Unafiki wa balozi wa Kenya Tanzania

Ndugu TX,
Kufuta ulichobandika hapa, ambacho ndicho kinachofanyiwa rejea na wachangiaji siyo ustaarabu maana wachangiaji wanaonekana wazushi!
Rudisha, au omba Mods wafunge mjadala huu.

Mtoa Hoja hapo juu "yako" kaiweka hio article.....au kuna mengine....? Next time mtoa Mada bado akiweka bandiko unachotakiwa ni kumquote..hata kama akifuta qoutation yako itabakia reference...!!!
 

Shangazi, nimekuelewa. Lakini naomba kukuuliza, kama hili la mahakama ya kadhi kinachosumbua ni kodi. Vipi mkataba wa Serikali na Makanisa ambapo Serikali itatoa fedha na upendeleo kwa kusomesha Wakristo, pia itatoa fedha ama kukopa kwa niaba ya Wakristo kwa ajili waendeshe shule na hospitali. Jee hapo ni sawa?.

Pili, mimi nazungumza ama naandika kile ninachosoma. Kama wewe unaniona mdini, haiwezekani wewe usiwe mdini. Manake unatumia kipimo gani kuniona mdini, wewe usiwe na chembe ya udini katika moyo wako. Kuhukumu nitahukumu, hili suala limehusu dini, unataka niseme kuwa hapa kuna ukabila wakati ni udini.
 

Kwani kasema mahakama ya kadhi isiwepo au kasema swala liangaliwe kwa undani zaidi?
 
Hivi jamani humu JF haina mambo mengine ya kuchangia ya kutuletea maendeleo kwa kasi ni mambo ya Udini tuuuu yanachangamkiwa badala ya kuhamasisha maendeleo ya shule, barabara, Umaskini uliokithiri ukitawala???? Tuache udini
 
hakuna pesa yoyote ile ambayo selikali inawapa shule. na shule zenyewe hata selikali ingetoa wanasoma watu wa dini zote including waislam. pia hata kama ingekuwa hivyo, waislam pia wangekuwa na uhuru wa kujenga mashule yao ili wapate nao. zaidi ya yote, hata kama waliingia, wana haki kwasababu mashule yao yalinyang'anywa ili tuchukuliane na watu waliokuwa illiterate kwa kiwango kikubwa. nina maana, tuligawana umasikini au ujinga ili tusome wote. isingekuwa hivyo, basi, wakristo tu ndo wangekuwa wamesoma hadi leo. wengine wangekuwa wafanyabiashara za samaki wa feri wakikaa mbagala, manzese na magomeni. tulifanya hivyo kuwasaidia tu.shukrani hamna?
 
Huyu Mfumwa kweli mfu--------we ulitaka aseme anzisheni mahakama ya kadhi ndo ufurahi? aaahahahahaah! haitatokea hiyo mahakama hata iweje kamanda, we endelea kuchapa kazi badala ya kupoteza muda wako kwa vitu visivo na msingi wowote.

Eti mahakama ya kadhi!!!-----------what is that??????

Rom
 
 
Kwa akili zako unafikiria kuwa hakukuwa na shule za Kiislam zilizo taifishwa!? Hivi mpala leo bado upo na ile ile propaganda ya "hawakusoma hao"
Nyie mlio soma mmelifikisha wapi Taifa hili, kila kukicha linanuka umaskini wa kutupwa? Unataka kunambia kuwa nyie wasomi (!?) Ndipo mlipoifikisha Tanzania hapa tulipo, yaani mnajivunia ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.
 
 
Kazi kweli kweli, mtu katoa ushauri unachotakiwa kufanya ni kuusikiliza na kuupima kama unafaa au haufai kumuita mnafiki hakutobadilisha chochote sana sana kunaonyesha jinsi uelewa wako wa mambo ulivyo mdogo. SMH!
 

,....TUACHE USHABIKI,TUONGEE UKWELI.
KWA MUJIBU MAGAZETI NILIYOSOMA NI KWAMBA BALOZI HUYO ALISEMA MAHAKAMA HIZO ZINALETA KERO HUKO KWAO NA AKASHAURI UMAKINI UWEPO KTK KUJADILI NA KUAMUA KAMA IWEPO AU LA.
Waraka wa MADHEHEBU YA KIKRISTO MBONA UNAJADILIWA NA KILA MTU ANATOA MAONI YAKE NA BADO PANAKALIKA?
Cha msingi kwakuwa wanaotaka mahakama hiyo wapo,waitetee hoja yao na wanaopinga waraka wa wakrito watoe hoja na WAUMINI WAELIMISHWE KUSUDIO NA NAMNA YA KUTEKELEZA MAAZIMIO YATAKAYO FIKIWA.
Ahsante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…