Ndugu yangu,
Nadhani tunachanganya mambo hapa.
1. Kichwa cha habari kinasema "Unafiki wa balozi wa KEnya tz"...Ukisoma mada unashangaa, badala ya kuona unafiki, unaona mtu anatoa ushauri wake kuwa, mkitaka kuanzisha mfanye homework yenu vizuri kwa maana wao ambao tayari wanazo, wanaona changamoto zinazowakabili.
2. Ulishawahi kusikia " best/good practices" that needs to be replicated? Kama jibu ni ndio, basi utakubaliana nami kuwa hakuna haja ya kufanya makosa pale mwenzio alishayafanya.Unachotakiwa ni kuchunguza alikosea nini na wapi na wewe uanzishe chako kwa kurekebisha yale makosa na siyo kuyarudia vilevile.
3. Inashangaza unaingiza udini hata mahali ambapo sio pake.Waraka - ambao ni mawazo ya kundi fulani katika jamii kuhusu suala fulani ambalo hata kikatiba watu wana uhuru kutoa mawazo yao, haifanani na kuanzisha taasis ndani ya mfumo wa serikali ambao watu wa imani zote watawajibika kugharamia kwa njia ya kodi zao.jARIBU KUTOFAUTISHA NDUGU.
4. Usihukumu watu kwa misingi ya dini kwa maana utashangaa utawabandika watu dini ambazo siyo zao!