kabisa, jana tumecheza 'Mechi Mazoezi' na Green Warriors na Kufungwa je, mbona hatusemi?

Mkuu nimetafuta vyanzo vyote vya habari vya club sijaona hayo matokeo,labda unisaidie kunambia ni chanzo kipi cha habari cha club ulipoyaona hayo matokeo

Shaffih Dauda kupitia Clouds FM Kipindi chao cha Michezo cha 'Sports Extra' jana Usiku Saa 3.
 
Mbona kwenye ukurasa wa insta wa shaffih nimeona matokeo ya Yanga kucheza na Mlandege, pia Azam kecheza na Trans camp, mbona hiyo mechi ya Simba na Green warriors hajapost? Km kweli Simba ilicheza hiyo mechi
 
Uzi huu haupo positive!! Ni kama Kuna jambo ulitaka kulisema lkn umeishia hewani na kubakia unalaumu tu.
 
Uzi huu haupo positive!! Ni kama Kuna jambo ulitaka kulisema lkn umeishia hewani na kubakia unalaumu tu.
Clouds walitangaza Jana mwishon mwa kipindi chao cha michezo, cha ajabu hawakuelezea zaidi, ngapi ngapi, wafungaji nani, Zaid ya kusema Simba huwa hafui dafu, inaonyesha hawakuwa na uhakika
 
Mimi ni 'Mjumbe' tu kama una 'Hasira' nenda 'Kamkwide' Mtangazaji wa Clouds FM Shaffih Dauda kwani ni Yeye ndiye alisema yote haya ile Jana.
Angalia hata manara amekanusha kwamba clouds hiyo habari wamezusha jana simba walikuwa gym hakukuwa na mechi yoyote
 
Angalia hata manara amekanusha kwamba clouds hiyo habari wamezusha jana simba walikuwa gym hakukuwa na mechi yoyote
Simba wanaficha ili isiadhiri mahudhurio ya mashabiki kwenye mechi ijayo, ila ni ukweli walifungwa 2-1
 
Simba jana haikucheza mechi yoyote na timu yoyote ile,,ni habari ya uongo na sielewi imetungwa kwa interest gani!
Asubuhi ya jana tulifanya Mazoezi Gym na jioni tulifanya Mazoezi ya uwanjani.

Very simple,,why hatujaulizwa? Au kuwauliza Green Warriors?
Huku kwetu ktk michezo mtu unaweza kusema na kutangaza lolote lile bila kujali na hakuna hatua za kuchukuliwa.

Wanasimba wala msifadhaike na taarifa za kutungwa,,tunalo ombwe la professionalism na ethics miongoni mwetu,,tuwasamehe maana kujua ulitendalo ni kipaji pia

Muwe na mchana mwema.
 
Kitu ambacho sijaelewa hapa ni kuwa,Je hiyo ilikuwa ni MECHI MAZOEZI au MECHI YA KIRAFIKI?
Kama ni MECHI MAZOEZI haikupaswa kuwa habari na hata huu uzi utakuwa ni matumizi mabaya ya bundle lkn kama ilikuwa ni MECHI YA KIRAFIKI basi naamini platforms zote za Simba wangeiripoti KABLA na BAADA ya mchezo.

Ikumbukwe kuwa mechi mazoezi hizo zipo kila siku timu inapofanya mazoezi ya FULL GAME...kuna nyakati hata SIMBA B (U-20) huwa wakicheza na wakubwa wao wadogo wanashinda au wanatoa sare na hatupewi habari yoyote humu sembuse hii.

Hebu tuwe fair kidogo.... Au kuna jambo unalichokonoa??
 
Basi kama Wao walifanya iwe 'Siri' namshukuru Shaffih Dauda kuiweka 'hadharani' na wana Simba SC hata habari 'mbaya' tuwe tunazisema tu pia.
Wewe unamuamini sana shafih dauda?
 
Nawewe kumbe unaakili za utopolo!!! Simba mnyama hajacheza wiki hii mechi ya kirafiki. Why wacheze mechi ya kirafiki. Manyani yalicheza coz kocha na mpya na haijui timu yake bado. Lile bango linalotrend ni la mechi ya Azam na transcamp watopolo waliedit. Kama shafii naye alihadaika Basi ni utopolo tuu Kama wewe.
 
Mbona kwenye ukurasa wa insta wa shaffih nimeona matokeo ya Yanga kucheza na Mlandege, pia Azam kecheza na Trans camp, mbona hiyo mechi ya Simba na Green warriors hajapost? Km kweli Simba ilicheza hiyo mechi

Kuna Watu huwa mnanilazimisha niwajibuni 'hovyo / kunya' kisha mnalaumu. Nimekuambia nimemsikia Shaffih Dauda akisema Jana. Msinichoshe!
 
Uzi huu haupo positive!! Ni kama Kuna jambo ulitaka kulisema lkn umeishia hewani na kubakia unalaumu tu.

Imarisha Kwanza 'IQ' yako ili iwe inaweza 'Kunielewa' GENTAMYCINE na ukiona sasa ipo sawa na zimetimia 100% rudi tena hapa Kujibizana nami.
 
Clouds walitangaza Jana mwishon mwa kipindi chao cha michezo, cha ajabu hawakuelezea zaidi, ngapi ngapi, wafungaji nani, Zaid ya kusema Simba huwa hafui dafu, inaonyesha hawakuwa na uhakika

Sasa kama hawakuwa na 'Uhakika' nayo kwanini tena 'Boss' wao kabisa Shaffih Dauda 'akasema' huku akiwa 'anafurahia' pia Simba SC Kufungwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…